Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Madhara Ya Kukosa Usingizi Na Wakati Wa Kumwona Daktari

3 min read
Madhara Ya Kukosa Usingizi Na Wakati Wa Kumwona DaktariMadhara Ya Kukosa Usingizi Na Wakati Wa Kumwona Daktari

Madhara ya kukosa usingizi kwa muda mrefu ni kama vile ongezeko la kasi la uzani wa mwili, kusombwa na mawazo na utendaji kazi uliopunguka.

Kulingana na utafiti uliofanyika, karibu kila mtu hutatizika na hali ya kukosa usingizi mara kwa mara maishani. Madhara ya kukosa usingizi kwa muda mrefu ni kama vile utendaji wako wa kazi kuathiriwa. Baadhi ya sababu zinazosababisha kukosa usingizi usiku ni kama vile, utumiaji wa dawa za kulevya, unywaji wa pombe, kuwa na mawazo mengi ama utumizi wa dawa za kimatibabu.

Kuna aina mbili ya kukosa usingizi. Kukosa usingizi kwa msingi, maarufu kama acute insomnia. Hali hii huwa ya siku chache kisha inaisha. Kukosa usingizi kwa sekondari, maarufu kama chronic insomnia. Hali inayozidi kwa zaidi ya wiki tatu na mara nyingi husababishwa na matatizo ya kiafya.

Vyanzo vya kukosa usingizi

madhara ya kukosa usingizi

Insomnia ya kimsingi haina chanzo na huisha baada ya siku chache. Wakati ambapo insomnia ya sekondari husababishwa na tatizo mwilini. Kukosa usingizi kwa muda mfupi mara nyingi huletwa na:

  • Kuwa na mawazo mengi
  • Kuwa na ratiba ya usingizi dhafifu
  • Kula chakula kingi muda mfupi kabla ya kulala
  • Kutia shaka kuhusu jambo fulani ama tukio lijalo
  • Kutolala wakati maalum baada ya kazi ama shule

Sababu za kiafya zinazoleta kutopata usingizi ni kama vile:

  • Matatizo ya afya ya kiakili
  • Unywaji wa dawa za kupunguza mawazo ama uchungu
  • Kuwa na saratani
  • Ugonjwa wa moyo
  • Kuwa na asthma

Madhara ya kukosa usingizi

Kukosa usingizi usiku kwa muda mrefu kuna madhara hasi kwa afya. Insomnia ya muda mrefu inakuweka katika hatari zifuatazo.

  1. Hatari iliyoongezeka ya hali za kimatibabu

Kama vile:

  • Kuongezeka kwa uzani wa mwili
  • Mfumo wa kinga kuwa hafifu
  • Ugonjwa wa moyo
  • Shinikizo la juu la damu
  • Kisukari

2. Matatizo ya afya ya kiakili

  • Kusombwa na mawazo
  • Kuwa na shaka
  • Kuchanganyikiwa
  • Kutatizika kufanya uamuzi
  • Kukosa hamu ya kuishi

3. Hatari iliyoongezeka ya ajali

Kukosa usingizi tosha huathiri ubongo na kusababisha haya:

  • Utendaji kazi wako kazini
  • Kufeli shuleni ikiwa wewe ni mwanafunzi
  • Kukosa hamu ya tendo la ndoa
  • Uwezo wako wa kukumbuka kufifia

Sababu zinazoongeza hatari ya kukosa usingizi

madhara ya kukosa usingizi

  • Kulala mchana
  • Kutokuwa na ratiba ya kulala
  • Kutofanya mazoezi
  • Kupoteza mwanafamilia ama rafiki
  • Kuwa na mawazo mengi
  • Kufutwa kazi
  • Kutumia simu kitandani
  • Kufanya kazi usiku
  • Kuwa kwenye mazingira yenye kelele usiku
  • Unywaji wa vileo na kaffeini

Wakati wa kuzungumza na daktari

Hata kama sote hutatizika na kukosa usingizi mara kwa mara, ni muhimu kuwasiliana na daktari unapotatizika na hali hii kwa muda wa zaidi ya wiki tatu. Atakufanyia kipimo na kuuliza kuhusu ishara ulizo nazo ili kubaini chanzo cha tatizo lile kisha kukupa dawa zinazokufaa.

Chanzo: WebMD

Soma pia: Faida Za Usingizi Kiafya Na Jinsi Usingizi Unavyoathiri Maisha Yako

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Health
  • /
  • Madhara Ya Kukosa Usingizi Na Wakati Wa Kumwona Daktari
Share:
  • Je, Kiamsha Kinywa Kina Manufaa Mwilini?

    Je, Kiamsha Kinywa Kina Manufaa Mwilini?

  • Vyanzo 5 vya Kuhisi Uvimbe na Maumivu ya Tumbo

    Vyanzo 5 vya Kuhisi Uvimbe na Maumivu ya Tumbo

  • Dalili za Ugumba Kwa Wanaume na Jinsi ya Kujikinga Dhidi ya Hali Hii

    Dalili za Ugumba Kwa Wanaume na Jinsi ya Kujikinga Dhidi ya Hali Hii

  • Je, Kiamsha Kinywa Kina Manufaa Mwilini?

    Je, Kiamsha Kinywa Kina Manufaa Mwilini?

  • Vyanzo 5 vya Kuhisi Uvimbe na Maumivu ya Tumbo

    Vyanzo 5 vya Kuhisi Uvimbe na Maumivu ya Tumbo

  • Dalili za Ugumba Kwa Wanaume na Jinsi ya Kujikinga Dhidi ya Hali Hii

    Dalili za Ugumba Kwa Wanaume na Jinsi ya Kujikinga Dhidi ya Hali Hii

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it