Covid-19: Jinsi Ya Kuishi Iwapo Kuna Lockdown Ya Homa Ya Korona Kenya

Covid-19: Jinsi Ya Kuishi Iwapo Kuna Lockdown Ya Homa Ya Korona Kenya

Jambo la kuwa na lockdown nchini Kenya linapata hisia tofauti kutoka kwa wananchi. Huku wengine wakitarajia kuwe na lockdown ili kuthibiti kuenea kwa virusi vya korona, wengine ikiwemo wana biashara wanao tegemea mapato yao ya kila siku kujimudu wanalia. Huku serikali ikifanya juu chini kusisitiza watu wabaki nyumbani bila ya kuweka lockdown, baadhi ya wananchi hawafuati kanuni hizi. Lockdown ni mojawapo ya chaguo ambazo nchi iko nayo ila je, wananchi wako tayari? Ni vyema kwa kila mmoja kuwa tayari iwapo kuwe na lockdown ya homa ya korona nchini Kenya ama baadhi ya sehemu za nchi.

how to survive a lockdown in Nigeria

Chanzo cha picha: Shutterstock

Jinsi ya Kuishi Iwapo Kuwe na Lockdown ya Homa ya Korona Nchini Kenya

1. Usitie shaka!

Iwapo kuna na woga ni asili kunapo kuwa na janga kubwa, ni vyema kwa kila mwananchi kuwa na ujasiri na kutokuwa na uwoga. Masaa machache baada ya rais Uhuru Kenyatta kutangaza kuwa shule zitafungwa na watoto kurudi nyumbani siku ya 13th Marchi 2020, watu wengi walishuhudiwa wakirudi kwenye za mashinani na kutoka mijini. Huku wengine wakinunua vitu vya nyumba vingi kadri wangeweza kubeba. Huku tishu zikisemekana kuisha madukani.

Na je, hatua mojawapo ya kujikinga kutokana na virusi hivi vya homa ya korona ni ipi? Epuka mahali kuliko na watu wengi na uzingatie umbali wa muingiliano!

how to survive a lock down in Nigeria

Chanzo cha picha: pixabay

2. Tengeneza orodha:

Chukua muda wako utengeneza orodha ya vitu utakavyo hitaji nyumbani mwako iwapo kutakuwa na lockdown ya homa ya korona nchini Kenya. Gawanya orodha hii kwa vitu muhimu na vile ambavyo sio muhimu sana.

Vitu vya muhimu vitakuwa kama vile: chakula, madawa, tishu, maji, mafuta (ya gari lako na jenereta)

Vitu visivyo vya muhimu: vifaa vya kuandika, karatasi, michezo ya mbao, betri, taa, fani na kadhalika.

coronavirus lockdown in Nigeria

Chanzo cha picha: pixabay

3. Tengeneza ratiba yako ya lockdown:

Kwa sababu hauna uhakika wakati ambapo mambo yatarudi kuwa kawaida kama hapo awali. Ni vyema uwe na ratiba ya mambo yafuatayo:

Mwangaza: Unapaswa kuratibisha wakati ambao unatarajia jenerata yako kufanya kazi. Huku ukiendelea kutarajia kuwa Kenya Power haitashuhudia kupotea kwa sitima kabla ya mambo kurudi kawaida. Iwapo unatumia sitima nyingi nyumbani, hakikisha kuwa mnapunguza utumiaji wenu. Kama vile kutumia mwanga asili wa jua mchana na sitima wakati wa usiku.

Chakula: Litakuwa jambo la busara kutengeneza ratiba ya chakula. Pia ni vyema kuangazia viwango vya chakula na kuwafunza watoto wako kuepuka kutupa chakula. Wakati huu ni muhimu kuwa na mafundisho mengi kama vile kuwafunza kuwa ni vibaya kutupa chakula kwani wengine wanakosa chakula hiki na kulala njaa.

Kazi na Shule: Shule zitakuwa zimefungwa kwa muda sana, hata kama si wakati wa likizo. Tengeneza ratiba ya mambo ya kufanya na uhakikishe kuwa wanasoma. Ni vyema pia ukijihusisha katika vipindi vyao vya kusoma. Hakikisha pia una thibiti wakati wao wa kutazama runinga na wana pata wakati mwingi wa kucheza ila ndani ya nyumba. Tafuta michezo ambayo mnaweza cheza nyote kama familia.

Kufanya kazi kutoka nyumbani huenda kukawa na matatizo yake. Hasa wakati huu ambapo watoto wako nyumbani. Lazima uwatunze na bado ufanye kazi, kwa hivyo una majukumu mengi mno. Unaweza tenga wakati wako wa kufanya kazi. Iwapo wewe hufanya kazi masaa manne kila siku. Unaweza amka masaa manne kabla ya watoto wako kuamka ili ufanye kazi. Wakati ambao wanaamka, utakuwa tayari ushamaliza kufanya kazi yako. Pia iwapo unamsaidizi wa kazi za kinyumbani, anaweza kuchungia watoto wako wakati ambapo unafanya kazi kuhakikisha kuwa hausumbuliwi na watoto unapofanya kazi.

Mapumziko na Mazoezi:

Kwa sababu wakati mwingi utakuwa nyumbani na huenda mwendo kwa mahala pa zoezi pamefungwa, ni vyema kuendeleza maisha yako ya zoezi. Tenga wakati angalau dakika 30 kila siku kufanya mazoezi kila siku. Ili kufanya jambo hili liwe la kupendeza zaidi, unaweza wahusisha watoto wako. Huku kutahakikisha kuwa uzito wao sio mwingi sana. Tenga wakati wa kupumzika. Ni muhimu sana kwa kila mzazi, majukumu mengi ya kifamilia na kikazi huenda yakafanya nishati yako kuungua. Mazoezi pia ni njia mojawapo ya kuhakikisha una pumzika.

4. Hakikisha kuwa unafuatilia habari za hivi punde zinazo aminika
Katika wakati huu ambapo kuna lockdown, ni vyema kuhakikisha kuwa unafuata habari hasa kwa mamlaka ya nchi yanayo aminika. Epuka kuamini habari za mitandao ya kijamii ambazo hazija dhihirishwa na wizara ya nchi. Vyanzo vya kuaminika nchini kenya ni kama vile Wizara ya Afya, WHO, na Serikali ya nchi ya Kenya.
lockdown ya homa ya korona kenya

Picha: Pixabay

5. Zingatia hatua za usalama dhidi ya homa ya korona (na uwafunze watoto wako hatua hizi)
Iwapo una jambo la dharura linalo kulazimisha kutoka nje ya nyumba, hakikisha wakati wote kuwa:
1. Una nawa mikono kwa kutumia sabuni na maji kabla ya kutoka nje ya nyumba, punde tu baada ya kufanya kazi ya kinyumbani na punde tu baada ya kurudi nyumbani.
2. Hakikisha kuwa wakati wote unaangazia umbali wa mita 1 (fiti 3) kati yako na mtu mwingine, iwapo unajipata miongoni mwa watu.
3. Epuka ummati wa watu
4. Usiguse uso wako (mapua, macho na mdomo)
5. Zingatia usafi wa mfumo wa kupumua kwa kufunika mdomo na mapua yako kwa kutumia upande wa ndani wa kiwiko chako ama tishu unapokohoa ama kuchemua. Iwapo utatumia tishu, itupe baada ya kukohoa.
Wafunze watoto wako hatua tulizo orodhesha hadi itakapo kuwa njia ya maisha.

Iwapo wewe ama mwana familia mwingine anahisi ama anadhihirisha ishara za COVID-19 kama vile joto jingi, kikohozi kilicho kauka ama kupungukiwa kwa pumzi, mpeleke kwenye kituo cha hospitali kilicho karibu nawe. Serikali ya Kenya imetenga hospitali maalum ambazo zitakuwa vituo vya wagonjwa wa korona. Nambari za dharura za kupiga ni hizi: 0800721316 Piga kisha uwajulishe unavyo hisi.

Huku Africaparent, tuko hapa kukuunga mkono kadri tuwezavyo. Pamoja tunaweza kabiliana na janga la COVID-19. Hakikisha uko salama!

Soma pia: See These Safety Tips For Preventing Coronvirus Infection

Written by

Risper Nyakio