Maandalizi 5 Ya Kujifungua Yaliyo Muhimu Zaidi Kwa Mama!

Maandalizi 5 Ya Kujifungua Yaliyo Muhimu Zaidi Kwa Mama!

Japokuwa huduma za mama kujifungua katika hospitali nyingi za umma ni bure, ni vyema wanandoa kujiandaa kifedha.

Afya bora kwa mama mwenye mimba ni muhimu kwake na kwa kiumbe kinacho kua tumboni mwake. Afya ya mtoto baada ya kuzaliwa huathiriwa na hali ya afya ya mama anapokuwa mjamzito. Kwa hivyo, mama anapaswa kujiandaa kivipi kabla ya kujifungua? Tuna angazia maandalizi ya kujifungua yaliyo muhimu kwa mama.

Maandalizi ya kujifungua kwa mama

maandalizi ya kujifungua

  • Kuhudhuria kliniki

Mama mwenye mimba na mumewe wana stahili kuhakikisha kuwa mama ana hudhuria kliniki zote anavyo paswa. Baada ya mama kufahamu kuwa ana mimba, anastahili kuanza kliniki kati ya wiki ya nane hadi ya kumi na mbili. Wasiliana na daktari wako ama ukitembelee kituo cha afya kilicho karibu nawe.

Kliniki zinasaidia kufuatilia hali ya afya ya mama na pia kudhibitisha iwapo mtoto anakua ipasavyo. Kugundua, kutibu na kuzuia matatizo ya kiafya ambayo yanaweza ibuka.

  • Mazoezi mepesi

Kufanya shughuli za kimwili ni muhimu kwa mama aliye na mimba. Ni vyema kufanya mazoezi mepesi ukiongozwa na mtaalum wa mazoezi aliye na vyeti. Kwani sio mazoezi yote yaliyo salama kwa mama aliye na mimba. La sivyo, mama anashauriwa kutembea kwa dakika angalau 30 kila siku.

  • Kufanya aerobics

mazoezi na ujauzito

Mara nyingi, mazoezi ya aina ya aerobics yana husishwa na watu wanao tamani kukata uzito. Mazoezi haya ni muhimu kama mojawapo ya maandalizi ya kujifungua kwa mama mwenye mimba. Aerobics za mama mwenye mimba ni tofauti na ya watu wengine. Yana usaidia moyo wa mama kuwa na nguvu zaidi, kupunguza maumivu ya ujauzito kama vile kuumwa na miguu.

  •  Kujipanga kifedha

Japokuwa huduma za mama kujifungua katika hospitali nyingi za umma ni bure, ni vyema wanandoa kujiandaa kifedha. Ikiwa mama atajifungua kupitia upasuaji, bila shaka kutakuwa na gharama. Kuna mahitaji mengi yanayo andamana na ujauzito. Kama vile kununua mahitaji ya mtoto na kulipia kliniki, mavazi ya mama na mengineyo.

  • Usafiri

Ni muhimu sana kwa wanandoa kufikiria kuhusu usafiri mama anapo kuwa na mimba. Namna atakavyo fika hospitalini ama anapo hudhuria kliniki. Atakaye msindikiza kwenda hospitalini na kumrejesha nyumbani.

Haya ni baadhi ya maandalizi ya kujifungua yaliyo muhimu kwa mama kabla ya kujifungua. Hakikisha kuwa uko makini kuya zingatia na kuhakikisha kuwa umepanga kila kitu inavyo stahili.

Chanzo: WebMD

Soma Pia: Chanzo Cha Kusongwa Na Mawazo Baada Ya Kujifungua Na Suluhu Lake!

Written by

Risper Nyakio