Majina Ya Kipekee Ya Watoto Wasichana Wa Igbo Ya 2020

Majina Ya Kipekee Ya Watoto Wasichana Wa Igbo Ya 2020

Unajua wanacho sema kuhusu wasichana wa Igbo kuwa warembo zaidi. Majina yao sio tofauti.

Kuchagua jina la mtoto msichana kuna hitaji utafiti na uamuzi mwingi. Baadhi ya wakati, nyanya na babu wa mtoto wata wapatia wazazi orodha ya majina ili wachague. Ila, hili pia halita rahisha kazi ya wazazi. Maneno yaliyo pendekezwa huenda haya tawapendeza wazazi kufuatia maana, umuhimu hata sauti yake. Hapa ni orodha ya majina ya watoto wasichana wa Igbo na maana yao.

Igbo names for girls

Historia ya Orodha Yetu ya Majina Ya Watoto Wasichana Wa Igbo

Mikusanyiko ya Igbo ya kumpatia mtoto jina

Lugha ya Igbo inatumika na watu kutoka  Kusinimashariki na pande za Kusini-kusini mwa Nigeria. Ni lugha yenye utajiri na inayo tumika sana. Majina ya Igbo sio tofauti. Majina mengi ya wasichana ya Igbo yana maana za ndani. Baadhi yake hata huwa kana kwamba hadithi.

Majina kama ‘Ekwutosi’ ama ‘Onukwube’ kwa kawaida huashiria kuwa wazazi wa mtoto wamekuwa wakiongelelewa mjini. Majina kama ‘Nkeiruka’ yana ashiria kuwa mtoto alizaliwa katika nyakati ngumu na kuwa wazazi wana matumaini ya maisha mema.

Jinsi dini inavyo athiri majina ya watoto wa kike wa Igbo

Tamaduni za kuwaita watoto majina hazija badilika sana hata na ukristo. Hata kama wazazi wengi wa kikristo wanachagua majina ya Igbo ya wasichana yanayo husisha jina la Mungu (Chukwu ama Chi), bado yana ashiria mambo yanayo zingira kuzaliwa kwa mtoto.

Katika visa ambavyo si vya kawaida, baadhi ya wazazi wabunifu pia huwapatia watoto wao majina ya kusifu. Majina kama vile ‘Ifenkili’, ‘Omalicha’. ‘Mma na ‘Ola’ ni baadhi ya majina maarufu sana ya kusifu yanayo patiwa watoto wa kike wa Igbo. Majina haya yana ashiria kuwa mtoto ni wa thamani na halinganishwi. Jamii zinaweza enda kwa vita kwa watoto kama hawa.

majina ya watoto wasichana wa Igbo

Baadhi ya majina ya ki Igbo ni ya kuamuru

Wana Igo mara kwa mara huwaita watoto wa kike majina ya kuamurisha. Majina kama haya yana onekana kuwa yaki mwongoza mtoto kwenye njia inayo faa ya maisha. Kwa mfano, mzazi huenda akamwita mtoto ‘Sopuruchukwu’, ama ‘Tochi’ kwa sababu wanawataka wawa heshimu Mungu ama Chukwu (ambalo ni jina wa Igbo wanamwita Mungu)

Mtoto anaye itwa jina ‘Lotanna’ ama ‘Jidenna’ hapaswi kamwe kusahau babake.

Mapacha hawana majina spesheli, kama ilivyo kesi kwa Yoruba. Wazazi wanatumia siri ama kuwapa majina yanayo anza na herufi sawa.

Jina la msichana linasema mengi kuhusu utu wake, historia na maisha ya usoni. Kwa hivyo, kabla ya kuchagua kutoka orodha ya majina, angalia orodha tuliyo kuandalia, ya majina ya kupendeza ya watoto wa kike wa Igbo. Kuwa na wakati mwema ukichagua jina litakalo mfaa mwanao.

