Madaktari Wa Mimba Ya Cryptic Nigeria: Uwongo Kuwahusu Wafichuliwa

Madaktari Wa Mimba Ya Cryptic Nigeria: Uwongo Kuwahusu Wafichuliwa

Madaktari wa mimba ya cryptic Nigeria sio wapya hata. Hali hii imetaabisha wanawake wengi wa Nigeria kwa miaka mingi, ila, kwa bahati mbaya, watu wengi wanajua machache sana kuihusu.

Wanawake wenye mimba ya cryptic, iwapo hata wanajua wana mimba, wanaamini kuwa mtoto anajificha mahali ndani ya uterasi. Imani hii ni maarufu kwa sababu kuna kisa ambapo mwanamke anaamini ana mimba ila kifaa cha kuonyesha mtoto (ultrasound) haionyeshi fetusi. Na inawabidi madaktari waende hatua kubwa kumshawishi kuwa ako kweli.

Habari Zaidi Kuhusu Madaktari Wa Mimba Ya Cryptic Nigeria

Miezi michache iliyopita, polisi wa Nigeria waligundua kikundi cha madaktari wa uongo katika sehemu fulani ya mashariki mwa nchi. Watu hawa waliwatumia vibaya watu walio kuwa wana kata tamaa; wanawake waliokuwa na hamu kubwa ya kupata watoto wao.

Wange waalika wanawake hawa kwenye hospitali yao na kuanza kuwadunga sindano na homoni zilizo wafanya wahisi kana kwamba wana mimba. Ila, hakukuwa na mtoto, na maelezo yao yalikuwa ni mimba ya cryptic. Wali waahidi waathirika wao kuwa watoto walijificha mahali nje ya uterasi zao.

Wakati ambapo waathiriwa walibeba mimba yao isiyo onekana kwa muda unaofaa, madaktari waliwafanyia upasuaji wa C-section na waka patia wanawake hawa na watoto wa kununuliwa ama kutekwa nyara. Uwongo huu wa kujifungua kwa mimba ya cryptic Nigeria kulikuwa na mafanikio hadi pale ambapo polisi walishika washukiwa hao.

Mimba ya Cryptic ni Nini?

cryptic pregnancy doctors in Nigeria

Mimba ya cryptic ni pale ambapo hakuna ishara za kibiolojia za mimba kwenye mwanamke aliye na mimba. Kwa mara nyingi, viwango vya hCG huwa havitambuliki kwa wanawake walio na hali hii. Vipimo vya mimba vitatoka vikiwa na ishara hasi haijalishi iwapo ni vya damu ama vya mkojo.

Katika visa vingi, huenda mwanamke akakosa kujua ana mimba hata hadi pale ambapo ataingia katika uchungu wa uzazi. Hata kama baadhi ya wanawake na hali hii watajua kuwa wana mimba, utakuwa muda wa kukanganya kwao kwa sababu hawana ishara za mimba.

Mwanamke anapo pata mimba na ujauzito wa kawaida, placenta inatoa hCG na kuimwaga kwenye ukuta wa uterasi. Kutoka kwa uterasi, homoni hii ya mimba inamwagwa kwenye mkojo na damu. hCG inaendelea kuongezeka hadi pale ambapo inaweza onekana kwenye vipimo vya mimba vya damu na mkojo.

Katika mimba ya cryptic, mwili hautoi viwango vikubwa vya hCG kama ilivyo katika mimba ya kawaida. Kwa sababu hii, vipimo vita onyesha matokeo hasi. Pia, kwa sababu mwili bado haujapitia mabadiliko yafaayo ya homoni ili kuegemeza mtoto, mtoto atakaa kwa muda zaidi kwenye tumbo.

Fetusi itakaa kwa muda zaidi kwenye uterasi katika mimba ya cryptic, ila mtoto anapozaliwa, anakua kawaida.

Dalili za mimba ya cryptic

Ni kawaida kwa waadhiriwa wa kujifungua mimba ya cryptic Nigeria kupata dalili za mimba mara kwa mara. Baadhi ya wanawake huenda wakapuuza dalili hizi kwani sio za kawaida.

