Kipindi cha ujauzito huleta mabadiliko mengi mwilini mwa mwanamke. Haya huwa ni pamoja na kichefuchefu, machovu na pia ongezeko la uzani. Haya mabadiliko hushurutisha kuzingatia kwa mambo kama vile lishe bora, mazoezi, mapumziko na pia unywaji maji kwa wingi. Ila, kuna madhara ya maji baridi kwa mama mjamzito?
Madhara Ya Maji Baridi Kwa Mama Mjamzito

- Kunywa maji baridi hujulikana kugandisha mafuta yaliyopo ndani ya mwili wetu. Hii hali inapoendelea huweza kusababisha shinikizo la damu kwani hukwamisha mzunguko mnyoofu wa damu mwilini.
- Maji baridi huhatarisha mwili kwani huhijati nguvu ya ziada kuyapasha joto. Maji baridi hayawezi kutumika na mwili lazima kwanza yapashwe joto.
- Maji baridi hujulikana kuunda kamasi nyingi kwenye mfumo wa kupumua na hivyo kusababisha msongamano na hatari ya maambukizi ya koo.
- Mtu anapokunywa maji baridi baada ya lishe, maji yale yanapopita kwenye tumbo husababisha kugandisha kwa mafuta yaliyo kwenye chakula. Hiki kitendo husababisha usagaji wa chakula kuwa polepole na kuchangia ukosefu wa choo.
- Pia wakati chakula kinapochelewa kusagwa kwa sababu ya kuganda, hukutana na asidi iliyoko tumboni. Hii huyeyusha mafuta kwa haraka kuliko chakula na baada ya muda husababisha saratani ya tumbo.

Faida Za Maji Baridi Kwa Mama Mjamzito
- Inapambana na kiharusi cha joto
Wakati jua limewaka kwa ukali sana ni vyema kutumia maji ya baridi. Hii hupunguza uwezekano wa kupatwa na kiharusi cha joto.
- Kinywaji kizuri baada ya mazoezi
Mama mjamzito anapofanya mazoezi joto la mwili huongezeka kutoka ndani. Katika hali kama hii ni vyema kunywa maji baridi ili kupunguza joto mwilini.
Umuhimu Wa Kunywa Maji Mengi Kwa Mama Mjamzito
- Unywaji maji husaidia katika utoaji wa sumu mwilini
- Maji huwa muhimu katika kutengeneza amniotic fluid. Hii huhitajika katika ukuaji vizuri wa mtoto aliye tumboni
- Maji humkinga mama mjamzito kutokana na maambukizi ya njia ya mkojo. Katika kipindi cha ujauzito mama huwa na uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa ya njia ya mkojo ama UTI.
- Maji hufanya ngozi ya mama kuwa nyororo na ya kuvutia
- Husaidia mama kuepuka kupata stretchmarks ama michirizi
- Maji huwa asilimia 70% ya ujenzi wa mwili na husaidia katika utendaji wa viungo vyote vya mwili
- Maji huongeza katika mzunguko wa damu
- Hubeba virutubisho vinavyotokana na chakula kwa viungo anuwai kupitia tishu
Hivyo, ni kweli kuwa kuna madhara ya maji baridi kwa mama mjamzito. Hii ikilingansishwa na yale ya vuguvugu ni bora kutumia ya vuguvugu.
Soma Pia: Hongera! Baada Ya Kungoja Miaka 10, Mwimbaji Evelyn Wanjiru Ana Mimba