Majina Ya Kipekee Ya Watoto Wa Kiume Ya Igbo

Majina Ya Kipekee Ya Watoto Wa Kiume Ya Igbo

Jina ni nini? Tazama majina haya na maana yake!

Orodha wa majina ya Igbo ya watoto wa kiume itakusaidia kuchagua jina la kipekee la mtoto wako.

 Je, watu huchagua vipi majina ya Igbo ya watoto wa kiume wao?

majina ya watoto wa kiume ya Igbo

Hizi ndizo sababu zinazo athiri jina la mtoto katika Igbo.

Some of these factors are: Baadhi ya sababu hizi ni

  • Hali iliyo zingira kuzaliwa kwa mtoto
  • Hali za wazazi wakati mtoto alipo zaliwa
  • Mahali pa kuzaliwa pia pana athiri majina ya watoto wa kiume wa Igbo
  • Nafasi ya mtoto kati ya ndugu zake
  • Mambo yanayo tendeka karibu na kuzaliwa kwake

majina ya watoto wa kiume ya Igbo

Tazama majina haya ya watoto wa kiume ya Igbo na maana

Diokpa: Mtoto wa kiume wa kwanza.
Ifeadigo: mwangaza umekuja. Jina hili linapatiwa mvulana ambaye ana mandugu wengi wa kike
Obiajulum:  Sasa moyo wangu umetulia. Jina hili pia hupeanwa kwa mtoto wa kiume aliye ngojewa sana.             Ikpa: shamba. Iwapo mtoto alizaliwa shambani, angepewa jina hili.
Dinta: mwindaji: Iwapo mvulana huyu angekuwa ama babake ni mwindaji mkuu.
Ebubedike: utukufu wa shujaa. Linapatiwa mtoto wa shujaa.
Nwigwe: Kijana wa mfalme.
Nwafor: Kijana aliye zaliwa siku ya soko ya Afor
Nworie: Kijana aliye zaliwa siku ya soko ya Orie.

Nweke: Kijana aliyezaliwa siku ya soko ya Eke
Nwankwo: Kijana aliye zaliwa siku ya soko ya Nkwo
Nwolisa: mtoto wa Mungu.
Olisa: Mungu
Ikechukwu: nguvu za Mungu. (mojawapo ya kawaida ya vijana wa ki Igbo)
Ikenna: Nguvu za baba
Chibunna: Mungu ni baba
Chukwuemeka: Mungu ametenda mema

Chinazo: Mungu anaponya
Chijindu: Mungu anashikilia maisha. Jina hili linapatiwa kwa kijana ambaye karibu apoteze maisha yake alipokuwa akizaliwa, ambaye mamake alikufa baada ya kujifungua, aliye zaliwa baada ya kifo cha mwana familia. Ni mojawapo ya majina ya ki Igbo ya vijana ya mtoto aliye zaliwa baada ya kifo kufanyika.                                                        Ozoemena: Lingine lisitendeke. Kisa kama cha hapo juu.
Chidindu: Mungu yu hai

Onwubiko: Kifo, tafadhali. Jina hili na maarufu kwa wazazi walio poteza watoto wengine.
Nnanna: baba ya baba. Jina hili linapatiwa kijana ili kuendeleza maisha ya babu yake.
Ifeanyichukwu: hakuna kitu kikubwa kuliko Mungu. Jina hili linapatiwa kwa kijana aliye tafutwa kwa muda mrefu ama kwa wazazi wanao taabika.
Obi: moyo. Obi pia ni jina la kwanza, kama tulivyo orodhesha hapa chini.

Baadhi ya majina ya vijana ya Igbo na maana

majina ya watoto wa kiume ya Igbo

Obinna: moyo wa baba ama kiwanja cha baba.
Obiora: moyo ama kiwanja cha jamii.
Obinne:  moyo wa mama
Obinwanne: upendo wa kaka
Obianwuna: wacha moyo/kiwanja kisife
Kanzekwe: machifu wa juu wakubaliane
Ojekanwaehi: anaye tembea kama ndama

Eze: Mfalme. hili pia huenda likawa jina la kwanza
Ezeamama: mfalme anaye julikana vyema
Ezeimenderi:  mfalme wa usiku
Ezeanyanaso: mfalme ambaye macho yanaona
Oguchinalurum: vita ambavyo Mungu anani pigania
Tobenna: mwabudu baba

Tobechukwu: Mwabudu Mungu
Lotanna: mkumbuke baba
Lotachukwu: kumbuka Mungu
Somadina: natumai nisiwe peke yangu
Chikamso: nafuata Mungu
Chibuzo: Mungu ndiye njia

Uzodimma: njia ni nzuri
Uzoma: njia nzuri
Nnamdi: baba yangu anaishi. Hili ni mojawapo ya jina la vijana wa Igbo aliye itwa baada ya baba yake aliye kufa.

Majina ya Igbo ya watoto wa kiume: Angalia maneno zaidi tuliyo orodhesha

Chinedu: Mungu anaongoza
Uchenna: mawazo ya baba
Uchechukwu: mawazo ya Mungu
Nwadiaso: mtoto huyu ni mtamu/mtakatifu
Beluchi: lia kwa Mungu

Nkemakolam: naomba wangu wasiniache
Chukwudi: Kuna Mungu
Chukwunonso: Mungu ako karibu
Munachiso: Niko na Mungu
Kamsiyonna: jinsi nilivyo mwuliza Mungu
Zikoraifechukwu: onyesha dunia mwangaza wa Mungu
Jidenna: mshike baba
Onyekachi: nani mkubwa kuliko Mungu?

Zeribe: epuka watu wabaya
Ochudo: anaye kimbiza amani
Ume: pumua
Uwazurike: wacha dunia ipumzike sasa
Oliseloka: Mungu amefikiria vyema
Chike: ni jina la mkato la 'chineke' lenye maana ya Mungu mwumbaji
Ndubueze: maisha ni mfalme
Chigoziem: Mungu anibariki

Okani: kuu
Ogugua: kujifariji
Okenna: kipande cha baba
Nwachukwu: mtoto wa Mungu
Kelechi: shukuru Mungu
Chizaram: Mungu alinijibu
Chibidoro: Mungu alianza

Nwabugwu: mtoto ni kitu cha fahari
Ugwu: mlima
Onu: shingo
Chimaobi: Mungu anajua moyo wangu
Muoneke:  roho inaumba
Muonanu: inaweza sikia
Onwuegbuchulam: twaomba kifo kisinichukue
Azubuike: nyuma/mgongo ndiyo nguvu

Kachimezuo: Mungu amalizie..
Amuka: kicheko ni kikubwa
Chukwumerije: Mungu aliumba safari
Chukwudumaga: Mungu ananiongoza (sio jina maarufu kwa sababu linaweza fupishwa kuwa 'maga,' kumaanisha mpumbavu)
Ezomchi: Namfuata Mungu
Enyinnaya: rafiki ya babake
Ogbonna: mwenye jina sawa na babake

Ejike: na nguvu
Ejidike: ana shikilia shujaa
Echezona: usisahau
Onyedikachi; nani kama Mungu
Onyeneke: anaye umba
Dikoma: shujaa mwenye moyo mwema
Okoro: mwanamme mwenye nguvu
Udo: amani

Haya ndiyo majina ya kipekee zaidi ya watoto wa kiume wa Igbo! Ni matumaini yetu kuwa utapata jina la kipekee kwenye orodha hii la mtoto wako wa kiume!

Kumbukumbu: Pulse.ng

Soma pia: A-Z Yoruba Names For Your Kids (With Meanings!)

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio