Shukrani kwa teknolojia ya kisasa, ujumbe kuhusu mimba na mambo ya kutarajia uko kila mahali. Mwanamke anapo mtembelea daktari wake na katika kliniki, anapata ujumbe kuhusu ujauzito. Jinsi ya kujitayarisha kuwa mama, na vyakula anavyo paswa kuchukua. Hata hivyo, kuna mabadiliko ya kushangaza katika mimba ambayo wanawake hukumbana nayo. Tazama!
Mabadiliko ya kushangaza katika mimba
- Kushindwa kumakinika

Katika trimesta ya kwanza, ugonjwa wa asubuhi humfanya mama kuhisi amechoka kifizikia na kiakili. Hata baada ya kulala kwa masaa manane yanayo shauriwa, mama bado atahisi uchovu. Huenda akalemewa kufanya baadhi ya mambo aliyo kuwa amezoea kufanya hapo awali.
Mabadiliko ya homoni ya HCG mwilini na shaka za mtoto anaye kua tumboni, kazi, familia na shaka zingine za maisha. Mama anapaswa kutengeneza makumbusho ya vitu muhimu anazo taka kufanya siku hiyo.
2. Nambari ya sindiria
Ongezeko la saizi ya sindiria ni mojawapo ya ishara za kwanza za mimba. Matiti za mama hufura na kuongezeka kwa saizi katika trimesta ya kwanza ya mimba. Mabadiliko yanayo sababishwa na ongezeko la vichocheo vya estrogen na progesterone. Hata hivyo, matiti huzidi kukua katika safari yote ya mimba.
Mwanamke anashauriwa kubadili saizi ya sindiria kadri chuchu zake zinavyo zidi kukua.
3. Mhemko wa hisia
Mhemko wa hisia huwa kawaida katika mimba. Kubadilika kwa homoni mwilini hufanya chuchu za mama ziwe nyeti. Kwa wanawake wanao tatizika na uchungu katika hedhi huwa na mhemko wa hisia zaidi katika mimba. Mwanamke anapo pata hisia hizi, huwa na furaha dakika moja kisha kuhisi ana udhika na kila kitu dakika nyingine.
Mara nyingi mhemko huu wa hisia huwa katika trimesta ya kwanza ya mimba. Wanawake wengine huenda wakajipata wakilia bila sababu. Kuwakasirikia wachumba wao na wanafamilia ovyo bila sababu.
4. Ngozi ya mama

Mama anapo kuwa na mimba, ngozi yake hung'aa. Mabadiliko ya kawaida katika mimba kufuatia mabadiliko ya viwango vya homoni mwilini. Hata hivyo, kuna imani kuwa uso wa mama hubadilika kufuatia jinsia ya mtoto anaye kuwa naye tumboni. Ikiwa ana tarajia mtoto wa kike, ngozi yake ya uso itakuwa na upele. Kwani mtoto atachukua urembo wake. Na anapo tarajia mtoto wa kiume, uso wake utang'aa. Hii ni imani tu isiyo egemezwa kwa njia yoyote ile na sayansi.
Mama anapo pata upele kwenye uso, anapaswa kuwasiliana na mtaalum wa ngozi. Amshauri kuhusu utaratibu wa ngozi anaopaswa kufuata.
5. Nambari ya kiatu
Katika mimba, mabadiliko mengi yanafanyika mwilini. Mwanamke atahitaji mavazi makubwa yanayo mtoshea kwani ataongeza uzito. Kunenepa mwili kutafanya miguu yake inenepe pia. Na atahitajika kununua viatu vikubwa.
Anapo punguza uzito baada ya kujifungua, huenda akarudia viatu vyake vya hapo awali. Ni muhimu kuvalia viatu na mavazi yasiyo m-bana.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Jinsi Ya Kuzuia Kutunga Mimba Kiasili Baada Ya Ngono