Orodha Ya Majina Maalum Ya Watoto Wa Kiume Nigeria

Orodha Ya Majina Maalum Ya Watoto Wa Kiume Nigeria

Ni lipi unataka zaidi kwenye orodha hii?

Sherehe za kuwapa watoto majina ni mojawapo ya matukio yanayo sifika sana Nigeria. Na kufanya uamuzi wa majina ya kike ama kiume ya Nigeria ni muhimu sana kwenye utamaduni wa Nigeria. Familia na jamaa na watu wa karibu wanakusanyika kusherehekea mwana familia aliye jiunga na familia. Pia, saizi ya sherehe ina tegemea na utajiri wa wazazi wapya; huku sherehe ikifika kilele mtoto anapo pata jina lake. Katika makala haya, tuna angazia baadhi ya majina ya watoto wa kiume Nigeria ya kubariki mtoto wako nayo.

Faida za majina mashuhuri ya watoto wa kiume Nigeria

majina ya watoto wa kiume Nigeria

Majina ni utabiri

Hali mbaya ya kiuchumi ya hivi majuzi ime wapatia wazazi msukumo wa kutabiri matumaini na ndoto kwenye watoto wao. Majina ya kitabiri na wazazi Nigeria wanawaita watoto wao wanayo yatarajia zaidi. Utapata kuwa majina maarufu kama Victory, Wealth, Riches na Favour yako kwa wingi.

Kuna vitu vingi vinavyo amua chaguo la majina Nigeria. Baadhi ya sababu hizi ni matukio yanayo tendeka kabla ama baada ya kuzaliwa; uhusiano wa kidini wa wazazi wapya; watu mashuhuri ambao wazazi wanapenda na nafasi ambayo mtoto amezaliwa kwenye familia.

majina ya watoto wa kiume Nigeria

Majina yana sema uhusika wa kidini

Ina julikana kwa umaarufu kuwa wana Nigeria ni watu wakunjufu na hamu hii huonekana hata kwa mienendo yao ya kimaisha, dini ama vitu wanazo penda. Majina maarufu ya kikristo ni kama vile God’s-Glory, God-is-Good na kadhalika. Majina haya yana dhihirisha wenye majina haya kama wakristo kamili. Baadhi ya wazazi huenda hata wakawaita watoto wao baada ya watu maarufu wa Mungu. Kwa mfano, kwenye kanisa ambako mchungaji mkuu ni David; sio jambo gumu kuwa na watoto wengi wa wafuasi wa kanisa hilo kuwaita watoto wao David. Jina hili ni maarufu sana Nigeria.

Hupaswi kuwa na shaka unapo pata majina kama Open Heavens, Yelutide, Alleluyah, Godspower, MightyGod, Breakthrough, Hand of God. Haya ni majina ya kumsifu Mungu.

Baadhi ya wakati, majina haya maarufu ya watoto wa kiume Nigeria yana heshimu serikali inayo tawala.

Katika mwaka wa 2011, rais wa hapo awali Goodluck Jonathan alishinda uchaguzi na kuwa jina maarufu kwenye nyumba za wana Nigeria wengi. Sababu haikuwa ya mbali, kwani wazazi wengi wapya waliomba ‘bahati nzuri’ kwenye maisha ya watoto wao. Bahati yake nzuri ilimdhibitisha kama kitambulisho cha kijana anaye kua kutoka maisha ya chini hadi ya juu. Goodluck Jonathan alizaliwa katika familia masikini na hata hawangeweza kumnunulia viatu vya shule. Alitembea miguu mitupu kwenda shuleni kila siku. Kwa njia fulani, kila mtu aliamini kuwa jina lake lilisaidia katika bahati yake njema.

Raisi mstaafu Kinsmen katika Bayela alipata umaarufu kufuatia majina yake ya kipekee kama Generali, Inspekta, Colonel, Heineken, Jubilee, Difference, ThankGod, Worldwide, Government, Confidence na kadhalika.

Majina yana sifu watu mashuhuri

Kadanda kama mchezo ni kitu kinacho waleta wana Nigeria wengi pamoja. Watu kutoka tabaka tofauti na darasa za kijamii wanapenda kuungana kuonyesha mapenzi yao ya mchezo huu wa kupendeza. Umaarufu wake na pesa nyingi ambazo wachezaji wanalipwa zime wapatia wazazi wengi msukumo kuwa watoto wao watageuka kuwa kama Cristiano Ronaldo, Leonardo Messi, Jay Jay Okocha na kadhalika.

Hivi majuzi, ili ripotiwa kuwa mwanamme waliwaita watoto wake watatu wa kiume baada ya wachezaji mashuhuri wa Manchester United Football Club. Vijana wake wali patiwa majina ya watu wanao sifika wa kadanda Ryan Giggs, Ole Gunnar Solksjaer na Eric Cantona. Ukifikiria kuhusu jambo hili, ingekuwa vigumu sana kwake kuyaeleza haya kwa majirani wake wa Yoruba kuwa ‘Ole’ haihusiki popote na kuiba kwani lina maana ya ‘mwizi’ huko Yoruba.

  Majina maarufu ya watoto wa kiume Nigeria na maana yao

Nigeria ina vikundi vingi vya kikabila. Kila kikundi kina baadhi ya majina maarufu ya watoto wa kiume. Baadhi ya familia zina hakikisha kuwa baadhi ya majina yana wakilishwa kwa kila kizazi, kumaanisha kuwa lazima mmtu mmoja awe na jina hilo kwa kila kizazi.

Majina yaliyo itwa watoto wadogo yalikuwa ishara ya nguvu za familia, utajiri, nafasi kwa jamii, mafanikio ya wazazi, na athiri kwenye jamii. Hali na matukio kabla na baada ya kuzaliwa kwa mtoto yanaweza athiri jina la mtoto. Yafuatayo ni majina katika kabila tofauti Nigeria na pia yaliko toka maana yake halisi.

Adeyemi  

Jina hili mara nyingi lina husishwa na taji ama ufalme. Ade lina maana ya taji ama ufalme. Ukitafsiri jina hili, lina maana, ‘nastahili kuvalia taji’ ama ‘ taji linanifaa.’

Akinbiyi  

Jina hila lina tambulisha uwezo wa baba kwani lina maana ya ‘shujaa alimzaa huyu.’

Abiodun   

Jina hili linamwambia kila mtu kuwa mtoto kama huyo alizaliwa wakati wa sherehe.

Banjoko   

Katika utamaduni wa watu wa Yoruba, watoto ambao hawajakomaa wanapata ‘Abiku’; watu waliamini kuwa watoto kama hawa walikuwa na uwezo wa kuzaliwa tena kwa njia tofauti. Na kwa hivyo kupata majina maalum ya watoto walio zaliwa kama hawaja komaa. Banjoko lina maana ya ‘kaa na mimi.’

Tanimola

Bila fiche, lina maana ya ‘Hakuna anaye jua kesho italeta nini.’ Na kuashiria kuwa wazazi wa mtoto huyu wana matarajio ya maisha ya mambo mema kwa mtoto wao.

nigerian boy

Umepata jina lililo kupendeza kwenye orodha yetu ya majina ya kiume ya Nigeria?

Majina ya Kiume Nigeria: Majina ya kiume ya Igbo na maana yake

Chukwuemeka

Katika Igbo, jina hili lina maana ya Mungu amefanya kitu kikuu. Hili ni jina unalo mpatia mtoto wa kiume aliye zaliwa kwa familia iliyo kuwa ikiomba na kutarajia kupata mtoto wa kiume.

Nnamdi  

Katika utamaduni wa Igbo, matumaini ya kupatana tena, yana hamasisha jina hili kwani lina maana ya ‘babangu yu hai.’ Wazazi wanawapatia watoto jina hili wanapo dhani kuwa baba yao amezaliwa tena.

Okafor   

Hili lina maana ya nilizaliwa Afor, mojawapo ya siku za wiki ya Igbo.

Fumnanya  

 Kama Banjoko katika utamaduni wa Yoruba, Fumnanya lina maana ya ‘nipende.’ Na ni jina linalo patiwa mtoto aliye zaliwa baada ya kifo cha mpendwa anaye aminika kuzaliwa tena.

Majina maarufu ya Hausa ya watoto wa kiume

Aminu  

Lina maana ya anaye aminika.

Faruq

Jina hili lina maanisha anaye baini kati ya ukweli na uongo.

Danjuma

Hili ni jina la mtoto aliye zaliwa siku ya Ijumaa.

Jina la mtu ni kitambulisho chake. Huko Nigeria, majina ni sifa, majina ya kuthibitisha na baadhi ya wakati, kile ambacho wazazi wana tarajia. Kama tulivyo ona, wana Nigeria wanaelewa upekee huu zaidi ya nchi nyingine ile. Utapata watu wakiwaita watoto majina ya kipekee ya vijana wao, ila kuna watu ambao wanabaki na kutumia majina ya utamaduni yanayo wapendeza.

Kwa hivyo mara unapo ona mtoto wa kiume wa Nigeria, kuwa tayari kusikia zaidi unapo uliza, ‘Jina lako ni nani?’ Huenda jibu lika kushtua.

Guardian NG

Soma pia: What your baby’s time of birth says about their personality

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio