Kenya ni nchi inayo julikana na kusifika kote kwani ina jamii zaidi ya 42 zote ambazo zina lugha tofauti na zingine. Kwa kweli tamaduni za nchi hii ni za kupendeza. Kila jamii ina majina maalum inayo ita watoto wake kufuatia historia yao. Hapo zamani, majina ya watoto wasichana nchini Kenya ili lingana na wakati ama mahali ambapo mtoto huyo alizaliwa. Kuna tamaduni ya kuwaita watoto majina ya nyanya zao pia. Kwa kawaida nyanyake mtoto ndiye aliye mpa mjukuu wake jina.
Makala haya yana angazia majina ya watoto wasichana Kenya na maana yake katika jamii tofauti.
Jamii ya Wakikuyu
Jamii hii inajulikana kuwa na mabinti wapenda pesa na wenye bidii zaidi katika kazi zao.
Mumbi
Jina hili ni maarufu sana na lenye heshima. Kwani Mumbi anajulikana kama mama aliye ianza jamii hii.
Lina maana ya mwenye kuumba.
Wanjiku
Katika jamii ya wakikuyu, kuna imani kuwa Wanjiku alikua mmoja kati ya mabinti tisa wa Mumbi. Jina hili lina maanisha
Wanjiru
Binti ya Gikuyu na Mumbi. Kwa kikuyu, ‘njiru’ ina maana ya nyeusi. Wanjiru ina maana ya kutoka kwa nyeusi.
Wangari
Moja kati ya mabinti tisa wa Mumbi. ‘ngari ina maana ya chui. Wa ina maana ya kutoka kwa. Jina la wanawake wanaosifika nchini kenya na duniani kote kama vile Wangari Maathai.
Nyambura
Watoto wasichana nchini Kenya wenye jina hili walizaliwa msimu wa mvua. Mbura ina maana ya mvua. Huenda pia akaitwa Wambura.
Wanja
Ina maana ya nje. Msichana aliye zaliwa nje.
Nyakio
Lina maana ya kufanya kazi. Msichana mwenye bidii kweli kweli. Jina la binti anaye pendeza.
Huenda pia akaitwa Wakio. Pia limetumika katika vitabu kama vile “The Beautiful Nyakio”.
Nyaguthii
Anaye penda kutembea. Huenda mamake ama nyanyake alipenda kutembea. Huenda pia akaitwa Waakuthii.
Muthoni
Jina maarufu katika jamii ya wakikuyu. Lina maana ya shemeji.
Murugi
Jina la kupendeza lenye maana ya anaye pika. Msichana anaye penda kujishughulisha pale jikoni na kutimiza majukumu yake ya msichana ya kiasili ya kupika.

Jamii ya Wakamba
Jamii hii inajulikana kuwa na wasichana warembo. Majina maarufu ni kama vile:
Mutheu
Msichana huyu ni msafi wa kitabia na kiroho. Hana doa lolote lile.
Mwende
Lina maana ya aliye pendwa. Huenda mamake ama nyanyakee alipendwa katika familia ile.
Syokau
Mwenye kupenda vita. Miongoni mwa wasichana usio taka kuchezea shere kwani hawaogopi vita.
Kathini
Watoto wasichana wenye jina hili walizaliwa kwa familia zisizo na hela. Lina maana ya maskini ama aliye teseka.
Kalekye
Maana yake asili ni msichana aliye achiliwa. Ana uhuru wa kufanya kinacho mpendeza. Jina la watu maarufu kama vile Kalekye Mumo.
Mueni
Lina maanisha mgeni. Aliye tembea mbali na kwao.
Muthethya
Anaye saidia ama msaidizi.
Kanini
Ina maana ya ndogo. Msichana mdogo. Kwa kawaida, wasichana wenye jina hili huwa na mili midogo.
Kalimi
Anaye lima ama anaye penda kulima. Familia ya wakumba ilijulikana kwa matembezi ya masafa marefu. Walitembea na kubadilisha vitu walivyo kuwa navyo kama mikanda na viondo na kupewa vyakula na jamii zingine. Iwapo nyanyake alipenda kulima, angemuita mjukuu wake Kalimi.
Mutindi
Maana yake ni kukawia. Msichana anaye penda kukawia katika kuli tekeleza jambo fulani.
Jamii ya waluo
Jamii inayo julikana kuwa na wasichana walio barikiwa na mili ya kupendeza.
Achieng
Msichana aliye zaliwa siku iliyo kuwa na jua kali ama msimu wa jua kali.
Adhiambo
Aliye zaliwa jioni.
Adongo
Mtoto aliye mchanga zaidi kati ya mapacha.
