Kupatia mtoto jina kunahitaji utafiti mwingi na utulivu. Hii ni kwa sababu hasa wana Nigeria wana tamaduni hasa za kuwapatia watoto majina. Hata kama tamaduni za kuwapatia watoto majina hutofautiana na kabila, kuna jambo moja maarufu. Wana Nigeria wote wana penda majina yanaayo eleza, hasa majina yaliyo wazi na yana maana kamili. Majina haya ya watoto wa kike Nigeria wanapendwa zaidi.
Tamaduni za kuwapatia watoto majina yali badilika na kuanziwa kwa Uislamu na Ukristo. Baadhi ya familia zilianza kuchagua majina ya kikristo ama kiislamu na wengine walibaki kuchagua majina ya kitamaduni. Wazazi mara kwa mara huchagua majina yanayo ashiria hali inayo zingira kuzaliwa kwa mtoto yule na wengine huwapatia watoto wao majina yanayo tabiri maisha ya usoni ya mtoto.
Majina maarufu ya watoto wa kike Nigeria na jinsi majina yana chaguliwa
Majina ya watoto wa kike Nigeria: Mwongozo
Huko Nigeria, kupata mtoto jina ni utabiri. Ni shairi na kuhadithi. Ni gumu.
Hakuna mzazi anaye taka kumtwika mtoto wake mzigo wa jina ambalo litakuja kumharibu. Kwa hivyo majina yana chaguliwa kwa umakini. Kwa kawaida, nyanya atajitolea na baadhi ya majina ya kumwita mtoto. Ni maarufu kuona watoto wakipewa majina hadi matano. Baadhi ya wakati, herufi ya kwanza, majina yote yana tengeneza jina simamizi (acronym) na wakati mwingine, mtoto huyu kutumia jina moja ama mawili kwa vyeti vyake rasmi.
Jina la mtoto hali amuliwi na jinsia yake tu. Lina amuliwa na nafasi yake kwenye familia. Kwa mfano, kwenye tamaduni za Igbo ni wasichana wa kwanza tu wanao itwa Ada.
Katika tamaduni za Yoruba, mapacha wanapatiwa majina kulingana na wanavyo zaliwa kwenye familia. Pacha wa kwanza anaitwa Taiwo (lenye maana ya, ‘aliye onja dunia wa kwanza’). Kehinde huwa jina la pacha wa pili lenye maana ya ‘aliye baki nyuma’.
Njia nyingine ya kuchagua jina kulingana na tarehe ya kuzaliwa
Kwa hivyo mtoto anaye zaliwa siku ya Ijumaa anaitwa Friday. Anaye zaliwa miezi ya Aprili, May na June anaitwa majina ya miezi hiyo na pia majina haya ni maarufu kwa watoto wa kike.
Baadhi ya wakati watoto wanapatiwa majina ya jamaa na marafiki walio karibu na familia. Kupatia mtoto jina kwa njia hii ni njia ya kuimarisha urafiki kati ya familia hizi.
Katika makala haya, tunakupatia orodha ya majina bora ya watoto wa kike Nigeria. Kupata jina linalofaa la mtoto wako haipaswi kuwa vigumu. Orodha yetu ina angazia kabila tatu kuu za Nigeria.
Ila kabla ya kuchapisha orodha yetu, kwanza tuangazie tabaka tatu kuu
Nigeria kuna kabila tatu kuu: Igbo, Hausa na Yoruba. Kila tabaka ina tamaduni za kipekee . Na lugha ambazo ni za kipekee wanazo zitumia.
