Majina 50 Ya Kipekee Ya Watoto Wa Kike Ulimwenguni

Majina 50 Ya Kipekee Ya Watoto Wa Kike Ulimwenguni

Unamtafutia mtoto wako wa kike unayemtarajia jina? Tuko hapa kukusaidia!

Unatafuta jina la kipekee la mtoto wa kike duniani kando na orodha ya majina bora kutoka Amerika. Kuna majina mengi mazuri ya watoto wa kike kutoka duniani kote. Kwa mfano: Aurora(Norwei), Mei (japani), Lesedi (Afrika Kusini), Catalina (Ajentina), na Sienna(Australia). Muundo na sauti ya haya majina huyafanya kuwa ya kipekee kati ya majina mengi tunayosikia kila walkati. Bado mvuto wao wa duniani kote huyafanya kutoshelezea hapa nyumbani Amerika ambako tabaka lake limeundwa na tamaduni tofauti. Tazama majina 50 ya kipekee ya watoto wa kike ulimwenguni.

Kuna sababu nyingi za kuchagua jina la mtoto wa kike ambalo lina uzoefu katika sehemu nyingine ya dunia.

“Wazazi wengine hutaka kuheshimu sehemu ya uzao wao – tunaona hilo katika familia zenye urithi tofauti,  haswa kama mtoto atapokea jina moja kutoka kwa mila moja  na wanataka kuheshimu mila hiyo  nyingine kwa jina la kwanza,” akasema Laura Wattenberg wa Baby Name Wizard. “Ama wanataka tu kujivunia mila yao.”

Lakini Wattenberg bado anasema watu sio lazima wawe na urithi kutoka nchi fulani ili kutumia jina lililo na uzoefu huko.

“Hili ni jina linaloyeyusha chungu katika mila,” anaelezea. Kwa mfano, hatupatani na Sean na tunafikiria kuwa anatoka Ayalandi. Majina yaliyo na uzoefu katika nchi zingine huwapa wazazi mawazo mapya ambayo bado yana mizizi nyuma yake.”

Kwa hivyo, wazazi katika mataifa mengine wanawapa watoto majina yepi? Bahati kwetu, Wattenberg na kundi lake huchunguza yanayoendelea katika nchi tofauti.  Tulipitia orodha zao kutafuta majina hamsini, ambayo ni makali katika sehemu zingine za dunia na yanaweza kutoshelezea vizuri watoto wa kike kutoka Amerika.

Chunguza haya majina hamsini ya watoto wa kike katika hii orodha  – tulijaribu kujumuisha kitu kwa kila mtu kutoka mataifa tofauti. Wattenberg anaelezea  kuwa sio kila nchi huifanya orodha yake ya majina kuwa wazi kwa umma, kwa hivyo sio kila sehemu imewakilishwa hapa. (lakini pia, tumegusia kila bara.)

Ni matumaini yetu kuwa orodha hii ya  majina 50 ya kipekee ya watoto wa kike ulimwenguni itawasaidia wazazi wanaotarajia kupata jina mwafaka la mwana wao atakayetalii dunia.

Camille

Majina 50 Ya Kipekee Ya Watoto Wa Kike Ulimwenguni

Picha Shurani kwa: CafeMom

Toleo la Camilla, Camille linasikika kuwa la kimtindo sana. (Ama tunafaa kusema tres chic?). Linamaanisha “nakawa” ama “asiye na kasoro.” Huwa ni chaguo la uzoefu  huko Quebec na katika nchi zingine zilizo na watu wanaozungumza Kifaransa zikiwemo  Ubelgiji, Uswisi na (bila shaka) Ufaransa.

Farah

Majina 50 Ya Kipekee Ya Watoto Wa Kike Ulimwenguni

Picha shukrani kwa: CafeMom

Humaanisha “furaha” katika Kiarabu, Farah ni jina mwafaka kwa mtoto wenye furaha, na hivi sasa liko katika nambari ya #12 ya majina ya wasichana wa kike Yordani.

Aurora

Majina 50 Ya Kipekee Ya Watoto Wa Kike Ulimwenguni

Picha shukrani kwa: CafeMom

Linamaanisha “macheo” katika Kilatini jina Aurora linatufanya kuwaza juu ya urembo wa aurora borealis. Hili jina la mbinguni lina uzoefu Norwei na katika mataifa mengi ya ulaya.

Mei

Majina 50 Ya Kipekee Ya Watoto Wa Kike Ulimwenguni

Picha shukrani kwa: CafeMom

Jina Mei ni ndogo na litamu kweli. Huwa katika safu ya majina kumi ya kipekee  ya watoto  huko Japani ambako humaanisha “uchipuko” ama “ota”. Katika uchina hili jina humaanisha “mrembo.”

