Kuinama katika mimba ni salama kama mtoto amefunikwa ipasavyo na uterasi. Amniotic fluid humlinda mtoto dhidi ya maumivu na kumwezesha kusongesha mwili mama anapoinama. Kuinama humfanya mama ahisi hana starehe. Madhara ya kuinama kwa mjamzito huongezeka ujauzito unapozidi kukua.
Madhara ya kuinama kwa mjamzito

Kuinama katika trimesta ya kwanza
Katika trimesta ya kwanza, mtoto angali mchanga, kwa hivyo, ni vigumu kwake kuathiriwa na kuinama kwa mama. Placenta inasaidia katika kumlinda mtoto. Kwa wanawake walio na mimba ya hatari, huenda wakashauri wasiiname na madaktari wao.
Kuinama katika trimesta ya tatu
Japo mimba inavyozidi kukua, ndivyo hatari za kuinama zinavyozidi. Mtoto amekuwa mkubwa katika trimesta hii na kuathiri mwili na nishati ya mama. Tazama sababu kwanini ni hatari kwa mama mjamzito kuinama katika kipindi hiki.
Hatari ya kuhisi kizungu zungu
Kuinama hufanya damu kusafiri kwenye sehemu ya mbele ya kichwa na kumfanya ahisi kizungu zungu kana kwamba anataka kuanguka. Ni hatari kwa mama kwani kuanguka kunaweza mwumiza mtoto ama kumweka katika hatari ya kuvuja damu anapoanguka.
Katika trimesta ya tatu, mimba ya mama imekuwa kubwa. Huenda akalegea na kuanguka. Kuanguka katika trimesta ya tatu kuna athari nyingi hasi kama vile, kuvuja damu, kuharibika kwa mimba ama placenta kuharibiwa.

Mimba humfanya mama ahisi uchovu mwingi, hasa katika trimesta ya tatu kwani imekua kwa sana. Wakati huu, mama huenda akawa anaumwa na miguu na mgongo kufuatia uzito ulioongezeka wa mtoto. Kuinama kutafanya maumivu haya yazidi.
Kuinama kunashinikiza tumbo na kunaweza sababisha ongezeko la asidi mwilini na kumfanya mama apate kiungulia. Kiungulia katika mimba humfanya mama akose starehe.
Jinsi ya kuinama katika mimba
Baada ya kuangazia madhara ya kuinama kwa mjamzito, ni vyema kumjulisha mama jinsi anavyopaswa kuinama katika mimba. Anaweza kujaribu njia hizi.
- Anaweza kutandaza magoti kisha kuchuchumaa
- Kutumia mikono kuusitiri mwili anapoamka
- Kukalia kiti kisha kuokota anachotaka kwa upole na utaratibu
Lakini inapowezekana, ni vyema kwa mama kujitenga na kuinama anapokuwa na mimba hasa katika trimesta ya tatu.
Soma Pia: Je, Kuna Madhara Hasi Ya Kufanya Mapenzi Katika Mimba Kwa Mama Mjamzito