Kwa kawaida kina mama wengi wanaposhika mimba huegemea kutofanya mapenzi. Hii ni kwa kuwa wengi huwa na hofu kuwa inaweza kuathiri mtoto. Ila hii hofu ina msingi wowote na kuna madhara ya kufanya mapenzi kwa mjamzito?
Kuna Madhara Ya Kufanya Mapenzi Kwa Mjamzito?

Kabla ya kuangazia iwapo kuna madhara ya kufanya mapenzi kwa mjamzito ni vyema kuelewa tumbo la uzazi. Mtoto huchukua nafasi kwenye uterasi. Hapa huwa amezingirwa na tabaka linalojulikana kama amniotic fluid. Hili tabaka humkinga mtoto kutokana na ajali. Pia humkinga mtoto kutokana na maambukizi.
Pili, uterasi na njia ya uzazi huwa imetenganishwa na mlango unaojulikana kama servix. Huu mlango huwa kizuizi kwa chochote kinachoweza kujipenyeza kwenye uterasi na kumdhuru mtoto. Hizi kinga mbili huwa dhabiti na tosha kumsetiri mtoto kutokana na ajali ama maambukizi.
Kina mama wengi huwa na hofu kuwa kufanya mapenzi kunaweza kuathiri mtoto lakini kama tumevyoona hapo awali ni kuwa hilo sio sawa. Kwa hivyo inawezekana kwa mama mjamzito kujihusisha na kufanya mapenzi kipindi chote cha ujauzito hadi pale atakapojifungua bila hofu ya kumjeruhi mtoto.

Ila, kuna dalili ambazo zinaweza kuashiria hali ya hatari? Hizi ni kama vile:
- Una historia ya mimba kuharibika. Iwapo una historia ya kuharibika kwa mimba kufanya mapenzi wakati wa ujauzito kunaweza kuwa sio wazo nzuri. Hii ni kwa kuwa inaweza kuhatarisha ama kuongeza nafasi zako za kumpoteza mtoto
- Unavunja damu. Iwapo utagundua kwamba unavunja damu wakati wa kufanya mapenzi ni vyema kwanza kusitisha na kumwona daktari wako. Inaweza kuwa sio jambo la dharura ila kuondoa shaka ni vyema kupata ushauri
- Iwapo unahisi uchungu wakati wa kufanya mapenzi. Jambo lingine la kuzingatia ni kama unahisi uchungu wakati wa kufanya mapenzi. Hii inaweza kuwa ishara ya maambukizi. Kwanza pata ushauri wa daktari kwani maambukizi yanaweza kumwathiri mtoto ama njia ya uzazi
- Mabadiliko ya homoni. Kina mama huwa tofauti, kuna wale huwa na hamu na ya mapenzi ilihali wengine hawapendelei kabisa. Hii hutokana na mabadiliko ya homoni kipindi cha ujauzito. Ni vyema mama kuelewa kuwa hii huwa ni sawa kabisa na hakuna jambo la kuhofia
- Iwapo daktari wako ameshauri hivyo. Kama baada ya uchunguzi daktari atapendekeza kusitisha kufanya mapenzi ni vyema kufuata ushauri wa daktari
Ni wazi kuwa madhara ya kufanya mapenzi kwa mjamzito sio makuu ila kunapokuwa na ushauri wa daktari. Jambo la msingi ni kuzingatia staili salama wakati wa kufanya mapenzi ili mtoto asiumie.
Soma Pia: Maswali 7 Maarufu Kuhusu Ngono Katika Mimba