Orodha yetu ya majina ya watoto wa kike Nigeria:

Majina ya Igbo na maana yake
Adaora- binti wa kwanza
Adaeze- binti wa mfalme
Amaka- mrembo
Adaku- binti wa tajari
Amarachi- Neema ya Mungu
Chioma- Mungu mwema
Chinyere- Neema za Mungu
Ifeoma- nzuri
Nneka- mama mzuri
Ngozi- baraka
Nkechi- wa Mungu
Nkiruka- kuna matumaini
Oluebube- miujiza
Obianuju- wingi
Ozioma- habari
Majina ya Yoruba na maana
Abebi- tuliomba mtoto wa kike
Adekemi- taji lina ni tunza
Adesewa- taji lina pendeza
Atinuke- yule aliye tunzwa kutoka alipo tungwa
Ayoola- furaha ya utajiri
Ayotola- furaha ni utajiri tosha
Ayotoluwafunmi- furaha ambayo Mungu amenipa
Bisi- binti wa kwanza wa familia
Bimpe- mrembo na wa kupendeza
Bosede- binti aliye zaliwa siku ya Jumapili
Foluwakemi- Mungu huwa utunzi wangu
Feyikemi- tabasamu zita ni zingira
Morenikeji- nimepata mwingine kama mimi
Mololuwa- nina Mungu
Oyinkansola- asali inamwagika kwenye utajiri
Omotola- watoto wana thamani ya utajiri
Olayiwunmi- napenda hali hii ya anga
Majina maarufu ya watoto wa kike Nigeria ya ki Hausa na maana yake
Bakuma- mgeni
Fara- mwenye sura laini
Gimbiya- binti wa mfalme
Hakuri- utulivu
Kuluwa- anaye pendwa zaidi
Kyauta- zawadi ya Mungu
Kyawo- msichana mrembo
Sarauniya- malkia
Tanoma- aliye zaliwa msimu wa kulima
Baadhi ya wana Hausas pia wanapenda majina ya Arabic, baadhi yao ni:
Aisha- kuishi, mafanikio
Aminah- salama, ulinzi
Habibah- anaye pendwa
Halimah- mtulivu
Kubra- mkuu
Latifah- mtulivu, mkunjufu, aliye badilika
Lubabah- haja ya ndani kabisa
Maimuna- aliye barikiwa ama mwenye bahati
Rabi’ah- wanne
Halimah- salama, afya
Zahrah- ua, kuvutia,
Zaytun- olive
Zubaydah- krimu ya mmea, kung’aa
Tazama orodha yetu ya majina ya watoto wa kike ya kuchagua jina linalo pendeza na lenye nguvu la binti yako.
Bila shaka kuna zaidi ya kabila 400 Nigeria. Kabila zisizo na watu wengi zina tofauti katika tamaduni zake za kuchagua majina ya watoto. Kwa mara nyingi, watu wa kabila ndogo huwa na zaidi ya lugha mbili ama hata tatu. Watu wa kabila tofauti huongea kwa urahisi.
Hapa chini kuna orodha ya majina ya watoto wa kike ya kabila ndogo nchini.
Wa Tiv
Iverem- baraka
Yahimba- hakuna kitu sawa na nyumbani
Morihinze- mtoto wa jinsia yoyote ni sawa
Hembadoon- mshindi
Limber- furaha
Wa Ijaw
Abinla- mtoto wa kike wa mfalme
Abiye- hamu yangu
Agake- ere- mwanamke mwema ni bibi mzuri
Alaere- malkia
Alayingi- mama wa kifalme
Wa Ibibios
Ekaete- mama ya baba
Uyai- urembo
Obongoawan- malkia
Ediye- mrembo
Affiong- mwezi
Wa Idomas
Akum- yangu
Anyaole- wanawake wanatengeneza nyumbani
Ebo- amani
Ogodo- mama ya wamama wote
Onyabahi- mwanamke anaye penda utajiri
Wa Urhobo
Isio- nyota
Omote- msichana
Erhuvwun- urembo
Enajemete- pia kuna wasichana
Wa Igala
Iye-mama
Ejura- wakati wa uwingi
Futumi- kushangazwa
Alami- msichana aliyezaliwa Alhamisi
Wa Itsekiri
Alero- msichana kifungua mimba
Besida- takdiri inavyotaka
Dolor- pesa
Ebeji- mapacha
Orighomisa- kichwa changu ni kizuri
Majina ya Bini/Edo yaliyo maarufu ya watoto wa kike wa Nigeria
Adesewa- ustawi, mafanikio, katikati ya utajiri
Akugbe- upamoja
Eseosa- zawadi ya Mungu
Esohe- zawadi ya bure
Ifueko- mpole
Itohan- huruma
Osasere- Mungu ni mkuu
Mwishowe, ni uamuzi wa mzazi. Wanaweza amua iwapo wangetaka kufuata utamaduni ama kuchagua jina jipya. Siku hizi, baadhi ya wazazi wana waita watoto wao baada ya watu mashuhuri wanao julikana kuburudisha watu kama vile Beyonce, Kim Kardashian ama Rihanna. Baadhi ya wengine wanageukia tasnia ya michezo ili kupata majina. Pia, wanaopenda kadanda wanawaita watoto wao majina ya wachezaji wanao wapenda.
Tusisahau kuwa baadhi ya majina haya yanaweza tumika na jinsia yoyote. Watu hutazama majina haya kama ya utamaduni ya wasichana ama wavulana.
Jambo moja halija badilika lakini. Familia za Nigeria na tabaka zina amini sana katika nguvu za jina. Ni muhimu kuchagua kwa umakini. Jina la mtoto linaweza kuwa ombi, takwa ama msukumo. Una amua kinacho jalisha zaidi kwako.
Kadri iwezekanavyo, mpe binti yako jina la kipekee linalo pendeza na linalo sherehekea tabaka na tamaduni zako. Jina la mwanao huenda likaanza mazungumzo.
Pulse NG
Soma pia: What your baby’s time of birth says about their personality
Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.