Tarajia Mabadiliko Haya Ya Mwili Baada Ya Kujifungua

Tarajia Mabadiliko Haya Ya Mwili Baada Ya Kujifungua

Kujua mabadiliko ya kutarajia baada ya kujifungua kunamsaidia mama kujua jinsi ya kujitayarisha. Soma zaidi!

Haijalishi jinsi ulivyo jitayarisha, kujifungua mtoto kutabadilisha matarajio yako yote. Vitabu vya ujauzito na darasa za utunzaji kabla ya kujifungua zita kuelezea wiki baada ya wiki mambo yatakayo kutendekea hadi mtoto wako anapo zaliwa. Ama hata baada ya kujifungua. Kuna mabadiliko mengi mwilini yanayo fanyika baada ya kujifungua.

Ukweli ni kuwa inapo fika kwa kujifungua mtoto- kupitia kwa upasuaji wa C-section ama njia ya kawaida, jambo hilo litahisi kama kitu usicho kijua hata kama ulikuwa umesoma kuhusu mada hii.

Lakini ikiwa umejifungua na hauna uhakika kuhusu mabadiliko yanayo tendeka mwilini mwako, hapa kuna mabadiliko unayo tarajia kushuhudia.

Mabadiliko baada ya kujifungua: Ukweli Kuhusu Mabadiliko Baada Ya Kupata Mtoto

jinsi ya kupata mtoto mrembo

1.Bleeding (lochia)

Utaanza kuvuja damu kutoka kwa uke wako punde tu baada ya kujifungua. Mwanzoni, damu hii itakuwa nzito ila kwa wiki zinazo fuata, itapunguka. Kuvuja damu baada ya kujifungua hudumu kwa wiki 2 ama 3 lakini inaweza endelea hadi baada ya wiki 6.

Ni asili kwa uterasi yako kutoa damu na tishu ili kuta ya uterasi ili ifufuliwe na nyingine mpya. Tarajia uchungu sawa na wa kipindi chako cha hedhi. Damu itaanza ikiwa na rangi nyekundu ila itazidi kuwa nyepesi zaidi hadi iwe ya pinki na mwishowe rangi sawa na ya maziwa karibu na mwisho wa kipindi hicho cha kuvuja damu.

Una shauriwa kutumia pedi badala ya tampons unapo shuhudia kuvuja damu baada ya kujifungua.

Ukigundua kuwa kiwango cha damu hakipunguki, wasiliana na daktari wako, huenda ikawa ulipata jeraha wakati wa kujifungua.

2.Kushonwa

Baadhi ya wanawake huhitaji kupasuliwa karibu na uke ili kurahisha kujifungua. Ila sio wanawake wote wanao hitaji utaratibu huu. Kushonwa ni muhimu kwa wanawake walio pasuliwa wakati wa kujifungua. Na kutunza mishono ni muhimu sana baada ya kujifungua.

Ni muhimu kuhakikisha sehemu hiyo ni safi kwa kusafisha mishono hiyo kila siku. Kwa angalau dakika 10 kila siku, unapaswa kuruhusu sehemu hiyo ipunge hewa ili usipate maambukizi. Ikiwa bado una vuja damu, toa chupi inayo kubana kwa muda.

Daktari wako anaweza kushauri dawa za kutuliza maumivu za kutumia kupunguza uchungu.

3. Tumbo yako itakuwa tofauti

Mabadiliko baada ya kujifungua:

Kwa sababu mwili wako umepanuka kutengeneza nafasi ya kuishi ya mtoto wako, kuna maana kuwa itachukua muda kurejesha shepu yake ya awali. Baada ya kujifungua, tarajia ngozi iliyo legea.

4. Chuchu zako

Kwa sasa kwani umejifungua mtoto, matiti yako yatapitia mabadiliko kadha wa kadha. Utahisi chuchu zako zina bana na ni laini mwili wako unapo anza kutoa maziwa ya mama ya mtoto wako. Sindiria nzuri ni muhimu kupunguza uchungu.

Hitimisho

Unapo jua unacho paswa kutarajia baada ya kujifungua, mabadiliko yanayo tendeka baada ya kujifungua haya kushtua sana. Tume orodhesha baadhi ya mabadiliko muhimu mwilini yanayo tendeka baada ya kujifungua ili uweze kutayarisha akili yako.

Vyanzo: nct.org.uk

NHS

Soma pia:Mwongozo Wa Sindano Unazo Hitaji Ukiwa Na Mimba

Written by

Risper Nyakio