Kuwa Makini Kuona Hatua Hizi Katika Mtoto Wako Wa Miezi Mitatu

Kuwa Makini Kuona Hatua Hizi Katika Mtoto Wako Wa Miezi Mitatu

Kama mzazi, kumbuka kuwa watoto wote hutofautiana. Usiwe na shaka unapo ona kuwa mtoto wako amekosa kutimiza hatua fulani hasa kama alizaliwa kabla ya miezi tisa kufika.

Katika mwezi wa tatu, mtoto wako ameanzia kuwa mkubwa na kuanza kufahamu mambo yanayo endelea kwa mazingira yake. Katika makala haya, tungependa kukuelimisha kuhusu maendeleo ya mtoto wa miezi mitatu na hatua muhimu unazo tarajia kuona katika mwezi huu.

Kumbuka kuwa hata tunapo angalia hatua hizi kwa watoto wako, kila mtoto ni wa kipekee na tofauti na mwingine. Na watoto hukua kwa kasi tofauti kwa hivyo usitarajie mtoto wako akue sawa na mwingine.

Maendeleo ya mtoto wa miezi mitatu: maendeleo ya mwendo

maendeleo ya mtoto wa miezi mitatu

Mtoto wa miezi mitatu anaanza kupunguza kushtuka aliko thibitisha katika mwezi wake wa kwanza. Nguvu za shingo yake zina imarika. Unapo mshika na kumsimamisha, kichwa chake haki legei. Nguvu zake za mwili wa upande wa juu zinatosha kusitiri kichwa chake na kifua na mikono yake anapolala kwa tumbo. Pia, nguvu za upande wa chini zinaegemeza miguu yake kurusha mateke. Ukiendelea kuwa makini kumtazama mtoto wako, utagundua kuwa mikono na macho yake zina andamana. Mikono yake ina mwendo wa kuja pamoja, kufunguka ama kujaribu kushika vitu vyenye rangi inayo ng'aa karibu naye na kujaribu kuziweka mdomoni.

Hatua na maendeleo muhimu kwa mtoto: Usingizi

mtoto kutoa jasho jingi akiwa amelala

Mfumo wa neva wa mtoto wako katika hatua hii bado una zidi kukua na kuimarika. Tumbo yake ina uwezo wa kuchakata maziwa zaidi ama formula. Mabadiliko haya yanaweza muwezesha mtoto kulala kwa masaa sita ama saba bila kuamka. Katika wakati huu, mama anaweza pata chanya cha kulala pia.

Mtoto wako akiamka katikati ya usiku, usikuwe na mbio ya kumchukua. Ngoja kidogo uone kama ataendelea kulala ama atazidi kulala. Akiendelea kulia, mchukue na umlishe ama umbadili nepi kwa giza. Kwani kuwasha sitima kutamfanya aamke na ashindwe kulala tena. Kufanya hivi kutamsaidia kutofautisha usiku na mchana na kujua kuwa, usiku ni wakati wa kulala tu.

Hatua na maendeleo muhimu kwa mtoto: Uwezo wake

Uwezo wa mwanao wa kuona na kusikia katika hatua hii umeanza kuimarika. Unapo ita mtoto wako ama kuongea, nafasi kubwa ni ata geuka na kutabasamu. Pia wameanza kusikiza muziki. Anapenda kuangalia vidoli vyenye rangi za kung'aa. Anafurahia kuona nyuso tofauti na unapo mwangalia ana kuangalia pia.

Hatua na maendeleo: Mazungumzo

maendeleo ya mtoto wa miezi mitatu

Katika mwezi wa tatu, mtoto hatumii kulia kama njia pekee ya mazungumzo. Mtoto hapaswi kulia zaidi ya lisaa limoja kila siku. Kulia kukizidi, ratibisha mkutano wa kumwona mtaalum wa watoto, huenda akawa na matatizo ya kiafya yanayo mwathiri na kumfanya alie.  Ana tabasamu na watu maarufu kama tabasamu za jamii.

Badala ya kulia anapo taka kitu ama kunapokuwa na jambo lisilo sawa, anaanza kutaamka maneno kama 'ah' ama 'oh' ama kutoa sauti za kitoto. Wazazi wana shauriwa kuzungumza na watoto wao. Iga sauti za mwanao ama umjulishe unacho fanya kinacho endelea mkiwa pamoja. Mtoto atakusikiza kwa makini unacho sema na uso wako unapo ongea. Ukifanya hizi kwa muda, ataanza kuiga unacho sema na kufanya. Hii ni njia bora ya kutengeneza utangamano na mtoto wako.

Maendeleo ya mtoto wa miezi mitatu: Vidokezo muhimu

Kama mzazi, kumbuka kuwa watoto wote hutofautiana. Usiwe na shaka unapo ona kuwa mtoto wako amekosa kutimiza hatua fulani hasa kama alizaliwa kabla ya miezi tisa kufika. Kuwa makini kugundua mambo haya kwa mwanao na uwasiliane na daktari wako:

  • Asipo fuata watu na macho ama vitu unapo viweka mbele yake
  • Asipo tabasamu unapo mwongelesha
  • Kama hafanyi juhudi za kufikia vitu na kuviweka mdomoni
  • Kuto itikia anapo itwa kwa kuangalia ama kuonekana ana sumbuka kunapo kuwa na kelele nyingi

Kumbuka vitu hivi

  1. Kuna wataalum wa watoto wanao wapatia wazazi hasa wa mara ya kwanza kuhusu ulezi. Kama vile jinsi ya kumlisha mtoto, unavyo paswa kumshika. Unavyo hitajika kumsafisha na kumlaza.
  2. Kuna baadhi ya watu wanao shauri wazazi kuwaanzia watoto vyakula vigumu, lakini unapaswa kungoja hadi anapo timiza miezi sita.

Vyanzo: NHS, WebMD

Soma Pia:Mambo 6 Muhimu Mama Wote Wanapaswa Kufahamu Kabla Ya Kuwaanzishia Watoto Chakul Kigumu

Written by

Risper Nyakio