Kukosa lishe tosha na bora katika ujauzito huwa na madhara zaidi na sio kwa mtoto peke yake. Afya ya mama itadhoofika huku mwili unapozidi kusitiri ukuaji wa fetusi tumboni. Kwani mwili wa mama hauna virutubisho tosha kuhimiza ukuaji bora. Madhara ya kutokula kwa mjamzito huongezeka kulingana na jinsi mama anavyokaa kabla ya kula tena baada ya mlo wake wa mwisho. Kukosa mlo mara kwa mara sio vibaya ila kukaa muda mrefu bila kula kutakuwa na athari nyingi hasi.
Madhara ya mjamzito kutokula

Matatizo ya kuzaliwa
Kukosa virutubisho muhimu mwilini kunasababisha matatizo ya kuzaliwa ama ulemavu. Mama asipokula vyema anapokuwa na mimba, mtoto atakosa virutubisho muhimu katika ukuaji wake. Kukosa kalisi tosha husababisha kuzaliwa kwa mtoto mwenye matatizo ya kiafya kama mifupa isiyo na nguvu. Mama anastahili kula vyakula vilivyo na kalisi nyingi kama mchicha, bidhaa za maziwa na samaki wa salmon.
Kujifungua kabla ya wakati
Kwa mwanamke anayetatizika zaidi na kutokula, huenda hali hiyo ikamfanya ajifungue kabla ya wakati. Mama pia ako katika hatari ya kupoteza mimba ama kujifungua mtoto aliyefariki. Iwapo mama atabeba mimba hadi trimesta ya mwisho, huenda akazaliwa akiwa na matatizo ya mafua ama moyo.
Afya ya mama kudhoofika

Mama asipokula apasavyo, ako katika hatari ya kukosa damu tosha mwilini. Anapokuwa na mimba, anastahili kula chakula tosha cha kuhimiza ukuaji wake na wa mtoto, kukosa kufanya hivi, kutasababisha kudhoofika kwa afya yake kwani mtoto anatumia virutubisho vyake kwa ukuaji wake. Mama anapokuwa na anaemia, atakosa nishati tosha mwilini na huenda akapata kizunguzungu.
Mama kutatizika kunyonyesha
Kuongeza uzito katika ujauzito humsaidia mama wakati wa kunyonyesha baada ya kujifungua. Wanawake wanaotatizika kukula wanapokuwa na mimba hutatizika kupata maziwa tosha ya mtoto. Mtoto hutegemea maziwa ya mama kupata vitamini muhimu katika ukuaji wake. Mama asipopata maziwa tosha ya mtoto, afya ya mtoto itaathirika.
Mama anapogundua kuwa anatatizika na kula anapokuwa na mimba, ni vyema kumweleza daktari wake ili ampe dawa zitakazo msaidia na hali yake.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Afya Yako Baada Ya Kupoteza Mimba, Fanya Haya!