Kufahamu kuwa una mimba unapokuwa tayari kuwa mama ni baadhi ya habari nzuri zaidi ambazo mwanamke anaweza pata. Kufahamu kuwa baada ya safari ya mimba, ataweza kumkumbatia mtoto wake mikononi mwake. Hata hivyo, hakuna anayemtayarisha mama kuhusu mabadiliko usiyotarajia baada ya kujifungua. Kila mwanamke ni tofauti na mabadiliko haya huwa tofauti kwa kila mwanamke.
Mabadiliko usiyotarajia baada ya kujifungua
- Tumbo kubaki kubwa

Nini hufanyika baada ya mama kujifungua? Tumbo huisha papo hapo? La hasha, huchukua muda. Baada ya mama kupata mtoto, tumbo hairudi ilivyokuwa kabla ya kupata mimba kwa kasi. Huchukua muda wa wiki 8 ama zaidi kabla ya tumbo kurudi kwa saizi yake ya kawaida kabla ya mimba. Ili tumbo iishe baada ya kupata mtoto, mama anastahili kula lishe bora na kufanya mazoezi baada ya kupona.
2. Hamu ya mapenzi kwenda chini

Baada ya kujifungua, mama anashauriwa kujitenga na kufanya mapenzi hadi anapopona, daktari humshauri kipindi bora kwake. Huenda ukatarajia kuwa baada ya kipindi hicho, atakuwa na hamu ya juu ya kufanya mapenzi. La. Mabadiliko mengi yanayotokea mwilini, kama kuongeza uzito wa mwili huenda yakamfanya mama kukosa kujiona anapendeza. Hali hii humfanya ajitenge na kuwa uchi mbele ya mtu mwingine. Mabadiliko ya homoni huenda yakamfanya akose hamu ya kufanya mapenzi na mchumba wake. Pia hana wakati tosha kwani wakati mwingi anamchunga mtoto mdogo.
3. Saizi ya maziwa
Mwanamke anapokuwa na mimba, saizi ya maziwa huongezeka. Kwani maziwa ndiyo chakula cha kipekee cha mtoto hadi anapofika miezi tisa. Mtoto anapokoma kunyonya, maziwa ya mama hupunguka kwa saizi. Tarajia punguko la saizi ya sindiria unazovalia mtoto wako anapoacha kunyonya.
4. Kupoteza nywele

Mabadiliko haya sio maarufu kwa wanawake wengi. Hata hivyo, kiwango cha wanawake huripoti kupoteza nywele wanapokuwa na mimba. Nywele za kichwani hupunguka ama kukatika katika safari ya ujauzito. Mabadiliko haya yanahusishwa na kiwango cha chini cha kichocheo cha estrogen. Wanawake wanaokuwa na viwango vya juu vya estrogen hawashuhudii mabadiliko haya kwani homoni hii hulinda dhidi ya nywele za kichwani kukatika.Baada ya kujifungua, ukuaji wa nywele za kichwani hurudi kuwa kawaida.
5. Kuongeza uzito wa mwili

Wanawake huongeza uzito wanapokuwa na mimba. Wengi wao hutarajia kuwa watapunguza uzito huu wanapoanzia kunyonyesha watoto. Kunyonyesha mtoto husaidia kukata uzito, lakini sio kwa kiwango cha juu. Mama anapokula chakula kingi bila kuzingatia kula mara tu anapohisi njaa, hushuhudia kuongezeka kwa uzito kwa kasi. Ni vyema kwa mama kula anapohisi njaa tu na pia kula chakula chenye afya. Huku akijitenga na vyakula vilivyo chakatwa, vilivyokaangwa kwa ufuta mwingi na vinywaji vyenye sukari nyingi ya kuongezwa kama soda.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Kupunguza Ufuta Kwenye Tumbo: Masharti 5 Ya Kufuata Kupunguza Uzito Kwa Kasi