Baada ya vipindi vingi chumbani cha kulala kujaribu kupata mimba, huenda hamu ya mwanamke ya kitendo cha mapenzi kufifia baada ya kushika mima. Ni jambo la kawaida na linalowafanyikia wanawake wengi na pia linaeleweka. Je, ni salama? Madhara ya kufanya mapenzi kwa mama mjamzito ni yapi? Kuna uwezekano wa kufanya mapenzi bila kumwumiza mama na fetusi.
Madhara ya kufanya mapenzi kwa mama mjamzito

Kufanya tendo la katika mimba ni salama kwa mama na mtoto anayekua tumboni kwani amelindwa na amniotic fluid. Hata hivyo, ni vyema kwa mama kuzungumza kuhusu ngono katika mimba na daktari wake kuhakikisha kuwa hatakuwa na matatizo.
Mama aliye na historia ya kupoteza mimba ako katika hatari ya juu ya kupoteza mimba tena na ni muhimu kwake kujadiliana kuhusu tendo la ndoa katika mimba na daktari wake. Kwa visa kama hivi, daktari anaweza kumshauri mama kujitenga na tendo la ndoa hasa katika miezi ya kwanza.
Hata kama mtoto analindwa na amniotic fluid, ni muhimu kwa mama mjamzito kuwa makini kwani maambukizi ya kingono yanahatarisha maisha yake. Mchumba wake anapaswa kujitenga na kuwa na wapenzi nje ya uhusiano wao.
Wakati ambapo tendo la ndoa sio salama katika mimba
- Mama anapokuwa na historia ya kupoteza mimba
- Mama mwenye historia ya kujifungua kabla ya wakati
- Maumivu ya tumbo yasiyoeleweka
- Gunia la amniotic kuvuja
- Kuwa na mimba ya zaidi ya mtoto mmoja
Manufaa ya kufanya mapenzi katika ujauzito

Wapenzi wanapata nafasi ya kutangamana. Ujauzito huwa kipindi chenye panda shuke nyingi kwa wanandoa wote wawili. Kupata muda wa kudumisha utangamano wao ni muhimu katika kipindi hiki.
Kupunguza uchungu na kukosa starehe. Mama hushuhudia uchungu katika mimba, kama vile kuumwa na mgongo, kufanya mapenzi kunasaidia kupunguza maumivu haya.
Kuboresha hisia zake. Mimba humfanya mama awe na hisia nyingi tofauti
Kumsaidia mama kulala vyema. Mapenzi katika mimba humsaidia mama kulala vyema na pia kutoa homoni za kumfanya ahisi vyema.
Mitindo salama ya kufanya mapenzi katika ujauzito

Katika mimba, ni muhimu kwa wanandoa kuzingatia mitindo ambayo ni salama kwa mama. Isiyomshinikiza wala kumfanya ahisi maumivu kwenye tumbo. Starehe kwake ni muhimu katika kipindi hiki. Ikiwa mtindo fulani mliokuwa mnaupenda hapo awali unamfanya mama akose starehe, ni muhimu kuuweka kando kwa sasa.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Njia Tofauti Ambazo Wanandoa Wanaweza Kufurahia Ngono Katika Mimba!