Kuna imani nyingi kuhusu kufanya mapenzi baada ya kujifungua. Je, ni salama kwa mama, utoaji wa maziwa ya mama utaathiriwa? Mama anaweza kupata mimba anapofanya ngono akinyonyesha? Kuna madhara ya kufanya mapenzi na mama anaye nyonyesha? Ni salama kufanya mapenzi kwa mama aliye jifungua.
Ila, ngoja wiki za kwanza mbili ziishe kabla ya kurejelea kufanya mapenzi, ili kuepuka kupata maambukizi. Kizazi kingali kina zidi kupona, kwa hivyo kurejelea mapenzi mapema sana huenda kukafanya mama apate maambukizi. Daktari wengi wanamshauri mama kungoja angalau wiki sita baada ya kujifungua kabla ya kufanya mapenzi.
Mama anaweza pata mimba anapo fanya mapenzi akinyonyesha?

Ni nadra kwa mama aliye jifungua na anaye nyonyesha kupata mimba kati ya miezi ya kwanza sita. Ila, kuna baadhi ya wanawake wanao tunga mimba. Kumbuka kuwa kunyonyesha sio mbinu ya kupanga uzazi. Haina uhakika wa asilimia 100.
Daktari wako atakushauri mbinu bora ya kuzuia mimba katika wakati huu unapo zidi kunyonyesha mchanga wako.
Athari za kunyonyesha kwa tendo la ndoa
Mabadiliko mengi hufanyika mwilini mwa mwanamke baada ya kujifungua.
Baadhi ya mabadiliko yanayo fanyika na kuathiri tendo la ndoa kati ya wanandoa ni:
- Ukavu wa uke wa mama. Mwanamke hukosa kupata utelezi unaohitajika ili kufanya mapenzi vizuri. Uke unapokuwa na ukavu, mama huenda akahisi uchungu katika tendo la kufanya mapenzi.
- Kukosa hamu ya kufanya mapenzi. Kupungua kwa kiwango cha homoni ya testerone mwilini mwa mwanamke huenda kukamfanya akose hamu ya kujiingiza katika tendo la ndoa. Ni kawaida kwa wanawake walio jifungua. Upe mwili wako muda upone.
- Ongezeko la homoni ya prolactin. Kichocheo hiki humfanya mama ahisi kuwa hana hamu ya mapenzi ama ametosheleka kingono.
Sababu za mama anaye nyonyesha kukosa hamu ya ngono

- Kuhisi uchovu. Hasa baada ya kutolala vya kutosha akimshughulikia mtoto
- Hofu kuwa kufanya mapenzi kutakuwa na athari hasi kwa mwili wake ama kumwumiza
- Hofu ya kutunga mimba angali ana nyonyesha
- Wasiwasi kuhusu mwili wake ulivyo badilika
Hakuna madhara ya kufanya mapenzi na mama anaye nyonyesha, ila ni vyema kuhakikisha kuwa mama wakati wote ana starehe, na ametosheka.
Chanzo: healthline
Soma Pia:Je, Kuna Uwezekano Wa Kukomesha Mimba Baada Ya Siku Nane?