Tess

Majina 50 Ya Kipekee Ya Watoto Wa Kike Ulimwenguni

Picha shukrani kwa: CafeMom

Jina Tess lilijulikana toka jadi kama msimbo wa Theresa – likimaanisha “mvuni” – lakini lilipata umaarufu  na sasa linapewa wasichana wadogo kama jina la kwanza kamili. Hili jina lina hadhi kuu Uholanzi.

Lesedi

most unique girl names in the world

Picha shukrani kwa: CafeMom

Hili jina ni la #8 kwa majina ya watoto wa kike Afrika Kusini. Lesedi humaanisha “mwanga” katika Tswana.

Amaia

most unique girl names in the world

Picha shukrani kwa: CafeMom

Jina la mbadala kwa Maya, Amaia humaanisha “mwisho” katika  Basque na lina umaaarufu  Puerto Rico.

Freya

Majina 50 Ya Kipekee Ya Watoto Wa Kike Ulimwenguni

Picha shukrani kwa: CafeMom

Freya alikuwa mungu wa kike wa uzazi katika Norse mythology. Hili jina kwa sasa ni #14 kwa wasichana nchini Welisi na lina umaarufu  Uingereza kote.

Catalina

Majina 50 Ya Kipekee Ya Watoto Wa Kike Ulimwenguni

Picha shukrani kwa: CafeMom

Catalina ni toleo la kihispania linalomaanisha “safi” ama “lisilo na kasoro.” Lina umaarufu Ajentina  na Chile.

Aoife

most unique girl names in the world

Picha shukrani kwa: CafeMom

Majiana ya Mwayalandi yanaweza kuwa magumu kwa wamerika kutamka lakini hili jina  – linalotamkwa EE – fa – waambie, “ ni kama Eva na F.” Linamaanisha “urembo” katika Gaelic  na lilikuwa moniker wa malkia shujaa. Linasikika kama chaguo la kufana sana kwetu!

Nina

Kwa hivi sasa jina la #2 kwa umaarufu la wasichana Slovakia, Nina ni jina la msimbo la Urusi  la Anne na Antonia. Pia linatumika katika lugha zingine.

Aisha

Majina 50 Ya Kipekee Ya Watoto Wa Kike Ulimwenguni

Picha shukrani kwa: CafeMom

Linalomaanisha “kuwa hai” katika kiarabu, Aisha ni jina moja la watoto wa kike lenye umaarufu Kazakhstan.

Tamar

most unique girl names in the world

Picha shukrani kwa: CafeMom

Tamar kwa hivi sasa ni jina la #1 la watoto wa kike Israeli. Ni jina la kiyahudi linalomaanisha “mtende.”

Isidora

most unique girl names in the world

Isidora linakaa jina mwafaka kwa wazazi wanaopendezwa na jina Isabel lakini wanatafuta jina lisilo na uzoefu Amerika. Hili jina ni maarufu Chile na ni mchanganyiko wa jina la mungu wa kike wa uzazi (Isis) na jina la uigiriki linalomaanisha “zawadi.”

Ramona

most unique girl names in the world

Picha shukrani kwa: CafeMom

Ramona ni tolea la kike la Ramone linalomaanisha “utunzi wa hekima.” Ni jina linalokuwa la kwanza kwenye safu ya  majina ya watoto wa kike Paraguay.

Sienna

most unique girl names in the world

Picha shukrani kwa: CafeMom

Sienna ni rangi ya hudhurungi, machungwa nyekundu na ni aina ya udongo  wa rangi sawia. Ni jina la umaarufu kwa watoto wa kike katika maeneo tofauti Australia.

Tui

most unique girl names in the world

Tui (linalotamkwa Twee) ni jina la kufana la mtoto wa kike New Zealand. Linatokana na jina Maori aina ya ndege.

Zahra

most unique girl names in the world

Picha shukrani kwa: CafeMom

Linalomaanisha “busara” ama “mwerevu,” Zahra kwa hivi sasa ni #1 katika majina ya wasichana Azerbaijan.

Seo-Yeon

most unique girl names in the world

Wazazi ambao huwapa watoto wao jina Seo-Yeon huwaza kuwa mema yamekuja kwao. Seo humaanisha “bahati nzuri” ama “ujao wa mema,” na Yeon humaanisha “rembo” ama “yenye neema.” Katika Korea jina hukaribia Seo-Yun  – Yun ikimaanisha “laini” na “nyororo.”

Astrid

most unique girl names in the world

Picha shukrani kwa: CafeMom

Jina lenye uzoefu la watoto wa kike Uswidi na Denmaki. Astrid ni jina la mchanganyiko likimaanisha “mungu” na “maridadi.”

