Mara nyingi tunapozungumzia bibilia, jambo la kwanza linalotujia akilini ni wanaume waliomtumikia Mungu. Ukweli ni kuwa, kuna mabinti wengi wanaotajwa katika bibilia waliomtumikia Mungu pia. Iwapo ungependa binti yako awe na jina la kibibilia, upo mahali panapofaa.
Kuna imani kuwa mtoto huiga sifa za jina lake. Kwa sababu hii, ni muhimu kwa wazazi kufahamu maana ya jina la mtoto kabla ya kuchagua kumpa jina hilo.
Orodha yetu ya majina ya wasichana ya bibilia na maana itakusaidia kuchagua jina bora kwa mwanao.
Majina ya Wasichana ya Bibilia na Maana

Abigail. Lina maana ya furaha ya babake. Mwenye maarifa na urembo.
Abihail. Jina linalotumika kwa jinsia zote mbili. Baba wa nguvu.
Adah. Mkusanyiko. Kwenye bibilia alikuwa bibi yake Lamech.
Anna. Jina lenye maana ya neema.
Ariel. Simba wa Yudah.
Bernice. Anayeleta amani
Bethel. Nyumba ya Mungu
Damaris. Mwanamke mchanga
Daniela. Mungu mhakimu wangu
Diana. Asiye na doa
Edna. Furaha
Elisheba. Mungu ni wingi
Elizabeth. Kiapo cha Mungu
Esther. Msichana mrembo
Eva. Maisha
Eunice. Ushindani mzuri
Gabriella/ Gabrielle. Mungu ni nguvu zangu
Hannah. Neema na upendeleo
Hope. Kuwa na matumaini
Jezebel. Asiye na doa
Joanna. Mungu ni wa neema
Jochebed. Anayeheshimika ama ukuu wa Mungu
Joy. Furaha
Junia. Malkia wa binguni
Keturah. Harufu nzuri ya kunukia
Lilian. Urembo usio na doa
Michelle. Aliye kama Mungu
Myra. Kulia ama kumwaga
Naomi. Mrembo, ama anayekubalika naye

Paula. Ndogo, jina la kike la Paul
Phoebe. Kung'aa
Priscilla. Ya zamani ama ya kale
Ruth. Kutosheka. Kwenye bibilia anafahamika kwa ukarimu wake
Salome. Amani
Serah/ Sarai/Sarah. Binti ya mfalme wa wingi
Selah. Jiwe
Serah. Binti ya mfalme
Sherah. Mwangaza
Shifra. Anayependeza
Shiloh. Mwenye amani ama zawadi yake
Tabitha. Mwenye jicho linaloona sawa
Talitha. Msichana mchanga
Terah. Ardhi ama dunia
Zemira. Anayesifiwa
Zillah. Kivuli
Zina. Mgeni
Zipporah. Urembo ama ndege
Soma Pia: Majina ya Watoto wa Kiume ya Kiingereza 2022 Yanayotamba