Lishe ni muhimu kwa mama mjamzito ili kudumisha afya bora kwake na kuegemeza ukuaji wa fetusi. Tangawizi ni bora kwa mama katika safari yake ya ujauzito, hasa katika trimesta ya kwanza. Hata hivyo, ni muhimu kwa mama kuitumia ipasavyo bila kukiuka viwango. Kabla ya kutumia viungo vyovyote katika mimba, ni vyema kuwasiliana na daktari ili akupatie kibali. Tangawizi inamsaidia mama kukabiliana na hali ya kichefu chefu ama ugonjwa wa asubuhi ulio maarufu katika trimesta ya kwanza ya mimba. Soma ziaid kuhusu madhara ya tangawizi kwa mjamzito.
Madhara ya tangawizi kwa mjamzito

Tangawizi ina anuwai ya faida, kama vile:
- Kusaidia kuboresha kuchakata chakula tumboni
- Kumpa mama hamu ya kula
- Kupunguza cholesterol zaidi mwilini
- Kuboresha mzunguko wa damu mwilini
- Ni antibacterial na anti viral bora
Madhara hasi na chanya ya tangawizi katika mimba
Mama anaweza kunywa maji yaliyo ongezewa tangawizi ama kuongeza tangawizi iliyo kunwa kwenye chakula chake. Unapotumia iliyokunwa, epuka kutumia viwango vingi. Utumiaji wa viwango vilivyo zidi vya tangawizi huenda vikasababisha matatizo kama vile kutokwa na damu ama mimba kuharibika.
Mama mwenye mimba anahimizwa kutumia tangawizi katika hali yake mbichi kabla ya kuchakatwa. Kisha kuiongeza kwenye chakula, chai na maji. Iwapo mama ana baadhi ya hali hizi, anapaswa kuepuka kutumia chai ya tangawizi.
- Shinikizo la damu
- Kisukari
- Homa
- Vidonda vya tumbo
Faida zaidi za tangawizi

Kulingana na utafiti uliofanyika, kiungo cha tangawizi kimedhihirishwa kuwa na faida zifuatazo.
- Kupunguza uvimbe
- Kupunguza sukari kwenye damu
- Kupunguza cholesterol zaidi
- Kulinda dhidi ya kukolea kwa damu
- Kulinda dhidi ya ugonjwa wa Alzheimer
Mama mjamzito ana jukumu la kuchunga afya yake na ya mtoto anayekua tumboni mwake. Ni muhimu kwake kuwa makini na kitu chochote anacho kula. Iwapo una shaka kuhusu chakula chochote, wasiliana na daktari ili akueleze ikiwa ni salama kwako kutumia kiungo chochote katika hali hiyo.
Chanzo: Healthline
Soma Pia:Utunzaji Katika Mimba: Jinsi Ambavyo Mama Anaweza Kujitunza Anapokuwa Na Mimba