Maambukizi 10 Yanayo Sababisha Mama Mjamzito Kupoteza Mimba

Maambukizi 10 Yanayo Sababisha Mama Mjamzito Kupoteza Mimba

Baadhi ya maambukizi yanayo sababisha kupoteza mimba wakati wa ujauzito.

Mimba ni wakati wa dharura kwa mwanamke. Lazima awe makini zaidi kwa afya yake na sio kwa sababu yake tu ila kwa sababu ya mtoto pia. Kuwa makini kwa afya yake kuna husisha kula vyema, kuchukua vitamini za kabla ya kujifungua, na kuepuka maambukizo. Kwa sababu kuna maambukizi yanayo sababisha kupoteza mimba, na kukatiza safari yako ya ujauzito.

Nyingi kati ya maambukizo ambayo yanaweza tendeka ukiwa na mimba huenda yakasababisha matatizo makubwa. Maambukizo ya ngozi, mfumo wa mkojo, wa kupumua huwa machache. Ila, baadhi ya maambukizi yanaweza pitishwa kutoka kwa kiinitete kabla ama wakati wa kujifungua na kuharibu kiinitete na kusababisha kuharibika kwa mimba ama kujifungua kabla ya wakati kufika. Angalia baadhi ya maambukizi yanayo sababisha kupotea kwa mimba wakati wa ujauzito.

Maambukizi Yanayo Sababisha Kupoteza Mimba

infections that can cause miscarriage

Klamidia (Chlamydia)

Maambukizi ya klamidia ni maradhi yanayo sambazwa kwa kawaida kupitia ngono. Kwa sababu maradhi haya kwa mara nyingi hayana dalili zinazo onekana punde, heunda yaka athiri watu wengi kuliko vile wataalum wanaweza hesabu. Kwa wanawake, hesabu ya maradhi haya kwa maradhi yote ya kizazi huenda yakatoa pus ambayo haisababishwi na kisonono. Maradhi haya huenda yakasababisha kupotea kwa mimba, uchungu wa uzazi usio komaa na kutoboka kwa mapema kwa membranes. Huenda yakasababisha kufura kwa macho (conjuctivitis) kwa watoto wadogo.

Kisonono (Gonorrhoea)

Kisonono ni maradhi yanayo ambukizwa kwa ngono kutoka kwa bakteria ya Neisseria gonorrhoeae. Bakteria hizi zina athiri ukuta wa urethra, kizazi, rectum na koo; ama membranes zinazo funika sehemu ya mbele ya macho (conjuctiva na cornea). Watu kwa mara nyingi huwa na uchafu kutoka kwa uke ama kibofu na huenda wakahitaji kuenda haja ndogo mara kwa mara. Iwapo mama mwenye mimba anapata maradhi haya katika hatua za mapema za ujauzito, huenda yaka sababisha kupoteza mimba. Katika hatua za baadaye za ujauzito, bakteria huenda ika sambaa hadi kwa macho ya kiinitete wakati wa kujifungua; na kusababisha conjuctivitis kwa mtoto mdogo.

Virusi vya Maambukizo ya Zika

Maambukizi haya kwenye mama mjamzito huenda yakasababisha mtoto kuwa na kichwa kidogo. Kichwa ni kidogo kwa sababu hakikui kwa njia ya kawaida. Virusi vya zika huenda pia vikasababisha kutokuwa kawaida kwa mtoto. Virusi vya zika husambazwa na mbu, ila huenda pia yakasambazwa kingono, kupitia kwa damu ama kutoka kwa mama mjamzito hadi kwa mtoto wake kabla na wakati wa kuzaliwa. Katika hatua za mapema za ujauzito, kutibu maambukizi huenda kukasababisha kupoteza mimba.