Venla

most unique girl names in the world

Venla sio jina tunalosikia kila siku lakini linaonekana kuwa linalojulikana na rahisi kutamka.  Ni jina la kike la Wendel linalomaanisha Vandal jina la ukoo wa kijerumani wa kale ya tano. Hili jina ni la umaarufu kwa watoto wa kike Ufini.

Yuna

Majina 50 Ya Kipekee Ya Watoto Wa Kike Ulimwenguni

Yuna ni jina maridadi na rahisi kutamka . Ni jina #3 kwa watoto wa kike japani na wakati mwingine hutumika na lugha zingine pia kama vile Chinese, Brazilian Portuguese na Korean.

Valentina

most unique girl names in the world

Jina la kimahaba! Nani hafikirii juu ya siku ya valentine wanaposkia Valentina? Hili jina ni #2 kwa watoto wa kike wanaozaliwa Mexico na lina umaarufu katika nchi  zingine zinazongumza uhispania.

Ines

most unique girl names in the world

Picha shukrani kwa: CafeMom

Ines ni tolea la kifaransa la Ines ama Agnes na kwa hivi sasa ni katika majina kumi ya watoto wa kike Ufaransa. Hili jina lenye utata ni chaguo mwafaka kwa wazazi wanapenda sauti ya majina ya kifaransa lakini hawataki yaliyo na uzoefu Amerika (kama vile Chloe,Eva, Sofia,etc)

Defne

Majina 50 Ya Kipekee Ya Watoto Wa Kike Ulimwenguni

 

Defne lina umaarufu Uturuki, ambako ni tolea la Daphne linalomaanisha jani la loreli ama “laurel.”

Luciana

most unique girl names in the world

Picha shukrani kwa: CafeMom

Hili ni jina la #2 kwa watoto wa kike Colombia. Luciana pia hutumika katika kiitaliano, kireno na nchi zingine zinazozungumza kihispania.

Julieta

Majina 50 Ya Kipekee Ya Watoto Wa Kike Ulimwenguni

 

Huwa chaguo la umaarufu kwa watoto wa kike Uruguay, Julieta hii mfano mwingine wa Julie ama Juliet ambazo hutufanya sote kufukiria juu ya mchezo wa kuigiza wa Shakespeare wa mahaba na huzuni.

Noemi

most unique girl names in the world

Picha shukrani kwa: CafeMom

Tolea la uhispania la Naomi ambalo kwa kiyahudi ni “furaha yangu” hili jina maridadi lina umaarufu Italia na mataifa mengine ya Ulaya na kusini mwa Amerika.

Tia

Majina 50 Ya Kipekee Ya Watoto Wa Kike Ulimwenguni

Tia wakati mwingine  ni ufupisho wa Letitia linalomaanisha “furaha” lakini linatumika kataika lugha nyingi tofauti na lina maana nyingi. Hutumika kwa mara nyingi New Zealenad ambako Tia alikuwa  mvumbuzi wa jadi na chifu.

Mariana

most unique girl names in the world

Picha shukrani kwa: CafeMom

Mariana hutumika kwa wakati mwingine kama mchanganyiko wa Maria na Ana lakini lilitokana na Marianaus linalomaanisha “Mars” – aka mungu wa kirumi wa vita. Ni jina lenye umaarufu Ureno.

Daniela

most unique girl names in the world

Picha shukrani kwa: CafeMom

Daniela hutokana na Daniel linalomaanisha “Mungu ni hakimu wangu.” Liko kwenye safu ya majina kumi bora ya majina ya watoto wa kike Uhispania.

Matilda

most unique girl names in the world

Picha shukrani kwa: CafeMom

Matilda ni jina lenye umaarufu katika maeneo tofauti ya Australia na Tasmania na utapata Matildas katika nchi nyingi duniani kote. Hili jina la nguvu kutoka Ujerumani huumanisha “shupavu kwenye vita.”

Marija

Majina 50 Ya Kipekee Ya Watoto Wa Kike Ulimwenguni

Picha shukrani kwa: CafeMom

J haitamkwi katika toleo la Slovene la Maria/Mary. Ni jina la #1 Bulgaria na mara nyingi hutumika Croatia pia.

Luisa

Majina 50 Ya Kipekee Ya Watoto Wa Kike Ulimwenguni

Picha shukrani kwa: CafeMom

Luisa hutokana na jina Louis linalomaanisha “aliyetambulika vitani.” Watoto wa kike wanaoitwa Luisa wanaweza kupatikana Ujerumani na nchi nyingine za ulaya.

