Kula vyakula vyenye viungo imekuwa desturi ya wengi toka jadi. Viungo huongeza ladha ya chakula. Kiungo kimoja maarufu sana ni pilipili. Ila wakati wa ujauzito kina mama wengi hupenda kujitenga na viungo kwa kuhofia mimba. Kuna madhara ya kula pilipili kwa mama mjamzito?
Madhara Ya Kula Pilipili Kwa Mama Mjamzito

Pilipili huwa na kemikali inayofahamika kama capsaicin. Hii ndiyo husababisha muwasho na joto la pilipili. Pilipili huwa na mazoefu sana kwa sababu ya faida zake . Kina mama huchanganyikiwa iwapo ni vyema kuendelea kuitumia. Jibu ni kuwa ni sawa kabisa kutumia pilipili na pia kula chakula chenye viungo. Hamna ushahidi kuwa pilipili ina athari zozote kwenye mama ama mtoto.
Mambo Ya Kuzingatia Wakati Wa Ujauzito
- Ukali wa tumbo la kiungulia. Tumbo la kiungulia ni kawaida wakati wa ujauzito. Vyakula vyenye viungo kwa mara nyingi huchochea huu moto. Hasa katika trimesta ya kwanza. Pindi mtoto anavyokuwa mkubwa huweza kusukuma asidi ya tumbo ndani ya umio na kusababisha kiungulia
- Ugonjwa wa asubuhi. Vyakula vyenye viungo vinaweza kusababisha kichefuchefu ama ugonjwa wa asubuhi kuwa mbaya zaidi. Hivyo ni bora kuepuka vyakula vyenye viungo kipindi cha kwanza cha ujauzito
- Kula pilipili kunaweza kusababisha dalili za mzio kwa kina mama wengine. Iwapo umekuwa na dalili za mzio kabla ya ujauzito ni vyema kujiepusha na vyakula vyenye pilipili

Manufaa Ya Kutumia Pilipili Kwa mama mjamzito:
- Husaidia kusawasisha kiwango cha sukari kwenye damu
- Husaidia kuondoa mkusanyiko wa damu kwenye sehemu moja ya mwili
- Husaidia kufungua kwa haraka na kwa ufanisi pua zilizoziba kwa mafua na kuruhusu kupumua kwa urahisi
- Husaidia kupunguza kuwepo saratani ya kwenye tumbo
- Husaidia kuongeza kiwango cha metabolic ambayo husaidia kuchoma mafuta
- Husaidia kupunguza kiwango cha cholesterol na kupunguza kiwango cha fibrin kwenye damu
Maswali Ya Kawaida Juu Ya Madhara Ya Kula Pilipili Kwa Mama Mjamzito
Kula pilipili kali kunaweza kusababisha leba na kuzaliwa mapema?
Kuna dhana kuwa capsaicin kwenye pilipili huwa na hatari ya kusababisha kubana kwa misuli ya uterasi. Hivyo pilipili itaweza kuchochea leba. Hii njia ya asili ilitumika kuchochea kuzaliwa kwa mtoto ila ni mila isiyo na msingi wa kisayansi.
Iwapo pilipili husababisha ugonjwa wa teratogenesis?
Pilipili huwa na wingi wa vitamini A, virutubisho muhimu wakati wa ujauzito. Hii ikitumika kwa wingi itakuwa na hatari kwa ujauzito na kusababisha teratogenesis. Ugonjwa hatari sana ambao unaweza kusababisha kuharibika kwa fetasi. Ila ni ngumu kufikisha hivi viwango kwa kula pilipili pekee.
Soma Pia:Mapumziko Ya Kitanda Katika Mimba Na Athari Hasi Kwa Mama