Wataalum Wana Haya Ya Kusema Kuhusu Lugha Ya Kitoto Na Athari Zake!

Wataalum Wana Haya Ya Kusema Kuhusu Lugha Ya Kitoto Na Athari Zake!

Watoto wanapo fika umri fulani, wazazi wanakoma kufurahishwa na lugha ya kitoto. Wana amini kuwa mtoto anapo fika umri unao faa, ni wakati wake kuanza kuzungumza kama watu wazima wanavyo, kwa maneno yaliyo kamilika na sentensi. Soma zaidi kuhusu lugha ya kitoto na athari zake.

Lugha Ya Kitoto Na Athari Zake

maendeleo ya mtoto wa miezi mitatu

Masomo mapya yanasema, walakini, lugha ya kitoto ina manufaa kwa mtoto na jinsi wanavyo kuza maneno yao na kufahamu lugha.

Kulingana na utafiti ulio chapishwa kwenye makala ya Kusoma Lugha Na Maendeleo, watafiti walidhibitisha kuwa watoto huwa na wakati rahisi kusoma maneno mapya panapo kuwa na silabi zilizo rudiwa.

Maneno kama vile mama, baba, dada ni rahisi kwa mtoto kutamka na kukumbuka.

Kulingana na Science Daily, Maneno haya yalikuwa na silabi sawa na rahisi kutamka.

Utafiti ulio fanyika ulidhibitisha kuwa watoto walipo rekodiwa wakiangalia vifaa , macho yao ilidhihirisha mwendo wa pole pole wakiangalia vifaa vilivyo kuwa na silabi zilizo rudiwa ikilinganishwa na vifaa vingine. Wataalum walisema kuwa hapo ni mahali pazuri pa kuanza kumfunzia mtoto maneno na lugha.

"Huu ndiyo ushuhuda wa kwanza kuonyesha kuwa watoto wana egemea upande wa kurudia wanapo soma maneno mapya," alisema Mitsuhiko Ota, ambaye ni kiongozi wa utafiti wa somo hilo.

Watafiti pia walisema kuwa sababu kwa nini watu wazima huongea kwa njia hiyo kwa watoto ni kwa sababu watoto huitikia vyema zaidi kwa maneno yaliyo rudiwa, na kwa sababu hiyo, matumizi ya maneno kama vile "dada" na "mama".

Wataalum Wana Haya Ya Kusema Kuhusu Lugha Ya Kitoto Na Athari Zake!

"Masomo mengine yanayo husiana na muziki, kuona na tabia yameonyesha kuwa watoto huonekana kusoma vyema zaidi na kurudiwa na vitu sawa," alisema mzazi mmoja." Utafiti huu unaashiria kuwa hayo ni sawa kwa maneno ya kusoma."

Je, huku kuna maana kuwa una paswa kumkubalisha mtoto wako kutumia lugha ya kitoto hadi anapo fikisha miaka mitano? La hasha, lakini hakuna ubaya kuwafunza lugha inayo faa punde tu wanapo weza kuzungumza vyema.

Je, una ujumbe zaidi ambao ungependa kutujulisha kuhusu mada hii? Tujuze kwa kuwacha ujumbe mfupi hapa chini!

Soma Pia: Kulinganisha Mbinu Za Ulezi Za Wazazi Wa Afrika Na Wa Umarekani

Written by

Risper Nyakio