Kuna idadi kubwa ya watu wanaotatizika na hali ya bloating siku hizi. Kuna madhara hasi ya gesi tumboni hali hii isipotatuliwa mapema ipasavyo. Vyanzo vya gesi kujaa tumboni huwa kama vile lactose intolerance ama mwili kushindwa kumeng'enya lactosi mwilini ama kuwa na saratani. Kufahamu ishara za tahadhari za kufura tumbo ni muhimu ili kupata usaidizi wa kimatibabu kabla ya hali kuwa dharura.
Madhara hasi ya gesi tumboni

Kupoteza uzito wa mwili. Hii ni mojawapo ya ishara hatari za gesi tumboni. Unapogundua kuwa una poteza uzito wa mwili bila kubadilisha lishe yako ama kuanza mazoezi makali, hicho ni chanzo cha shaka.
Maumivu makali ya tumbo. Gesi kujaa tumboni na kuandamana na kichefuchefu na kutapika ni ishara kuwa una kidonda kwenye tishu za tumbo. Kukaa muda mrefu bila hali hii kutatuliwa kunakuweka katika hatari na uchungu mwingi usioweza kustahimili. Pata matibabu kwa kasi.
Damu kwenye haja kubwa. Unaposhuhudia kuwa kufura tumbo kunako ambatana na kuenda haja kubwa yenye damu, hii ni ishara kuwa una tatizo kubwa zaidi. Huenda ikawa ishara ya saratani ya uterasi na ni vyema kufanyiwa vipimo.
Joto. Joto inayoambatana na kufura tumbo mara nyingi huwa kufuatia maambukizi. Sababu nyingine ya kupata matibabu kwa kasi.
Vyanzo vya kufura tumbo hatari

Saratani ya ovari. Ni baadhi ya saratani zisizo za kawaida, hata hivyo, husababisha vifo zaidi katika wanawake, hasa walio na umri zaidi ya miaka 50. Mbali na vifo, saratani ya ovari inasababisha ongezeko la uzito wa mwili kwa kasi na utasa.
Saratani ya uterasi. Mbali na kufura tumbo, saratani ya uterasi inaweza kusababisha kuvuja damu kwenye uke, uchungu wa pelviki ama kuhisi uchungu unapoenda haja ndogo.
Saratani ya tumbo. Katika siku za kwanza, saratani ya tumbo haina ishara, mbali husababisha vitu kama kutatizika kumeng'enya chakula, kufura tumbo, kutapika kupoteza uzito wa mwili, kichefuchefu na maumivu ya tumbo.
Gesi tumboni mara nyingi huwa hali inayojisuluhisha na kuisha baada ya siku chache bila matibabu yoyote. Ila, hali hii inapozidi na kuambatana na ishara kama damu kwenye haja kubwa, ni muhimu kufanyiwa vipimo kudhibitisha vyanzo vyake.
Soma Pia: Madhara Ya Tangawizi Kwa Afya Ya Mjamzito