Uandalizi Muhimu Maishani Kabla Ya Kupata Mimba

Uandalizi Muhimu Maishani Kabla Ya Kupata Mimba

Ni muhimu pia kwa mwanamke kujua wakati ambapo ana rutuba zaidi. Kwani ataongeza nafasi zake za kupata mimba.

Kuna vitu vingi ambavyo wanandoa wanapaswa kuzingatia kabla ya kupata mimba. Makala haya yana kuelimisha kuhusu maandalizi muhimu kabla ya kupata mimba.

Maandalizi Kabla Ya Kupata Mimba

kupata mtoto baada ya miaka 35

Kabla ya wanandoa kufanya uamuzi wa kupata mtoto, wanapaswa kuwa na mjadala wazi kuhakikisha iwapo wana maoni sawa kuhusu mambo haya.

  1. Uwezo wenu wa kumhudumia mwanao

Mtoto ana mahitaji mengi ya kifedha, kihisia na wakati. Wanandoa wana stahili kujitathmini kuona iwapo wana wa uwezo wa kifedha wa kumhudumia mtoto wao. Kwa wakati, wanapaswa kuangalia kama mama anaweza chukua muda mbali na kazi kumhudumia mtoto hadi pale ambapo atahisi ako tayari kurudi kazini. Katika wakati huu, mnapaswa kujadili iwapo mama atakuwa anafanyia kazi nyumbani ama mwanamme ata tekeleza majukumu yote ya kinyumbani.

Kihisia, wote wawili wanapaswa kuwa wamekomaa kihisia na kufanya uamuzi kuwa wako tayari kuwa na kumtimiza majukumu ya kihisia ya mtoto.

maandalizi ya kupata mimba

2. Kukoma kutumia mbinu za kupanga uzazi

Kabla ya kuanza juhudi za kutunga mimba, wanandoa wanapaswa kukubaliana kuhusu wakati bora wanapo paswa kukoma kupanga uzazi.

Ni muhimu pia kwa mwanamke kujua wakati ambapo ana rutuba zaidi. Kwani ataongeza nafasi zake za kupata mimba. Kwa kawaida, siku ya 14 baada ya kuanza kipindi chako cha hedhi huwa siku ambayo mwanamke ana rutuba zaidi na ni rahisi kwake kupata mimba.

Kumbuka kuwa ikiwa mbinu ya kupanga uzazi mnayo tumia iliwekwa mwilini na daktari, msijaribu kutoa peke yenu. Endeni kwa kituo cha afya ili daktari aweze kutoa kifaa kilicho tumika kuwalinda dhidi ya kupata mimba.

3. Kumwona daktari

Kuna virutubisho muhimu ambavyo mama anapaswa kuchukua anapo taka kupata mimba. Kuzungumza na daktari ni muhimu ili aweze kuwashauri kuhusu mambo mnayo stahili kufanya ili kuongeza nafasi zenu za kutunga mimba haraka na pia kwa urahisi. Mwanamke anastahili kunywa tembe za virutubisho hivi: Vitamini D, iron, kalisi na foliki acid.

Mbali na hayo mama ana stahili kuanza kuishi maisha yenye afya. Kama vile kula lishe bora yenye virutubisho vinavyo hitajika mwilini. Kukoma kutumia sigara na pombe kwani vitu hivi vitatatiza mchakato wao wa kupata mimba.

Chanzo: WebMD

Soma PiaMwongozo Wa Mimba Wiki Baada Ya Nyingine

Written by

Risper Nyakio