Ana

most unique girl names in the world

Picha shukrani kwa: CafeMom

Ana ni jina maridadi linalomaanisha “ennye neema” ama “mkarimu.” Namabri moja kwa majina ya wasichana Austria hili jina pia lina umaarufu uhispania , ureno, Uswizi, Serbia na mataifa mengine.

Nora

most unique girl names in the world

Picha shukrani kwa: CafeMom

Nora kwa wakati mwingine huwa ufupisho wa Honora (kumaanisha “hekima”) ama Eleanor (kumaanisha “mwanga”). Hutumika katika lugha zikiwemo uholanzi, uingereza, Ujerumani, kiairish, kiitaliano, kinorwei na kiswidi. Noara kw ahivi sasa inaongoza safu ya majian ya watoto wa kike HUngray na mataif mengine ya ulaya.

Sóley

most unique girl names in the world

 

Tnalipenda hili jian maridadi la Icelandic Soley ambalo ni jina la kombetindi, ua ya mwituni la manjano.

Isla

most unique girl names in the world

Picha shukrani kwa: CafeMom                                                                                                                                                                            

Isla hutokana na jina la kisiwa uskoti: huja katika #4 kwa majina ya watoto usskoti na uingereza.

Yasmine

most unique girl names in the world

Picha shukrani kwa: CafeMom

Yasmine hutokana na jina la kiarabu la mti unukiao vizuri wa jasmine. Yasmines wanaweza kupatikana ubelgiji, ufaranasa na Quebec.

Adele

most unique girl names in the world

Picha shukrani kwa: CafeMom

Adele lilitokana na  ufupisho wa Adelaide linalomaanisha “utajiri.” Liko kwenye orodha ya majina kumi bora ya watoto wa kike Ufaransa.

Liliana

most unique girl names in the world

Picha shukrani kwa: CafeMom

Kulingana na Baby Name Wizard, Liliana humaanisha “lily,” ambalo ni msimbo mzuri wa hili jina. Lin aumaarufu Poland na pia kuna Lilianas wanaopatikana Hungary na Portugal.

Mila

most unique girl names in the world

Picha shukrani kwa: CafeMom

Kati ya majina ya watoto ya kike yaliyomaarufu Uswizi ni Mila linalomaanisha “rafiki mwenye neema.” Ni jina maarufu katika nchi zingine pia.

Tereza

most unique girl names in the world

Picha shukrani kwa: CafeMom

Jina la pili katika Czech republic , Tereza huja na Z ambayo ni tofauti na Theresa linalomaanisha “mvuni.”

Alise

Majina 50 Ya Kipekee Ya Watoto Wa Kike Ulimwenguni

Picha shukrani kwa: CafeMom

Alise  linamaanisha Alice katika Latvia ambako ni jina la #3 kwa umaarufu.

Bianca Maria

most unique girl names in the world

Picha shukrani kwa: CafeMom

Bianca humaanisha “nyeupe,” na Maria humaanisha “Mary.” Yote mawili huunda hili jina ambalo ni la kawaida kwa watoto wa kike Romania.

Polina

most unique girl names in the world

Picha shukrani kwa: CafeMom

Iwapo Polina linaonekana kama jina la uchache labada ni kwa sababu ni tolea la kike la Paul linalomaanisha “mdogo.” Polina ni jina la #3 Belarus.

Katarina

most unique girl names in the world

Picha shukrani kwa: CafeMom

Katarina ni jina la kwanza la wasichana Serbia (na pia linajulikana vizuri Amerika). Ni aina nyingine ya Katherine linalomaanisha “swafi”  ama “bila ila.”

Linnea

most unique girl names in the world

Picha shukrani kwa: CafeMom

Linnea ni mojawapo ya majina yenye umaarufu Uswidi.  Ni jina la ua ambalo mswidi karl Von LInne alijiita baada yake.

Aylin

Majina 50 Ya Kipekee Ya Watoto Wa Kike Ulimwenguni

Picha shukrani kwa: CafeMom

Aylin (linalotamkwa kama Eileen) linamaanisha “kutoka kwa mwezi” na ni maarufu Uturuki na Azerbaijan.

Anastasia

Majina 50 Ya Kipekee Ya Watoto Wa Kike Ulimwenguni

Picha shukrani kwa: CafeMom

Anastasia humaanisha “wa kufufuka” na ni maarufu katika wakristo . Kwa hivi sasa huongoza safu ya majina ya watoto wa kike Urusi, Ukraine na Georgia.

Ni matumaini yetu kuwa orodha hii ya majina 50 ya kipekee ya watoto wa kike ulimwenguni imewasaidia.

Soma pia: The most unique names with Biblical meanings for girls

Makala haya yalichapishwa kwa mara ya kwanza CafeMom na kuchapishwa tena theAsianparent na idhini yao.

Written by

Risper Nyakio