German Measles

Pia yanajulikana kama rubella, maambukizi haya huenda yakasababisha matatizo, hasa kutokua kwa kutosha kabla ya kuzaliwa; cataracts, matatizo ya moyo; matatizo ya kusikia, na ukuaji ulio chelewa. Rubella ni maambukizi ya virusi vilivyo rahisi kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine na huwa na ishara nyepesi, kama vile maumivu ya uchungu wa viungo na upele; ila huenda ukasababisha kupoteza mimba na matatizo mengi ya kujifungua iwapo mama anapata maambukizi ya rubella wakati wa ujauzito. Rubella hapo awali ilijulikana kama 'German Measles' ama '3-day measles' kwa sababu inasababisha upele ulio sawa na unao sababisha measles. Ila virusi tofauti ndizo zinazo husika.

Maambukizi Yanayo Sababisha Kupoteza Mimba

maambukizi yanayo sababisha kupoteza mimba

Maambukizi ya Cytomegalovirus 

Kuna maambukizi ya kawaida ya herpes iliyo na ishara nyingi sana: kutoka kwa kutoona ishara kwa joto jingi na kuchoka (maambukizi ya mononucleosis inayo fanana); hadi kwa ishara zilizo ongezeka zinazo husisha macho, ubongo na viungo vingine vya ndani. Kwa mwanamke mjamzito, maradhi haya huenda yaka pita kwenye placenta na kuharibu maini na ubongo wa kiinitete; na kiinitete huenda kikawa hakijakuwa kinavyo tarajiwa. Huku huenda kukasababisha matatizo ya chromosomes na kuharibika kwa mimba.

Chickenpox (Varicella)

Unapokuwa na maradhi ya chickenpox wakati wa mimba, hatari yako ya kupoteza mimba huongezeka. Maambukizi haya huenda yakaharibu macho ya mtoto na kusababisha matatizo ya miguu; kuto ona ama matatizo ya akili. Na kichwa cha kiinitete huenda kikawa kidogo kuliko kawaida.

Toxoplasmosis

Na maambukizi haya, vimelea vyenye seli ya protozoan maarufu kama Toxoplasma gondii  ndiyo yanahusika. Wakati mwingi, maambukizi haya haya sababisha dalili zozote, ila baadhi ya watu huwa na lymph nodes zilizo fura, joto jingi; kujihisi mgonjwa, na wakati mwingine koo iliyo kali ama kutoona vizuri na kuumwa na macho. Kwa watu walio na mfumo wa kinga usio na nguvu kufuatia virusi vya ukimwi ama hali nyingine, toxoplasmosis huenda ikatokea tena na kuadhiri ubongo. Ni maambukizi ya protozoa na huenda yaka sababisha kupoteza mimba, kifo cha kiinitete ama matatizo ya kujifungua.

Listeriosis

Ni maambukizi ya bakteria yanayo ongeza hatari zako za uchungu wa uzazi usiokomaa, kupoteza mimba na stillbirth. Watoto wachanga wanaweza ambukizwa ila, ishara huenda zika chelewa hadi wiki nyingi baada ya kuzaliwa. Listeriosiscomes kutoka kwa ishara chanya ya bakteria  Listeria monocytogenes hupata mtu akikula chakula kilicho haribika.

Maambukizi ya Bakteria ya Uke (Bacterial Vaginal Infections)

Maambukizi ya uke kama vile bacterial vaginosis huenda yakasababisha uchungu wa uzazi usiokomaa, kupoteza mimba ama kutoboka kwa membranes zilizo na kiinitete.

Maambukizi ya Mfumo wa Mkojo (Urinary Tract Infection)

Maradhi haya huongeza hatari ya uchungu wa uzazi usiokomaa na kutoboka kwa membranes ambayo yameshikilia kiinitete.

Jinsi ya Kutibu Maradhi Ambayo Husababisha Kupoteza Mimba

medication

Wakati mwingine, dawa kulingana na kutoshanishwa kwa umuhimu na hatari.

Ili kuamua iwapo utatibu na dawa za kawaida dhidi ya maradhi, daktari wako atapima kiwango cha hatari cha kutumia dawa dhidi ya hatari za kutumia maambukizi.

Web MD, MSDManuals

Soma pia: Is It Safe To Take Antibiotics During Pregnancy?

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Ayeesha kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio