Kwa watu walio peke yao, wasio na wachumba, kupata mtu anaye wafaa huenda kukawa jambo gumu sana. Walakini, ukwele kuhusu kupata mchumba ni rahisi sana. Ila, watu wengi hawajui mahali pa kupatana nao ama jinsi ya kuanza. Iwapo uko tayari kupata mwenzi na kuwacha klabu ya watu wasio na wachumba. Makala haya yana kuelimisha mahali bora pa kupatana na mchumba wako. Kama bibilia inavyo sema, kila mtu ana mchumba ambaye Mungu alimuumbia.
Hatua za Kupatana na Mchumba Wako: Mahali Bora Pa Kupatana Na Mchumba Wako
- Hatua ya kwanza
Fahamu mchumba unaye mtaka
Hatua hii ya kwanza ni muhimu sana. Ikiwa una uhakika kuwa ungependa kuanza kutafuta mchumba, chukua kalamu na karatasi. Kisha uandike vitu ambavyo una angalia kwa mwanamme na vitu ambavyo lazima awe navyo. Anavyo kaa, tabia zake, dini yake, vitu vya ziada anavyo penda kufanya wakati wa mapumziko yake. Je, lazima muwe wa dini moja?

2. Hatua ya pili
Badilisha orodha hiyo iwe skeletoni ya mchumba unaye tafuta
Orodha yako inapaswa kuwa ya mtu haswa unaye tafuta. Ila ni vyema kufahamu kuwa huenda usitimize kupata mtu aliye na vitu vyote unavyo tafuta. Huenda ukafunga jicho lako kwa mambo mengine. Kwa kuangalia orodha hiyo, utafahamu vitu muhimu kwako unavyo angalia kwa mchumba utakaye mpata. Na huenda ukapata vitu ulivyo puuza na huenda vikawa muhimu kwako. Ni vyema kutafuta mtu ambaye mnapenda kupenda vitu sawa, kwa mfano, kuenda kanisani, kufanya mazoezi, kutembea na kadhalika.
3. Fahamu vitu ambavyo watu wengine hutafuta kwa wachumba
Kuna utafiti mwingi ulio chapishwa kuhusu vitu ambavyo wanawake wanatafuta kwa wanaume na vitu ambavyo wanaume wanatafuta kwa wanawake. Kufanya hivi kutakusaidia kujua vitu unavyo paswa kusisitiza unapo anza jukumu lako la kutafuta mchumba.
Wanaume wanatafuta: Utu, ucheshi, sura, kupendeza, pesa, dini, kazi kumjua kupitia kwa rafiki.
Wanawake wanajulikana kutafuta: Utu wa kupendeza, ucheshi, kupenda vitu sawa, maarifa, usafi, kupendeza, dini, pesa, talanta, kazi na hata sauti.
4. Kujipenda kwanza
Huwezi penda mtu mwingine ikiwa hujipendi kwanza. Kwa hivyo hakikisha kuwa unajipenda na ikiwa kuna sehemu ambazo hazikupendezi, fanya uwezavyo ili zipendeze. Iwapo unahisi una uzito mwingi, anza kufanya mazoezi, nunua nguo mpya, anza kunywa maji, anza utaratibu wa kutunza uso wako na kadhalika. Ili uwe na ujasiri wa kuongea na watu wengine. Kwa njia hii, akili na mwili wako zitakuwa kurasa sawa. Amini kuwa unahitaji mambo yote mazuri maishani.
5. Anza kutafuta mchumba wako
Jambo linalo watatiza watu wengi wasio na wachumba ni mahali pa kupatana nao. Kwa hivyo tuna kuelimisha kuhusu mahali bora zaidi pa kupatana na mchumba wako. Tafuta vikundi vya kijamii na sherehe ambapo huenda mchumba unaye mtafuta huenda akawa. Na mahali ambapo utaweza kuzungumza na watu wengi tofauti. Ni muhimu sana kwako kugundua mtu unaye mtafuta na mahali ambapo huenda ukapatana naye. Mahali bora zaidi pa kupatana na mtu ambaye ungependa kuwa na uhusiano naye ni mahali unapo penda kuwa wakati wako wa ziada. Kama vile vikundi vya watu wasio na wachumba, kanisani, mtandao wa kutafuta wachumba, kufanya mazoezi na kadhalika.
Kazini pia ni mahali ambapo watu hupatana na wachumba wao. Ila ni vyema kuwa makini kwani huenda kuka athiri kazi yako.
6. Usiwasukume watu mbali

Iwapo umekuwa peke yako kwa muda mrefu, huenda ikawa utawasukuma watu ama ukatae kuwa kwa uhusiano kwa sababu umezoea kuishi peke yako. Ila, ni vyema sana kuwa na mchumba kwani, huenda ukahisi upweke. Wape watu nafasi ya kukuonyesha mapenzi, na hakuna anaye jua, huenda ukapata mchumba uliye kuwa unatafuta wakati huo wote!
Mambo ya kufanya huku ukiendelea kumtafuta mchumba wako.
1. Omba Mungu akusaidie
Ni vyema kuomba ili umpate mtu atakaye kufanya uhisi mapenzi. Na Mungu atakuongoza.

2. Endelea kufanya kazi
Usikome kufanya kazi yako kwa sababu unamtafuta mchumba. Kama Ruth kutoka kwa bibilia, huenda ukampata mchumba wako unapo fanya kazi.
3. Wajulishe marafiki wako kuwa unatafuta mchumba
Huenda mchumba wako akawa ni rafiki wa rafiki yako. Wanaweza panga jinsi utakavyo patana na rafiki zao na kuona iwapo mna tafuta vitu sawa.
4. Kuwa mtulivu
Kutafuta na kumpata mchumba sio jambo linalo fanyika kwa siku moja. Kuwa mpole na uamini kuwa mtapatana kwa wakati unao faa.
Kumbukumbu: thescriptures.co.uk
Soma pia: Matamanio Ya Kingono Ambayo Wanawake Katika Ndoa Huwa Nayo