Dada: Kuna Maana Ya Kiroho Ya Rasta?

Dada: Kuna Maana Ya Kiroho Ya Rasta?

Huenda rasta zikawa ni mtindo wa nywele kwa baadhi ya watu ila kwa wengine zina maana. Watoto wanao zaliwa na rasta wanatambulika kama dada.

Huko Nigeria hasa sehemu ya Kusini na Mashariki, kuona mtu akitembea mtaani akiwa na rasta sio jambo la kushangaza. Wakati ambapo zinavaliwa kama mtindo, kuna watu ambao wanazaliwa nazo wakiwa wadogo. Na ni kwa watu hawa sababu za kiroho zinatumika sana. Watoto wanao zaliwa na rasta wanaitwa Dada. Na kwa sababu ya umuhimu wa kiroho, wakati mwingine wanaishi kwa umri fulani kabla ya kunyoa nywele. Umri unao faa huenda ukawa kati ya miaka mitatu hadi kumi na tano. Baadhi ya wakati, ni mtoto anaye uliza wazazi wamnyoe ama nywele yake ibaki. Ila, maana ya kiroho ya rasta ni nini?

Maana ya kiroho ya rasta

Dada: Kuna Maana Ya Kiroho Ya Rasta?

Huko Nigeria, wakati ambapo kitu chochote kina husishwa na roho, watu wengi wana kitazama kwa njia fulani. Kwa hivyo haijakuwa rahisi kwa watoto na watu wazima walio zaliwa kwa njia hii. Wanatazamiwa kuwa tofauti, na kwa njia isiyo furahisha. Ila, kilicho saidia ni wanao valia rasta kwa kuamua wanaifanya iwe vigumu kutambua walio zaliwa nazo. Na imesaidia kupunguza uwoga wa watu walio zaliwa na dada wana tazamiwa. Makala haya yana angazia maana ya kiroho ya rasta, ya kidini na kitamaduni.

  • Maana ya kidini ya rasta

maana ya kiroho ya rasta

Kuna hadithi kwenye bibilia kuhusu Samson na Delilah. Wakristu wengi wana ifahamu hadithi hii. Katika hadithi hii, nguvu za Samson huwa zimehusishwa na rasta kichwani chake. "Samson alipoteza nguvu zake baada ya nywele zake kukatwa". Pia kuna sehemu ingine kwenye kitabu cha Leviticus 21:5 inayo wauliza wachungaji kuto nyoa nywele zao. Inasoma, "Hawata nyoa nywele zilizoko kichwani chao, na pia hawatanyoa ndevu zao, ama hata kukata sehemu yoyote mwilini mwao. Hii ndiyo sababu ya kibibilia kwa nini wana rasta huwa na rasta kichwani.

Walakini, rasta ni maarufu kwa watu walio kwenye Cherubim na Seraphim huko Nigeria. Mchungaji S.A Adreniran, anaye ongoza mojawapo ya kanisa kubwa zaidi huo Jos, anasema kuna wazazi wachache kati ya wafuasi wake walio na watoto dada. Walakini, haamini ni maarufu kwa wafuasi wake tu.

Kwa Bi na Bw. Musa, kuzaliwa kwa watoto wao kuliwafungua macho kwa uwezo mkuu wa watoto wenye rasta. Kulingana na wao, kuzaliwa kwa Samson na Francis kuliwasaidia kusoma vitu fulani kuhusu Dada. Wana amini kuwa watoto hawa wawili wana nguvu zaidi kuliko watoto wengine wa umri wao. Ili ripotiwa kuwa wawili hawa walianza kutembea bila ya kutambaa. Kwa wazazi wao, watoto hawa wenye rasta wana maanisha nguvu. Walitamatisha hivi baada ya mtu asiye julikana kukata kitita kimoja cha nywele za Samson na kufanya akose nguvu. Kama matokeo, alichapwa na wavulana ambao alikuwa na nguvu kuwashinda hapo awali.

  • Imani za kitamaduni za rasta

maana ya kiroho ya rasta

Watu wa Yoruba wana waita watoto walio na rasta "Dada", na wana Igbo huwaita "Ezenwa" ama "Elena". Kwa wana Yoruba na Igbo, watoto walio na dada ni watu wa kiroho kwa sababu ya nywele zao. Pia wana julikana kama watoto wanao leta mali ama utajiri. Wana sherehekewa na nywele yao inaguswa na mama zao tu. Na ishara zake ni cowries katika tamaduni zote mbili. Kwa hivyo, kwa profesa Augustine Agwuele, kuwa dada ni kuwa wa-maana. Wakati wao huku unatambulika kama wa maana na wala sio mabaya.

Hata kama anasema kuwa nywele lazima ikatwe ili watoto watangamane na wanajamii bila kukaa tofauti. Ila, haukati nywele yake tu, kuna hatua lazima zifuatwe. Lazima nywele zikatwe kando ya mto. Kisha ukate nywele na uweke kwenye kontena iliyo na maji ya mto ndani. Hii ni kwa sababu iwapo mtoto atagonjeka hapo baadaye, maji yale ya mto na dawa zinaweza ponya ugonjwa wa mtoto. Hatimaye, kwa tamaduni za Yoruba na Igbo, sherehe ya kukata nywele inafanywa kabla ya umri wa miaka 14.

Soma pia: 20 Signs that you have a gifted child

Chanzo: Researchgate, News Tower

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Lydia Ume kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio