Maisha Baada Ya Mtoto Kuwasili: Mambo Ambayo Hukufahamu!

Maisha Baada Ya Mtoto Kuwasili: Mambo Ambayo Hukufahamu!

Watoto wanasoma kupitia kwa kuona na kuingiliana na mazingira. Utajipata ukiweka sura tofauti ili kumfurahisha mtoto wako.

Maisha baada ya kujifungua hubadilika sana. Uhusiano wako na mchumba wako pia utaathiriwa na kuwasili kwa mtoto. Tazama baadhi ya mambo yanayo tendeka katika maisha baada ya kujifungua!

Wakati wote ni wasaa wa mtoto

jinsi ya kujifungua mtoto shupavu

Hongera kwa kujifungua! Sasa wewe ni mama, wa mara ya kwanza ama unaitwa mama tena. Ratiba ya mtoto ni yako sasa. Baada ya kutoka hospitalini, watoto hulala hadi masaa 18 kwa siku. Ila sio kwa mara moja, wataamka mara kwa mara kunyonya, kubadilishwa nepi na kupakatwa kwa wingi. Baada ya wiki chache, watoto huanza kupata ratiba ya kulala, katika wakati hasa. Hakikisha kuwa anapo lala, unachukua muda kupumzika pia, kwani akiamka hutapata wasaa wa kulala.

Ratiba mpya ya wakati wa usiku

Kuwa na mtoto mdogo kuna maanisha haupati usingizi tosha kama ilivyo kuwa hapo awali. Ila, haitakuwa muda mrefu sana, lakini, hadi mtoto wako anapo lala usiku, mnapaswa kusaidiana kumshika mtoto usiku na mchumba wako. Hakikisha kuwa mchana haufanyi kazi nyingi mtoto wako anapo lala, chukua nafasi hiyo kulala pia.

Utakuwa na wageni wengi

maisha baada ya kujifungua

Marafiki na jamaa wako wata kutembelea kukuona pamoja na mtoto wako. Hakikisha kuwa wageni sio wagonjwa na kila mtu ana nawa mikono kabla ya kumshika mtoto. Ukihisi kuwa umechoka na unahitaji kupumzika, uko huru kuwaambia watembee wakati mwingine.

Uhusiano wako na mpenzi wako una badilika

Tofauti na hapo mbeleni, ambapo wakati wote ulikuwa wa mchumba wako, mambo yana badilika. Wakati mwingi, mama atakuwa akimtunza mtoto, kwa hivyo wakati wa kuwa na mchumba wake utapungua. Ni vyema kuhakikisha kuwa mnatenga wakati wa kuwa pamoja, angalau mara moja kwa wiki.

Umejiunga na chama cha dunia nzima

Chama maarufu kama ulezi. Mara tu, unapata marafiki wengi. Wageni pia wana tabasamu mnapo kutana nao. Wamama walio na watoto wakubwa wanaanza kukushauri. Kila mtu anataka kujua unavyo endelea.

Uso wako unampendeza mtoto wako

maisha baada ya kujifungua

Watoto wanasoma kupitia kwa kuona na kuingiliana na mazingira. Utajipata ukiweka sura tofauti ili kumfurahisha mtoto wako. Katika wiki za kwanza chache, utagundua kuwa mtoto wako ana usoma uso wako na baadaye kuanza kukuiga. Tabasamu na ufanye yote uwezavyo ili kumhimiza akuangalie kwa makini.

Unahitaji msaada

Watoto bila shaka ni baraka na wana leta furaha nyingi, ila, wana hitaji kutunzwa kwa makini. Usijaribu kufanya yote peke yako. Ni vyema kwa wachumba kusaidiana. Hakikisha unapata muda wako peke yako kila siku huku mpenzi wako akikusaidia kumtunza mtoto. Ikiwa hauna mchumba, uliza rafiki ama mwanafamilia mmoja akusaidie.

Watoto wana hitaji mazungumzo

Kuzungumza na mtoto ni muhimu sana ili kuhimiza utangamano kati yenu, na mtoto pia atasoma. Unavyo zidi kufanya hivi, ndivyo mambo haya mawili yanavyo tendeka, hakikisha kuwa unatumia maneno kamili unapo zungumza na mwanao.

Utafanya makosa

Hakuna mwongozo wa ulezi na kuwa mzazi bora. Ila, una gundua mbinu yako ya ulezi katika safari hii. Usiwe mgumu kwako sana. Hakuna mzazi ambaye hafanyi makosa yake. Na usiige mtindo wa mwingine, fanya kinacho mfaa mwanao. Ukiwa na shaka, zungumza na daktari wa mtoto anaye kushughulikia.

Soma piaJinsi Ya Kupunguza Uzito Baada Ya Kujifungua: Vidokezo Vya Nyumbani

Written by

Risper Nyakio