Hapa ni orodha ya majina ya watoto wasichana wa Igbo na maana yake, kutoka A-Z

A
Adaeze – Binti wa kwanza wa mfalme
Akachukwu –  mikononi mwa Mungu
Adamma – binti wa kwanza mrembo
Adaego – binti wa kwanza anaye leta mali na utajiri
Adaoma – binti wa kwanza mzuri ama mrembo
Ahunna – Mmoja anaye kuwa na mwili wa babake ama wana fanana na babake
Akunna – utajiri ama mali ya baba

B
Bianonyerem – kuja uishi nami
Binyerem or Binyelum –kaa na mimi

C –
Chizitaram – Mungu alinituma
Chideziri – Mungu aliandika
Chibuzo – Mungu anakuja kwanza ama Mungu ni mkuu
Chinedu – Mungu anaongoza ama ana niongoza
Chiagoziem – Mungu ameni bariki
Chioma – bahati nzuri ama Mungu mwema

Chibundu – Mungu ni maisha
Chimdi – Mungu wangu yu hai
Chiamaka – Mungu ni mwema
Chinenye – Ni Mungu anaye peana
Chimamanda – Mungu wangu hata kosa
Chika – Mungu ni mkuu zaidi
Chizoba – Mungu ataishi kunilinda
Chinyere – Mungu alinipa

E
Eberechi – Neema za Mungu
Ekemma – Aliye zaliwa siku ya soko ya Eke
Ekpereamaka – maombi ni lazima ama ni vyema kuomba
Ekene – sifu

Esimnachi – Nilitoka kwa Mungu
Ekwutosi – Usini ongelelee vibaya ama wacha kuniharibia jina langu
Ezinne – mama mwema
Ezimma – mama mwema
Ezichi – Mungu mwema

F
Fechi – Hudumia Mungu ama msifu Mungu

G
Ginikachukwu – nani mkuu kuliko Mungu?
Ginikanwa – nini cha thamani zaidi kuliko mtoto?

list of igbo female names

Religious moms and dads somtimes choose names that honour God

I
Ifeanyi – hakuna kilicho kigumu sana kwa Mungu
Ihechukwu – Mwangaza wa Mungu
Ihunna – uso wa baba ama anaye fanana na baba
Ifechukwu – mwangaza wa Mungu
Ifedimma – kitu chema
Ifenkili – mrembo wa kushika

Ifunanya – mapenzi
Ifeoma – mrembo ama yule mwema
Ifeyinwa – hakuna kinacho linganishwa na mtoto
Ihuoma – aliye barikiwa ama mwenye fadhili
Ijeawele – kuwa na safari njema
Ijemma – kuwa na safari ya kupendeza

Majina zaidi ya watoto wasichana ya Igbo yako

J
Jachimma – msifu Mungu

K
Kairaluchukwu –  Tumwachie Mungu
Kosisochukwu – inavyo mpendeza Mungu
Kambili – wacha niondoke
Kamsiyonna – Mungu alinipa nilicho itisha

Kamsoluchukwu – Wacha nimfuate Mungu
Kasarachi – Mwambie Mungu ama mpe Mungu siri zako
Kasiemobi – nifariji
Kelechi – Mshukuru Mungu

L
Lebechi – mtazamie Mungu
Lotachukwu – mkumbuke Mungu

M
Mma – mrembo
Mmadiya – mmoja ambaye urembo wake unamfanya bwanake afurahie
Mkpulumma – mbegu nzuri
Mmasichukwu – matakwa ya Mungu

N
Nne – mama
Nnedimma – mama mwema
Nnenna – mama ya baba / nyanya
Nneka – mama ni mkuu

Nchekwube – mwamini Mungu
Nkechi – ni ya Mungu
Ndidiamaka – utulivu ni mwema
Nkeiruka – maisha ya usoni yana ng’aa

O
Ogadimma – itakua vyema
Oluchi – Umbo la Mungu ama uumbaji wa Mungu
Oma – nzuri ama rembo
Ogechi – wakati wa Mungu
Omasirichi – anaye mpendeza Mungu

Obiageli – aliye kuja kufurahia utajiri
Ola – lulu
Olaedo – dhahabu
Olaocha – fedha
Olachi – wa thamani wa Mungu
Olamma – lulu inayo pendeza

S
Somtochukwu –  msifu Mungu nami
Sopuruchukwu – heshimu Mungu
Sochi – Mungu tu

U
Ugoeze –  fahari ya mfalme
Uloaku – benki ama mahali ambapo mali yana hifadhiwa
Ugommaeze – wa kupendeza ama anaye leta fahari kwa mfalme

Z
Zara – Mungu alijibu
Zikeoranachimdimma – onyesha dunia kuwa Mungu ni mwema
Zinachimdimma – onyesha kuwa Mungu ni mzuri

Vyanzo: BBC News World Africa

Soma pia: Igbo names for boys

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio