Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Ratiba ya lishe bora ya kuzingatia nchini Kenya ya mama mja mzito

4masomo ya dakika
Ratiba ya lishe bora ya kuzingatia nchini Kenya ya mama mja mzitoRatiba ya lishe bora ya kuzingatia nchini Kenya ya mama mja mzito

Lishe bora ni muhimu kwa mama mja mzito. ana paswa kula vyakula vitakavyo mpa nguvu na pia mtoto wake mchanga. Zingatia kumpa vyakula bora vilivyo na protini na vitamini kwa wingi.

Ni jambo la busara kwa mama mwenye mimba kujua lishe bora ya mjamzito. Anahitaji kula vyakula ambavyo vitaongeza nguvu kwa mwili. Pia ni muhimu kwani ana maisha ya kiumbe ndani yake. Yeye na mtoto wana hitaji vyakula ambavyo vitawasaidia kukua. 

Ratiba ya mwanamke mja mzito ya kufuata ni rahisi sana na muhimu kuzingatia. Haijalishi mahali ama wakati anapo amua kuzila. Wasaa pia anaokula unaweza badilika lakini azingatie kula vyakula bora. Mama mja mzito ana stahili kupata gramu 100 za protini kila siku.

Ratiba ya lishe ya mjamzito inafaa kuwa na,

Kunde

Vyakula vya jamii ya kunde ni muhimu kwani huwa na viwango vingi vya protini. Mimea mingine kama soya, peas, karanga na maharagwe pia husaidia mama kupata mahitaji yake ya protini.

Mayai

lishe bora kwa mama mwenye mimba

Mama anapaswa kuchukua mayai angalau manne kwa kila wiki. Inasaidia kuupa mwili protini na vitamini A na pia kumzuia kupata maradhi.

Viazi vitamu

Vina vitamini A. Ni muhimu katika ukuwaji wa macho ya mtoto, mifupa na ngozi.

Nyama

Nyama kama vile ya kuku, ng’ombe, samaki, nguruwe ina protini nyingi ambayo mama mja mzito anastahili. Inasaidia katika ukuwaji wa mwili wa mtoto.

Mboga za majani

Kama vile spinach, kabeji na mchicha. Huwa na rangi ya kijani ambayo ina virutubisho vinavyo hitajika mwilini. Zina vitamini A na B.  Muhimu katika ukuaji wa mwili na kutengeneza na kuongeza damu mwilini. Kukosa mboga hizi husababisha mama kupata ugonjwa wa anaemia.

Maji

Maji ni muhimu sana kwa mama mja mzito na pia kwa mwanawe. Inasaidia katika unyonywaji wa chakula cha mtoto tumboni. Pia inasaidia kinyesi chake kutokua kigumu. Mama mja mzito ana paswa kuhakikisha kuwa anakunywa maji angalau litre moja kila siku.

Lishe bora ni muhimu sana kwa mama mja mzito. Hii ni kwa sababu ana maisha ya kiumbe kinachokua ndani yake kinacho mtegemea. Ni muhimu sana kwa mama kuhakikisha anakula chakula cha kutosha na chenye afya. Zingatia lishe bora ya mjamzito wakati wote.

Lishe Bora Ya Mjamzito: Trimesta ya kwanza

Iwapo ana shida ya kichefu chefu, wakati wa asubuhi anaeza kula kiamsha kinywa kidogo, kama vile tunda ama kupakua chakula kidogo. Wakati wa jioni, ale chakula kingi kinacho kuwa na mahitaji yote. Iwapo anakiungulio, anashauriwa kukipakua kiamsha kinywa kingi na kiwango kidogo wakati wa usiku. 

Ni muhimu sana kwa mama mja mzito kuepuka kunywa kahawa nyingi. Pombe na uvutaji wa sigara huathiri ukuwaji wa mtoto aliye tumboni. 

Folic Acid

Ni muhimu sana katika safari ya uja uzito. Mama anapaswa kupata viwango vinavyo hitajika. Wataalum wa lishe wana washauri wamama waja wazito kuhakikisha kuwa wana kula vyakula bora na matunda kwani huko ndo watapata folic acid ya kutosha. Mwana mke anapo enda kumtembelea daktari wake, anashauriwa kuhusu tembe anazo paswa kuchukua ili kupata madili haya. 

Uzito wa mama

Ni jambo la kawaida kwa kila mama mja mzito kuongeza uzito na mwili pia anapo kuwa na mimba. Hii ni ishara kuwa mtoto aliye tumboni mwake pia anakua. Uzito wa mama usipo ongezeka, kuna uwezekano mkubwa kuwa mtoto wake hakui pia. Lishe bora inamsaidia mama na mtoto wake kukua na kupata kilo nyingi. Pia ni muhimu kujua kuwa mama mja mzito hafai kujialia mpaka anapo ongeza kilo kupindukia. Anaweza jihusisha na mazoezi kidogo kama vile kutembea. Mtoto anapo kuwa mkubwa sana tumboni mwa mamake, inakuwa tatizo kubwa mwanamke anapo jifungua. Wakati mwingine inabidi amefanyiwa upasuaji. Ni muhimu kwa kila mama kuhakikisha kuwa haongezi uzito kupindukia kiwango kinachofaa. Katika trimesta ya kwanza, anapaswa kuongeza kilo chache kuhakikisha kuwa hata ongeza kilo zaidi katika trimesta zifuatazo.

Lishe baada ya kujifungua

Lishe bora ya mjamzito inasaidia katika ukuaji wa mtoto. Lishe bora inapaswa kuzingatiwa hata mama anapo jifungua. Hii ni kwa sababu mtoto wake mchanga anategemea chakula mama anacho kila. Ili mtoto kupata afya bora na kuepuka magonjwa, ni muhimu mama kula vyakula bora. Madili yanayo hitajika kwa mwili na vitamini pia kwani ni muhimu sana katika ukuwaji wa mtoto. Pia lishe baada ya kujifungua inasaidia mama kupata shepu yake aliyo kuwa nayo kabla ya kupata mimba. Wa mama wengi hujiachilia wanapo pata mimba na baada ya kujifungua. Kwa hivyo uzito wao unaongezeka na kupata mili mikubwa. Kupata mimba si sababu kamili ya kuuwachilia mwili wako kuwa mkubwa kupindukia. 

Mama anapomlisha mtoto kutoka kwa matiti yake, inamsaidia kupunguza uzito alio upata alipo kuwa na mimba. 

Read Also: Food timetable for students on a tight budget

 

 

img
Yaliandikwa na

Risper Nyakio

  • Nyumbani
  • /
  • Feeding & Nutrition
  • /
  • Ratiba ya lishe bora ya kuzingatia nchini Kenya ya mama mja mzito
Gawa:
  • Kutengeneza ratiba mwafaka ya lishe nyumbani nchini Kenya

    Kutengeneza ratiba mwafaka ya lishe nyumbani nchini Kenya

  • Je, Ungependa Usaidizi Wa Kupanga Ratiba Ya Lishe Ya Wiki Moja?

    Je, Ungependa Usaidizi Wa Kupanga Ratiba Ya Lishe Ya Wiki Moja?

  • Vyakula Vitakavyo Kusaidia Kupata Mtoto Mwenye Afya Bora na Urembo

    Vyakula Vitakavyo Kusaidia Kupata Mtoto Mwenye Afya Bora na Urembo

  • Jinsi Ya Kutengeneza Ratiba Ya Lishe Nchini Kenya

    Jinsi Ya Kutengeneza Ratiba Ya Lishe Nchini Kenya

  • Kutengeneza ratiba mwafaka ya lishe nyumbani nchini Kenya

    Kutengeneza ratiba mwafaka ya lishe nyumbani nchini Kenya

  • Je, Ungependa Usaidizi Wa Kupanga Ratiba Ya Lishe Ya Wiki Moja?

    Je, Ungependa Usaidizi Wa Kupanga Ratiba Ya Lishe Ya Wiki Moja?

  • Vyakula Vitakavyo Kusaidia Kupata Mtoto Mwenye Afya Bora na Urembo

    Vyakula Vitakavyo Kusaidia Kupata Mtoto Mwenye Afya Bora na Urembo

  • Jinsi Ya Kutengeneza Ratiba Ya Lishe Nchini Kenya

    Jinsi Ya Kutengeneza Ratiba Ya Lishe Nchini Kenya

Pata ushauri wa mara kwa mara kuhusu ujauzito wako na mtoto wako anayekua!
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • Zaidi
    • TAP Jamii
    • Tangaza Nasi
    • Wasiliana Nasi
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2022 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
Kutuhusu|Timu|Sera ya Faragha|Masharti ya kutumia |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it