Madaktari Bora Zaidi Wa Watoto Nchini Nigeria

Madaktari Bora Zaidi Wa Watoto Nchini Nigeria

Kutafuta huduma za kimatibabu huenda kuka kutatiza sana. Hasa unapo taka kuwajua madaktari wa nchi tofauti wanao sifika kwa kazi yao nzuri ya kuwatibu watoto ikiwemo hali zingine na hata watu wazima. Kutafuta madaktari bora wa watoto huenda kukawa na changamoto nyingi. Lazima uwe makini kwani kosa ndogo huenda lika mwathiri mtoto pakubwa. Pia unapaswa kuwa makini na mtaalum wa watoto unaye mchagua kwa sababu huwezi penda kuchagua daktari kisha upige foleni ndefu unapo enda kumtembelea. Tume orodhesha madaktari bora zaidi wa watoto nchini Nigeria na anwani zao. Chagua aliye karibu zaidi na wewe na aliye na vyeti unavyo hisi kuwa ni muhimu na lazima.

Madaktari bora zaidi wa watoto nchini Nigeria

Daktari Simisola Ajasa

Daktari Simisola Ajasa (MBBS) ni daktari mshauri wa watoto huko Lagos na mshiriki katika Mayriamville Medical Centre (MMC). Amehitimu kama daktari wa matibabu kutoka chuo cha matibabu cha Chuo Kikuu cha Lagos na ana uzoefu wa zaidi ya miaka 10. Ana uzoefu wa matibabu ya watoto ya dharura, na pia ana vyeti vya matibabu ya kwanza. Mbali na hayo, yeye ni mtaalum wa wanandoa na kuwa shauri.

 

Anwani:

144, Bode Thomas Street,, Surulere, Lagos, Nigeria.

 

paediatricians in nigeria

Daktari Yashua Alkali Hamza

Daktari Yashua Alkali Hamza ni mshauri wa matibabu ya watoto na ana uspesheli wa afya ya uma na uzoefu wa madawa ya kinga na utafiti. Alikuwa mkubwa wa madaktari wa matibabu ya watoto katika mojawapo ya hospitali kubwa zaidi za umma, Murtala Mohammed Specialist Hospital, Kano; na amekuwa akihusika katika kudhibiti wa ubora katika vifaa tofauti vya umma na kibinafsi huko Kano na FCT.

Anwani

7, Fez Street Off Kumasi Crescent, Wuse II, FCT, Abuja, Nigeria.

Madaktari Bora Zaidi Wa Watoto Nchini Nigeria

Daktari Omotayo Fawi

Daktari mkuu wa watoto aliye hitimu kutoka chuo kikuu cha afya ya kisayansi cha Chuo Kikuu cha Ilorin mwaka wa 2000. Pia ni mmoja wa wataalum kutoka West College of Physicians na anapendelea Neonatology, Nephrology na Emergency Paediatrics. Ana uzoefu wa matibabu ya mechanical ventilator na CPAP na utunzaji wa dharura wa watoto wachanga na watoto walio zaliwa kabla ya kukomaa. Anaongoza madaktari wa watoto na ni miongoni mwa madaktari bora zaidi nchini.

Anwani

Udi Hills Close, Aso Drive, FCT, Abuja, Nigeria.

 

Daktari Olatunde Odusote

Mshauri aliye na uzoefu uliodhihirika kufuatia historia yake kwenye tasnia ya hospitali na utunzaji wa afya. Ana uzoefu wa uongozi wa utunzi wa afya, utunzaji wa afya, utafiti wa kliniki, huduma ya wateja na masomo ya matibabu.  Huduma za utunzaji wa afya na cheti kutoka Chuo Kikuu cha Matibabu cha South Africa.

 

Anwani

1-5 Oba Akinjobi street, Ikeja, Lagos, Nigeria.

Madaktari Bora Zaidi Wa Watoto Nchini Nigeria

Daktari Abiola Oladepo (FMCPaed, M.B; B.S.)

Ni daktari mshauri wa afya ya watoto na uspesheli wake ni Neonatology. Anapenda kufanya kazi na kutunza afya ya watoto na ana uzoefu wa utunzaji wa dharura wa watoto walio wagonjwa na watoto walio zaliwa kabla ya kukomaa.

Anwani

7 Ogalade Close, Off Ologun Agbaje Street, Victoria Island, Lagos Island, Lagos, Nigeria.

 

Hitimisho

Ni matumaini yetu kuwa orodha hii ya madaktari wa watoto Nigeria itakusaidia unapo mpeleka mtoto wako hospitalini mara ijayo.

Soma pia: The best gynaecologists in Lagos

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Lydia Ume kisha yakatafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio