Mambo Yote Unayo Paswa Kujua Kukosa Maji Tosha Mwilini Ukiwa Na Mimba

Mambo Yote Unayo Paswa Kujua Kukosa Maji Tosha Mwilini Ukiwa Na Mimba

Maji tosha mwilini ukiwa na mimba ni muhimu sana kwa afya ya mama na mtoto. Kukosa maji yanayo hitajika huenda kuka hatarisha maisha yako na mtoto.

Kukosa maji tosha mwilini ukiwa na mimba hutendeka unaposa maji tosha mwilini kuwezesha utendaji kazi wake wa kawaida. Kwa hivyo, ni vyema kujaribu kutatua tatizo hili kwa kasi.

Kukosa Maji Mwilini Ukiwa Na Mimba: Unahitajika Kunywa Maji Kiasi Kipi?

Mwili wako huvuta ugiligili kutoka kwa vyanzo tofauti. Kwa hivyo ugiligili ambao mwili wako unahitaji sio lazima utoke kwa maji wakati wote. Vyanzo vingine ni kama vile chai, sharubati, matunda na kadhalika. Tofauti ni kuwa vyanzo hivyo vingine vina upa mwili wako maji na kalori. Kwa hivyo chaguo bora kutoa ugiligili ni maji.

Kawaida, wanawake wajawazito wanashauriwa kuongeza kiwango chao cha chakula. Kwa hivyo kiwango cha maji unacho paswa kunywa kinaweza hesabiwa kupitia kiwango cha chakula unacho kila. Kwa hivyo ikiwa unakula kalori 2000 kwa siku, utahitaji 2000 ml za maji kwa siku. Ikiwa hesabu hizi zinakukanganya, hakikisha kuwa unakunywa angalau glasii 8-10 za maji kila siku. Kiwango hiki kinapaswa kukupa ugiligili zaidi ambao mwili wako unahitaji kufanya kazi inavyo stahili.

maji tosha mwilini ukiwa na mimba

Sababu Za Kukosa Maji Tosha Mwilini

Baadhi ya sababu maarufu zinazo sababisha kukosa maji tosha mwilini ukiwa na mimba.

 • Kuendesha: Kuna mabadiliko ya viwango vyako vya homoni unapokuwa na mimba. Mabadiliko haya yanaweza athiri mwendo wa chakula tumboni na kusababisha kwenda msalani mara nyingi zaidi. Kadri unavyo enda msalani ndivyo mwili wako unapoteza maji. Maji haya yana hitaji kurudishwa mwilini kasi iwezekanavyo.
 • Ugonjwa wa asubuhi: Wanawake wengi hushuhudia ugonjwa huu wanapokuwa na mimba, asilimia 80. Ishara zake huwa kupitisha mkojo mara kwa mara, kutapika, kichefu chefu na kutoa jasho. Ishara zote hizi husababisha mwili kupoteza maji na kufanya mwili ukose kuwa na maji tosha.
 • Hyperemesis Gravidarum: Hii ni hali ya kichefu chefu na kutapika sugu inayo tendeka ukiwa na mimba. Inasababisha mwanamke kutapika siku yote, na kumfanya apoteze uzito wa mwili. Mwili hupoteza maji mengi na kukosa maji tosha hushuhudiwa. Ila, hali hii ni nadra.
 • Joto jingi: Sababu zingine za kukosa maji tosha mwilini ukiwa na mimba ni joto jingi. Kuwa na joto jingi sana kunaweza sababisha kupoteza maji mwilini. Na kusababisha kutapika.
 • Kusafiri kwa hewa: Unapo safiri kwa hewa, ndege huwa na maji hewani. Ili kuepuka kukosa maji mwilini, kunywa maji mengi wakati huo.
 • Hali ya hewa yenye joto: Joto jingi huenda ikakufanya kukosa maji mwilini ukiwa mjamzito. Kukiwa na joto, ni kawaida kutoa jasho jingi. Kadri unavyo toa jasho, ndivyo unavyo kosa maji mwilini.

drink water

Ishara za kukosa maji mwilini ukiwa mjamzito

Wakati wote, mwili wako utaku ashiria unapokosa maji tosha ya kuendeleza utendaji kazi mwilini. Hapa chini kuna baadhi ya ishara ambazo unaweza ona.

 • Kiu ni moja kati ya ishara za kwanza za kukosa maji mwilini ukiwa mjamzito. Unahisi hamu ya kunywa kinywaji fulani. Tatizo ni kuwa watu wengi hupuuza ishara hii. Na kusema watakunywa maji baadaye. Na kwa sababu hii, ishara zingine huanza kuonekana kwa sababu kiu ya maji haiku toshelezwa. Hakikisha kuwa unakunywa glasi ya maji kila lisaa.
 • Unapo pitisha mkojo wa manjano yenye harufu kali na mbaya, hiyo ni ishara wazi ya kukosa maji mwilini. Ni jambo la busara kunywa glasi moja ya maji.
 • Ishara nyingine ni kuumwa na kichwa na huenda ukahisi kizungu zungu, kana kwamba umesimama mahali juu. Jambo hili hufuatia kupunguka kwa shinikizo la damu linalo sababishwa na kukosa maji mwilini.
 • Viungo vya mwili kama mdomo, mapua, ngozi hukauka. Hizi zote ni ishara za kukosa maji. Pia, midomo yako huenda ika kauka.
 • Uchovu ni ishara nyingine ya kukosa maji mwilini.

What Are The Causes Of Hiccups

Matatizo Ya Kukosa Maji Mwilini Ukiwa Na Mimba

Ukiendelea kukosa maji mwilini ukiwa mjamzito, una hatarisha yafuatayo:

 • Maambukizi ya mfumo wa kukojoa: Una pitisha ugiligili ama maji maji mengi unavyo enda msalani. Na unavyo fanya hivi, viini vinatoka kwa mfumo wako. Ukiwa na maji maji kidogo mwilini, hauendi msalani mara kwa mara. Na viini vichache vinatoka mwilini mwako. Na huenda ukapata maambukizi ya mfumo wako wa kukojoa. Usikawie kunywa maji.
 • Maumivu ya kichwa: Maumivu ya aina hii huenda yaka dumu hadi masaa matatu. Cha kuhuzunisha zaidi ni kuwa hauwezi kunywa dawa kuyaponya kwa sababu ya ujauzito. Kwa hivyo, epuka kwa kunywa maji mengi uwezavyo.
 • Joto jingi kupindukia: Una hatari ya kuwa na joto jingi mwilini usipo kunywa maji tosha. Mara nyingi katika mimba, una uzito zaidi na mwili unatatizika kutoa joto zaidi. Punguzia mwili wako kazi kwa kunywa maji tosha.
 • Matatizo ya kujifungua: Amniotic fluid inamzunguka mtoto wako anaye kua. Pia, ina majukumu mengine muhimu kama vile kudhibiti joto na kumlinda mtoto. Majimaji haya yana sawasishwa na maji ambayo mama anatoa. Kwa kuto kunywa maji tosha, mama ana hatarisha kuathiri ugili gili huu, na huenda uka sababisha matatizo wakati wa ujauzito.
 • Kujifungua kabla ya wakati: Kujifungua kusiko komaa unapo jifungua mtoto wako kabla ya wakati unao faa. Hili ni jambo mbaya. Na mojawapo ya vitu ambavyo vinaweza sababisha ni kukosa maji mwilini. Huenda ukashuhudia kuongezeka kwa kiwango chako cha damu na kukufanya uwe na uchungu wa mama wa mapema.

Ikiwa kukosa maji mwilini mahututi ama zito, hali hii inaweza rekebishiwa nyumbani. Lakini ikiwa una shuhudia ishara sugu, hakikisha umemwona daktari bila kukawia. Daktari huenda akashauri intravenous therapy. Itakusaidia kupata maji na virutubisho ambavyo ulipoteza.

Chanzo: Medical News

Soma Pia: Je, Ni Salama Kunywa Maji Moto Ukiwa Na Mimba?

Written by

Risper Nyakio