Mabadiliko 7 Ya Ajabu Yanayo Tendeka Ukiwa Na Mimba Usiyo Yafahamu

Mabadiliko 7 Ya Ajabu Yanayo Tendeka Ukiwa Na Mimba Usiyo Yafahamu

Kuona vyema ni mojawapo ya mabadiliko katika mimba yasiyo angaziwa kwa umakini. Tuna orodhesha mabadiliko zaidi ambayo watu hawa fahamu.

Mwili wako hupitia mabadiliko mengi unapokuwa na mimba. Mbali na mabadiliko yanayo julikana, kama vile tumbo kuwa kubwa na ugonjwa wa asubuhi, kuna mabadiliko machache ya ajabu ya mimba ambayo haya julikani sana.

Mabadiliko ya ajabu ya mimba

  1. "Hiyo ni harufu ya nini?"

mabadiliko ya ajabu ya mimba

Katika trimesta ya kwanza, huenda ukagundua kuwa akili yako yina chukuliwa na harufu. Baadhi ya harufu huenda zika kufanya kuhisi vibaya ama kuku kasirisha na kuzidisha ugonjwa wako wa asubuhi. Habari nzuri ni kuwa, huku kunapaswa kupunguka baada ya trimesta ya kwanza.

2. Homa ya mimba (rhinitis)

Ukijipata kuwa una homa ukiwa na mimba, usiwe na shaka kwani ni kawaida. Kiwango cha juu cha damu kwenye mwili wako unapokuwa na mimba kinaweza sababisha kufura kwa mishipa ya damu iliyoko kwenye mapua na kusababisha kufungana. Kulingana na BabyCenter, hadi asilimia 30 ya wanawake wenye mimba hutatizika kutokana na mapua yaliyo fungamana bila kuwa na mizio ama maambukizi yoyote. Huenda ukashuhudia tatizo hili kama mwezi wa pili na huendelea kuwa mbaya ujauzito wako unapo endelea kukua na kupunguka baada ya kujifungua.

3. Je, naonja damu? (gingivitis)

Huenda ukagundua kuwa ufizi wako wa meno una fura na kuwa laini na kutoa damu baada ya kusugua meno. Ufizi wa meno unao toa damu una athiri karibu nusu ya wanawake wanao tarajia, na ambao mabadiliko ya homoni yana fanya midomo yao kuwa nyeti kwa bakteria. Hakikisha kuwa unafuata usafi unao faa wa meno na usiwe na hofu ya kwenda kwa daktari wa meno.

4. Kuto tosheleka

Wanawake wengi hushuhudia ongezeko la hamu ya kufanya mapenzi kufuatia mabadiliko ya homoni wanazo shuhudia, hasa viwango vya homoni za testosterone na progesterone.

Kila mwanamke ni tofauti. Badhi yao huenda wakawa na vipindi sugu vya ugonjwa wa asubuhi na kukosa hamu ya kufanya mapenzi. Wakati ambapo wengine huenda wakawa na hamu ya kufanya ngono wakati wote. Chochote ambacho utahisi, hakikisha kuwa unaongea na mchumba wako.

5. Naona vyema sasa

jinsi ya kupata mtoto mrembo

Wakati wa ujauzito, mama hushuhudia mabadiliko mengi mwilini hasa katika viwango vya homoni, mzunguko wa damu mwilini na huenda yaka athiri uwezo wake wa kuona. Kwa sababu hii, sio wazo la busara kununua miwani mpya. Mabadiliko ya uwezo wa kuona yanayo andamana na ujauzito sio ya kudumu, na yata badilika miezi michache baada ya kujifungua. Walakini, ikiwa una bahati, huenda ukabadilisha uwezo wako wa kuona milele.

6. Kusahau ovyo

Ukijipata kuwa una sahau ovyo ukiwa na mimba, usiwe na shaka. Jambo hili hututendekea sote. Ujauzito hau athiri akili yako kifizikia, lakini unakufanya kuhisi una kwazwa kimawazo ama kuchoka sana na kukufanya usifikirie kwa kasi. Mara nyingi, utakuwa na mawazo kuhusu kujitayarisha kwa sababu ya mtoto unaye taraji, na homoni nyingi huenda zika athiri akili yako. Jitunze kwa kuzingatia utaratibu wako wa kulala na uhakikishe kuwa una pumzika vya kutosha.

7. Nilikuwa na ndoto ya kushangaza

Asilimia kubwa ya wanawake huwa na ndoto wazi wanapokuwa na mimba. Kinacho sababisha hakija dhibitika, huenda ikawa ni kwa sababu ya homoni. Lakini pia huenda ikawa ni kufuatia mabadiliko ya mtindo wa kulala. Kulingana na wataalum, wanawake waja wazito wana usingizi unao katizwa kwa sana, na wanapo amka kutoka kwa usingizi mwepesi, wana nafasi zaidi za kukumbuka walicho ota. Hofu zako na matarajio ya kuwa mama na ujauzito huenda yaka onekana kwenye ndoto zako.

Soma Pia:Jinsia Ya Kujua Iwapo Una Mimba Kabla Ya Kufanya Kipimo

Written by

Risper Nyakio