Kuna Uwezekano Wa Kutumia Maji Na Chumvi Kuzuia Mimba?

Kuna Uwezekano Wa Kutumia Maji Na Chumvi Kuzuia Mimba?

Kuna imani kuwa mwanamke anaweza kutumia maji na chumvi kuzuia mimba kwa kusafisha uke wake mara tu baada ya kufanya mapenzi.

Kwa wanawake ambao wangependa kutoa manii kwenye uke wao baada ya tendo la ndoa, kwa sababu yoyote ile. Kwa usafi wao ama hata kuepuka kupata mimba. Kuna njia kadha wa kadha ambazo wanaweza kutumia kusuluhisha hili, hata ingawa hakuna njia inayo egemezwa na sayansi kuwa inaweza toa manii kwenye uke. Unaweza kutumia maji na chumvi kuzuia mimba kwa kuosha uke wako.

Kuna njia zaidi ambazo mwanamke anaweza kutumia kusafisha uke wake bila matatizo. Ni vyema kwa mwanamke ikiwa hayuko tayari kuwa na mimba, kuwasiliana na daktari baada ya tendo la ndoa.

Njia tofauti za kusafisha uke baada ya tendo la ndoa

maji na chumvi kuzuia mimba

Katika tendo la ndoa, kibofu huingizwa kwenye uke wa mwanamke. Na katika kitendo hicho, manii kuachwa kwenye sehemu hii ya mwili. Ikiwa wanandoa hawakutumia kondomu walipo jihusisha katika mapenzi.

Sehemu ya mwili ya uke katika wanawake huwa na uwezo wa kujisafisha baada ya kufanya mapenzi. Lakini, kwa sababu tofauti, wanawake hufanya uamuzi wa kusafisha sehemu hii baada ya ngono. Njia rahisi zaidi ni kutumia maji ya vuguvugu safisha sehemu hii.

Kulingana na Shirika la Afya ya Kingono, wanawake wana shauriwa kutumia maji ya vuguvugu pamoja na sabuni isiyo na harufu. Hii ni kwa sababu harufu kali huenda ika sababisha mwanamke kukosa starehe na kubadili kiwango cha pH cha uke wake.

Manii yanaweza toka kwenye uke?

maji na chumvi kuzuia mimba

 

Kuna sababu tofauti za kutaka kutoa manii mwilini, kwa usafi, ama na lengo la kuzuia kupata mimba. Manii yanapo patana na yai mwilini mwa mwanamke, huli rutubisha na kusababisha ujauzito.

Kumbuka kuwa, manii yana uwezo wa kudumu mwilini mwa mwanamke baada ya ngono kwa kipindi cha siku tano ama saba. Hakuna njia ya kisayansi iliyo onekana kutoa manii mwilini. Hizi ni baadhi ya njia ambazo mwanamke anaweza kutumia

Kutumia maji na chumvi: Muda tu baada ya tendo la ndoa, mwanamke anaweza tumia maji ya vuguvugu pamoja na chumvi kusafisha uke wake.

Kuenda haja ndogo: Kuna baadhi ya watu wanao amini kuwa, kwenda msalani baada ya ngono husaidia kutoa manii mwilini. Kumbuka kuwa mkojo hutoka mwilini kupitia kwa urethra na manii huwa kwenye uke wa mwanamke.

Kukoga: Kuna imani kuwa, kuoga baada ya ngono hutoa manii mwilini. Lakini maji haya hayafikii uterasi, kwa hivyo hayatoi manii kutoka kwa uke.

Kuna imani kuwa mwanamke anaweza kutumia maji na chumvi kuzuia mimba kwa kusafisha uke wake mara tu baada ya kufanya mapenzi. Ila, hakuna egemezo la kisayansi kwa imani hii. Njia ya kipekee ya kuepuka mimba baada ya ngono ni kwa kuwasiliana na mtaalum wa afya.

Chanzo: WebMD

Soma PiaMbinu 3 Kuu Za Kuzuia Kutunga Mimba (Jinsi Ya Kuzuia Mimba)

Written by

Risper Nyakio