Majina Maarufu Zaidi Ya Watoto Wa Kiume Kenya 2020

Majina Maarufu Zaidi Ya Watoto Wa Kiume Kenya 2020

Makala haya yana rahisisha wakati wako wa kuchagua jina la mtoto wako wa kiume. Chagua mojawapo ya majina haya!

Safari ya mimba ni mojawapo ya vitu vya kupendeza zaidi katika maisha ya wanandoa. Ingawa ina changamoto zake kama vile kichefuchefu na ugonjwa wa asubuhi hata kufura kwa miguu kwa baadhi ya wanawake. Safari hii ni huwa yenye mapenzi na furaha zaidi kwa wanawake. Kuchagua jina la mtoto huwa mojawapo ya mambo magumu katika safari hii. Punde tu unapo fanya scan ya kutambua jinsia ya mtoto, unapaswa kuanza kufanya utafiti wa majina ambayo ungependa kumpea. Iwapo una tarajia mtoto wa kiume, tuna orodhesha majina mazuri ya watoto wa kiume 2020 bora zaidi.

Majina hubeba maana kubwa katika maisha ya mtoto, hii ndiyo sababu kwa nini wazazi huwa makini sana katika majina wanayo waita watoto wao. Tazama baadhi ya majina ya kipekee ambayo unaweza mwita mtoto wako wa kijana unaye jifungua mwaka huu.

Majina Maarufu Zaidi Ya Watoto Wa Kiume Kenya 2020

Majina mazuri ya Swahili ya watoto wa kiume Kenya

Wakati mwingi, wazazi hupendelea kuwaita watoto wao majina ya Swahili kwani ni ya kipekee na sio maarufu sana. Pia, majina ya Kiswahili yana uzito katika maisha ya mtoto na kusaidia katika kuyapa maisha ya mtoto shepu.

Abasi. Mtu mkali, mtoto wa kiume mwenye nguvu.

Abdala. Lina maana ya mtumishi wa Mungu.

Azaan. Anaye ibuka kama mtu mwenye nguvu.

Ashura. Rafiki anaye andamana nawe.

Bahati. Mtoto wa mfalme.

Daudi. Anaye pendwa.

Jabali. Jina hili la kupendeza lina maana ya kuwa na nguvu kama jiwe.

Barasa. Lina maana ya kukutana ama mkutano.

Tajiri. Watoto wenye jina hili huleta utajiri kwa familia kwani ni jina la mtu mwenye tabaka la juu.

Fadhili. Mkarimu, mwenye mapenzi.

Mhina. Jina hili lina maana ya anaye furahi na mwenye kuheshimika.

Shomari. Hili ni jina bora la mtoto ambaye alikutatiza kujifungua. Iwapo alikusumbua na kurusha mateke sana, huenda ikawa kuwa baada ya kuzaliwa, atakuwa mtoto mwenye fujo. Kumpa jina hili huenda kukamsukuma kwa njia nzuri na kumhamasisha kufanya mema maishani.

Majina Maarufu Zaidi Ya Watoto Wa Kiume Kenya 2020

Majina ya KiAfrika

Gitonga. Mwanamme tajiri ama anaye leta utajiri kwenye nyumba.

Gacoki. Anaye rudi.

Gakuru. Aliye zeeka ama mwenye umri zaidi.

Chitundu. Nyumba ya ndege.

Muthii. Anaye penda kutembea ama aliye zaliwa wakati ambapo wazazi walikuwa matembezini.

Amara. Mwenye maisha yasiyo isha, kubarikiwa na bila mwisho.

Alhaadi. Anaye ongoza.

Chiumbo. Yule mdogo.

Ohon. Aliye hifadhiwa.

Odongo. Wa pili kati ya mapacha.

Omwancha. Anaye wapenda watu.

Odikinyi. Aliye zaliwa asubuhi mapema.

Wambua. Aliye zaliwa wakati wa mvua.

Majina Maarufu Zaidi Ya Watoto Wa Kiume Kenya 2020

Majina mengine ya kizungu

Asher. Lina maana ya kubarikiwa, kuwa na bahati na furaha.

Henry. Anaye ongoza nchi.

Declan. Mwanamme anaye omba na aliye na wingi wa uzuri na mema.

Jasper. Anaye leta urithi mwingi.

Silas. Anaye ishi kwenye msitu.

Jack. Anaye amini mema ya Mungu.

Theodre. Zawadi kutoka kwa Mungu.

Junior. Mdogo wake.

Kumbukumbu: webmd, Tuko

Soma pia: Orodha Ya Majina Yanayo Maanisha Dua Njema

Written by

Risper Nyakio