Baadhi ya dalili za mimba ya cryptic:

 • Vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida
 • Vipimo hasi vya mimba vya mkojo na damu
 • Ultrasound hasi
 • Mimba inayo kaa kwa muda wa miezi 22 hadi miaka  kwa kukosa viwango tosha vya homoni
 • Dalili za mimba zinazo potea na kuonekana
 • Baadhi ya wakati mimba ya cryptic haina dalili zozote

cryptic pregnancy doctors in Nigeria

Kinacho Sababisha Mimba Ya Cryptic

Wanawake wengi wanakumbana na tatizo la homoni kuto kuwa sawa huenda wakapata mimba ya cryptic. Walakini, kutokuwa sawa kwa homoni sio sababisho la pekee la hali hii.

Sababu zingine:

1. Polycystic ovarian syndrome (PCOS)

PCOS huenda ikasababisha mtiririko zaidi wa homini mwilini, na kuifanya iwe vigumu kutambua mimba kwa vipimo.

2. Ufuta wa chini wa mwili (low body fat)

Wakati ambapo asilimia ya ufuta wa mwili uko chini sana, huenda ikawa vigumu kupata vipimo kamili vya mimba. Kutokuwa sawa kwa homoni ni athari ya kuwa na ufuta wa mwili wa chini zaidi, na hii huenda ikaifanya iwe vigumu kupata vipimo sawa vya mimba.

3. Uthibiti wa uzalishaji (Birth control na emergency contraception)

Baadhi ya mbinu za kuthibiti uzalishaji huenda zikafanya mwili udhani kuwa hakuna mimba hata mwanamke anapokuwa nayo. Hii ni kwa sababu mbinu hizi hutoa homoni mwilini, na baadhi ya homoni hizi huenda zikafanya kuwa vigumu kugundua mimba kwa vipimo na ultrasound.

Tembe za asubuhi ya kuraukia na emergency contraceptives huenda zikasababisha hali hii. Huku kunatendeka pale ambapo tembe hizi zinakosa kufanya kazi ama iwapo mwanamke aliichukua akiwa amechelewa.

4.  Mimba ya hivi karibuni

Baada ya mwanamke kujifungua, huenda ikachukua muda kabla ya viwango vya homoni zake kurudi kawaida. Mambo huenda yakawa na tatizo iwapo mwanamke anapata mimba inayo karibiana na mimba ya awali.

5. Mimba angali bado ananyonyesha

Viwango vya homoni kwa wanawake wanao nyonyesha wakati wote huwa juu ya kawaida. Kwa hivyo, iwapo mama anaye nyonyesha ana mimba, huenda ikawa vigumu kwao kuwa na uhakika.

Mambo ya kutarajia katika mimba ya cryptic

Pregnancy Scam

 • Muda mrefu wa gestation
 • Uzito mdogo wa kujifungua
 • Uchungu wa uzazi wa muda mrefu
 • Hatari ya juu ya matatizo ya kuzaliwa

Madaktari wa mimba ya cryptic Nigeria: Hali zisizo husika

Kwani hali hii inachanganya sana, watu wengi baadhi ya wakati huhusisha chanzo chake kwa vitu ambavyo vinaweza athiri mimba ya mwanamke.

Mimba ya cryptic haisababishwi na:

 • Pepo mbaya
 • Mawazo mengi
 • Lishe
 • Mtindo wa maisha
 • Geni za mama na baba
 • DNA ya mama au baba

Kujifungua mimba ya cryptic Nigeria huenda ikawa ya kukanganya mwanamke anaye amini ana mimba hata pale ambapo hapana ishara kuthihirisha anacho fikiria. Kujua cha kutarajia na hali hii kutafanya iwe rahisi kwako kukabiliana nayo.

Kumbukumbu: Cryptic Pregnancy Support Group

Organic Facts

Soma pia: How to stop fibroids from growing during pregnancy

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio