Kuna Maana Gani Utosi Wa Mtoto Wako Unapo Piga?

Kuna Maana Gani Utosi Wa Mtoto Wako Unapo Piga?

Unaifahamu sehemu nyeti zaidi ya mtoto wako na kwa nini unapaswa kuilinda?

Utosi wa mtoto ni sehemu laini na wamama wengi wa mara ya kwanza wanaelewa haja ya kulinda sehemu hii ya kichwa cha mtoto wao, utosi wa mtoto kupiga huenda kukaibua hofu. Makala haya yana kuelezea mambo ya kuwa makini kuangalia!

Kabla kuangazia sababu kwa nini utosi wa mwanao unaweza kuwa ukipiga, ni vyema kwanza kuelewa sehemu hii ya mwili wa mtoto wako.

Utosi wa mtoto ni nini hasa?

Utosi wa mtoto ni sehemu laini inaonyesha mahali ambapo skull yake haijakomaa kabisa baada ya kuzaliwa. Sehemu hii kwa kisayansi inajulikana kama fontanels. Ni vyema kufahamu kuwa mwanao ana hizi sehemu laini juu ya kichwa chake na nyingine nyuma ya kichwa chake na kufanya sehemu mbili laini kwenye kichwa chake kidogo.

Kwa nini mtoto ana sehemu laini?

 1. Ubongo wa mtoto wako bado utakua baada ya kuzaliwa, kwa hivyo sehemu hizi zina kubalisha ubongo wake kukua kwa kasi baada ya kuzaliwa kwake.
 2. Kichwa cha mtoto kina uwezo wa kupita kwa kanali ya kuzaliwa kwa sababu sehemu hizi laini zina fanya kichwa kiweze kujikunja na kubadili muundo huku kikipita kwenye mfumo wa kuzaliwa.

Kuna Maana Gani Utosi Wa Mtoto Wako Unapo Piga?

Jinsi ya kutambua wakati ambapo kuna kasoro na utosi wa mtoto wako

 1. Utosi ulio bondeka

Iwapo sehemu hii laini imerudi upande wa ndani, huenda ikawa ni ishara kuwa mtoto hana maji tosha mwilini, kwa hivyo unapaswa kumpeleka mtoto hospitalini bila kukawia ili apate matibabu.

 1. Sehemu laini iliyo fura

Iwapo unapata kuwa fontanel ya mtoto imefura, huenda hii ikawa ni ishara kuwa kuna shinikizo kwenye ubongo wa mtoto. Huenda hii ikawa hali ya kuhatarisha maisha yake, kwa hivyo bila shaka, unapaswa kumpeleka mtoto kuona daktari.

 1. Kichwa kuinama

Baadhi ya watoto huenda wakawa na vichwa vilivyo songa upande mmoja badala ya kuwa katikati, huenda hii ikawa ni kufuatia tatizo linalo msumbua. Ili kutoa shaka za hali inayo julikana kama torticollis, unapaswa kumpeleka mtoto kwa mtaalum wa afya ya watoto. Kwa visa vingi, hali hii inaweza tibiwa kwa tiba ya fizikia ili kunyoosha misuli na kusaidia mtoto kubadili kichwa chake kiwe sambamba bila kukosa starehe.

 1. Hali inayo fahamika kama craniosynostosis

Kwa visa vilivyo nadra zaidi, mtoto anaweza pata hali inayo julikana kama craniosynostosis, ambapo vipande viwili kichwani mwake vina shikana. Hii inaweza badili shepu ya kichwa cha mtoto kwa sababu ubongo unakua na kuharibu kichwa cha mtoto kwa sababu ya kukosa nafasi. Wataalum wa matibabu wata shauri upasuaji kutenganisha sehemu hizi zilizo shikana.

Vitu muhimu vya kujua kuhusu utosi wa mtoto kupiga

Kuangalia utosi wa mtoto wako ukipiga wakati wa mpigo wao wa roho huenda likawa ni jambo la kukutia hofu, ila wakati wote si ishara ya jambo mbaya. Utosi wa mtoto kupiga huenda ukakusaidia kujua kinacho endelea na afya ya mtoto wako.

 • Kupiga kwa sehemu laini ya mtoto wako kutakoma kadri anavyo zidi kukua na sehemu ili kufungana.
 • Membrane nono hutengeneza sehemu ya kumlinda mtoto na kulinda ubongo wake unao endelea kukua, ila kila mtu hata watoto wachanga- hawapaswi kumshika shika mtoto ovyo hasa katika sehemu hiyo laini.
 • Sehemu laini ya kichwa cha mtoto wako itaanza kufungana akifika miezi sita na kufungana kabisa katika miezi 18.
 • Mtoto wako ana sehemu mbili laini - moja katikati ya kichwa chake na nyingine nyuma ya kichwa chake, kwa hivyo unapaswa kuwa makini sana unapo mgusa kichwa.
 • Sehemu iliyo ingia ndani huenda ikawa ni ishara kuwa hana maji tosha mwilini, na sehemu iliyo fura kuashiria kuwa ana maumivu ya kichwa.
 • Watoto wanao lia huenda wakawa na sehemu laini ya kichwa iliyo fura. Kwa hivyo mtoto wako anapo lia na kutapika, sehemu yao laini inayo piga haipaswi kukusumbua sana.
 • Kuna imani zisizo za kweli kuwa baadhi ya mafuta ya kienyeji yatasimamisha sehemu laini kupiga. Wakati ambapo hakuna aliye fanya utafiti kudhibitisha jambo hili, unapaswa kuwa mtulivu na kungoja hadi wakati ambapo sehemu hii itajifunga yenyewe.

Kichwa ni sehemu nyeti sana ya mwili wa mtoto wako, na kwa hivyo, unapaswa kuwa makini sana unapo mshika kichwa. Wakati ambapo sehemu laini itajifunga peke yake bila tatizo lolote, ni muhimu kuhakikisha kuwa hakuna kitu kinacho msumbua. Ukigundua kitu kisicho cha kawaida kuhusu fontanel ya mtoto, tafadhali mpeleke kwa daktari aangaliwe!

Kumbukumbu: WebMD

Soma pia: Maana Na Sababu Za Mtoto Kujigonga Kichwa Kutumia Mikono

Written by

Risper Nyakio