Heko Vincent Kipchumba: Mbio Za London Marathon 2020 Za Wanaume

Heko Vincent Kipchumba: Mbio Za London Marathon 2020 Za Wanaume

Mbio za London Marathon 2020 zimekuwa vinywani vya watu wengi kwa muda mrefu sana. Huku wanariadha wakiji kakamua na kufanya mazoezi kabambe kutayarishia mbio hizi, wananchi wa Kenya na duniani kote wamekuwa wakingoja mbio hizi kwa muda sasa. Aliye kwa mwanga wa mbio hizi ni Eliud Kipchoge, mwananchi wa Kenya aliye fanya bendera ya Kenya ipepee duniani kote upande wa riadha na kufanya nchi yetu itambulike na kusifiwa kwa mbio za masafa marefu.

Heko Vincent Kipchumba: Mbio Za London Marathon 2020 Za Wanaume

Eliud Kipchoge ni mzaliwa wa mwaka wa 1984 tarehe 5 Novemba. Ni mwanariadha wa mbio za masafa marefu na hapo awali alikuwa katika mbio za mita 5000. Katika maisha yake ya mbio na kuwa mwana riadha, ameshinda mbio 12 kati ya 13 alizo jumuika nazo. Ushindi wake wa kwanza ukiwa katika mwaka wa 2003 katika IAAF World Cross Country Championships akiwa na miaka 18. Katika mwaka wa 2012, alibadilisha na kuingia katika mbio za masafa marefu na kushikilia rekodi ya mkimbiaji wa kasi zaidi wa pili duniani kote na rekodi ya 59:25.

Anashikilia rekodi ya dunia katika mbio za masafa marefu za wakati wa 2:01:39. Rekodi aliyo weka Septemba 16 mwaka wa 2018 huko Berlin na alipo vunja rekodi ya hapo awali kwa dakika 1 na sekunde 18. Ushindi wa mbio hizi ulimpa jina la mkimbiaji mkuu zaidi duniani.

Ila kadri na watu wengi walivyo tarajia kuwa kiongozi na simba wa Kenya wa mashindano ya mbio za masafa marefu angeleta tuzo ya mkimbiaji bora zaidi katika mbio za mwaka huu za London Marathon. Bwana Eliud Kipchoge hakuongoza mbio hizo. Mshindi wa Kenya kwa mbio hizi za wanaume ni Vincent Kipchumba na kuleta tuzo ya fedha nchini. Alimaliza wa pili baada ya Kitata kutoka Ethiopia.

Heko Vincent Kipchumba: Mbio Za London Marathon 2020 Za Wanaume

Bado tuna sherehekea ushindi wa Vincent Kipchumba aliendeleza kufanya bendera ya nchi yetu kupepea. Na kwa Eliud Kipchoge, kila mshindi huwa na siku yake ya kupumzika na pia kuwapisha wengine waongoze. Kama nchi na wananchi wa Kenya, tunazidi kumpongeza kwa juhudi alizo tia ili kuwa mmoja wa walio jiunga na mbio hizo za london marathon 2020.

Soma Pia:Nyumba 5 Za Watu Mashuhuri Kenya Ambazo Lazima Utazame

Written by

Risper Nyakio