Aoko
Jina hili lina maana ya binti aliyezaliwa nje.
Apiyo
Aliye mzee kati ya mapacha.
Atieno
Aliyezaliwa usiku.
Awiti
Mtoto msichana aliye okotwa kando ya barabara.
Awino
Aliyezaliwa msimu wa mahindi kutia maua(flowering).
Ayoo
Mtoto aliye zaliwa kando ya barabara.
Auma
Aliyezaliwa akitizama chini
Akeyo
Msichana aliyezaliwa msimu wa kuvuna.
Akoth
Mtoto msichana aliye zaliwa msimu wa mvua.
Jamii ya wameru
Mabinti hawa wanajulikana kuwa wenye hasira zaidi.
Kathure
Jina la kupendeza na linalo tumika zaidi. Lina maana ya aliye chaguliwa.
Kambura
Msichana aliyezaliwa wakati wa mvua.
Gakii
Binti anaye penda kutengeneza uji.
Karimi
Lina maana ya anaye penda kulima.
Kagwiria
Msichana anayependa kufurahi.
Mukami
Lina maanisha anayependa kukamua.
Kendi
Msichana aliyependwa zaidi.
Nkatha
Mwenye mali. Mara nyingi watoto wenye jina hili huibuka kuwa matajiri.
Kathambi
Msichana msafi, anaye penda kuoga wakati wote.
Makena
Binti anaye penda kufurahi. Kama vile Dj Pierra Makena.
Jamii ya wakisii
Kwamboka
Lina maana ya kuvuka. Binti asiye na uwoga wa kuanza upya na kuvuka mipaka ya kufaulu maishani.
Kerubo
Lina maana ya uwanja.
Nyachoka
Jina hili lina maanisha nyuki. Wasichana hatari.
Nyachera
Ina maana ya njia, msichana anayependa kushika njia ama aliyezaliwa njiani.
Nyaboke
Maana yake ni asali. Msichana anayependa asali.
Kemunto
Maana ya jina hili ni ziwa.
Bosibori
Mwenye uhuru wa kufanya atakacho. Kwa kawaida wasichana wenye jina hili hawana uwoga wowote.
Bisieri
Lina maana ya mlango.
Gesare
Maana ya jina hili ni kunde.

Jamii ya wamaasai
Wanajulikana kwa kuwa na wasichana wanao pendeza na wasio na maneno mengi.
Nashipae
Mwenye furaha nyingi.
Naserian
Ina maana ya amani. Msichana anaye penda amani na utulivu.
Nasieku
Msichana anayependa kufanya mambo haraka haraka.
Nemelok
Kipenda roho cha wote. Anapendwa na kila mtu.
Naeku
Aliyezaliwa asubuhi na mapema.
Naipanoi
Aliye mkubwa zaidi.
Namunyak
Binti aliye mrembo kati ya wote.
Jamii ya wataita
Wana mabinti wanao sifika kwa urembo wao.
Wakio
Maana yake ni msichana wa usiku.
Wakesho
Kesho ina maana ya siku inayofuata. Msichana wa kesho.
Wachia
Mtoto msichana aliyezaliwa barabarani.
Wawuda
Binti anaye julikana kupenda kuanzisha shida.
Waleghwa
Aliye kataliwa.
Mkamburi
Mburi ina maana ya mbuzi, mka ni bibi ya.
Mkangondi
Maana ya mka ni bibi, na ngondi inaashiria kondo.
Malemba
Matawi yaliyo nawiri yenye rangi la kijani.
Mkabili
Maana yake ni alama za kuzaliwa.
Jamii ya wakalenjin
Cherop
Aliyezaliwa msimu wa mvua
Chepkemoi
Msichana aliyezaliwa usiku.
Chebet
Mtoto msichana aliyezaliwa majira ya saa sita za mchana/ alfajiri.
Cheruto
Aliyezaliwa katikati ya safari
Chepng’etich
Msichana aliyezaliwa majira ya asubuhi kabla ya kuwapeleka wanyama malishoni.
Chemaiyo
Lina maana ya aliyezaliwa watu walipokuwa wakiunywa mvinyo.
Chepkemei
Aliyezaliwa wakati wa ukame.
Cherono
Mtoto aliyezaliwa jioni.
Cheplagat
Aliyezaliwa mapema kabla ya saa sita za usiku.
Chepchirchir
Mtoto aliyezaliwa watu walipokuwa na mbio.
Chemutai
Msichana aliyezaliwa asubuhi na mapema.
Haya ni baadhi ya majina maarufu zaidi ya watoto wasichana Nchini Kenya. Tuna tumai kuwa kwa sasa umefahamu maana ya jina lako.