Kwa kawaida usingizi huwa na manufaa kadhaa kwa binadamu. Lakini kama kila kilicho na manufaa pia huwa na madhara. Madhara ya kulala sana huwa yepi?
Madhara Ya Kulala Sana

Imebainika kutokana na utafiti kuwa, kulala kwa zaidi ya saa 9 na zaidi ya dakika 90 wakati wa mchana huongeza hatari ya mtu kupigwa na kiharusi. Huo utafiti ulionyesha kuwa wale ambao hawakuwa na tatizo la kupooza au shida nyingine kubwa za kiafya ni wale wanaolala chini ya saa nane.
Pia hatari ya kupooza ilionekana kuongezeka kwa asilimia 25 kwa watu ambao walipumzika kwa zaidi ya dakika 90 mchana. Wale ambao hulala kwa muda mrefu usiku na kulala muda mrefu wakati wa mchana wana uwezekano wa asilimia 85 ya kupatwa na hali ya kupooza mwili.
Wakati uchunguzi huo ukifanyika, watu walichunguzwa kwa muda wa miaka sita na 1557 kati yao walipooza kwenye harakati za kuchunguzwa. Kwa kawaida mtu mzima mwenye umri wa kati ya miaka 18-64 anahitaji saa 7-9 za kulala kila usiku.
Sababu za kuwa na usingizi mwingi
Kuna aina mbili za usingizi usioisha zinazofahamika kama aina ya msingi na ya sekondari . Aina ya msingi hutokea pale ambapo hakuna shida nyingine yoyote ndani ya mwili inayofahamika baada ya vipimo mbalimbali. Chanzo chake hudhaniwa kuwa madhaifu ndani ya mfumo wa umeme.
Aina ya sekondari ni ule usingizi usioisha na sababu zake zinafahamika. Dalili kuu za usingizi usioisha ni kupata uchovu mkali wa mwili unaodumu, kusinzia sinzia na kushindwa kuamka kwa wakati kutokana na kuwa na vipindi virefu vya kulala. Dalili zingine ni pamoja na kuishiwa na nguvu, kuwa mkali, kuwa na hofu , Kukosa hamu ya chakula, kupoteza kumbukumbu, kutojihisi kufanya chochote.

Kuna sababu nyingi ambazo huchangia usingizi usioisha aina ya sekondari. Hizi ni kama vile:
- Magonjwa ya usingizi kama narcolepsy na sleep apnea
- Kutolala vyema wakati wa usiku
- Kuwa na uzani mkubwa
- Matumizi ya pombe
- Majeraha ndani ya kichwa au magonjwa ya mfumo wa neva
- Matumizi ya dawa Jamii ya tranquilizers
- Msongo wa mawazo
Baadhi ya matatizo ya usingizi kupita kiasi hayawezi kuzuilika ila ni vyema kujikanga na vihatarishi.
- Kufanya mazingira unayolala kuwa rafiki
- Kupunguza matumizi ya pombe na kahawa
- Kuacha kutumia dawa zinazosababisha kusinzia
- Kutofanya kazi hadi usiku wa manane
- Kutokula mlo mzito wakati wa kulala
Kwa kawaida wengi hufahamu umuhimu wa usingizi ila wachache huelewa madhara ya kulala sana. Kupooza ni athari moja inayoongaza na inayotokana na kulala sana.
Chanzo: WebMd
Soma Pia:Manufaa 3 Ya Kumkanda Mtoto Kwa Mtoto Na Mama