Kulingana na desturi na mila za jamii nyingi nchini kenya, mtoto wa kijana alienziwa sana. Ilikuwa sherehe kubwa kijana alipozaliwa katika familia. Si kana kwamba mtoto wa kike hakufurahikiwa kwani wote ni baraka, ila nderemo na vigelegele vya kumkaribisha kijana vilikuwa zaidi. Kila jamii nchini Kenya ina majina ya watoto wavulana.
Majina mengi hutegemea mahali ambako watoto hawa walizaliwa ama msimu. Tuna kusudia kukupatia maarifa zaidi kuhusu majina maarufu zaidi ya watoto wavulana nchini Kenya katika baadhi ya jamii zinazo patikana nchini hii.
Makala haya yana angazia majina ya watoto wavulana nchini Kenya na maana yake
Jamii ya wataita
Mwamburi
Jina hili lina maanisha mtu wa mbuzi nyingi. Mvulana mwenye jina hili huenda alizaliwa wakati familia yao ilikuwa na mbuzi wengi.
Mwakima
Lina maana ya mpole. Mvulana mpole asiye na maneno mengi. Huenda pia akawa na aibu kidogo.
Mwang’ombe
Mtu wa ng’ombe. Alizaliwa katika familia yenye ng’ombe wengi ama wakati ambapo familia yake ilikua imebarikiwa na ng’ombe wengi. Pia kuna uwezekano alipokuwa anazaliwa kulikuwa na ng’ombe karibu.
Mwanjala
Kijana mwenye jina hili alizaliwa wakati kulikuwa na ukame mkali.
Mwakio
Mvulana mwenye jina hili alizaliwa usiku ama kulipokuwa na giza.
Mwangolo
Katika jamii hii, ngolo inamaana ya mtima ama ukipenda roho. Lina maana ya mpendwa.
Mwawasi
Huenda likawa ni jina la ukoo wake ama alizaliwa wakati familia ilikua inapitia shida nyingi.
Mwakisha
Kisha ina maana ya sehemu ya juu zaidi ya muwa isio tamu.
Kituri
Ina maana ya kimya. Mtu asiongea maneno mengi, kwa ujumla, amekimya ama kutulia.
Mwashimba
Ina maana ya simba. Huenda alipozaliwa kulikuwa na simba karibu.
Mwashighadi
Shighadi ina maana ya nje. Mvulana mwenye jina hili huenda alizaliwa nje ama pia nje ya ndoa.
Mbogho
Ina maana ya nyati. Kuna uwezekano kuwa kijana huyu alipokuwa anazaliwa kulikuwa na nyati karibu.
Jamii ya wamaasai
Leboo
Mtoto aliyezaliwa kwa kichaka.
Lekisho
Mtoto mwenye adabu na heshima zake.
Lemayian
Jina hili lina maana ya kubariki.
Sironka
Lina maana ya safi, lisilo kuwa na doa.
Koinet
Maana yake ni mrefu. Kwa mara nyingi wavulana wenye jina hili huwa warefu.
Lemuani
Aliyezaliwa katika familia ya larfe.
Jamii ya wakalenjin
Kiprop
Aliyezaliwa msimu wa mvua.
Kipkemoi
Mvulana aliyezaliwa usiku.
Kibet
Mtoto wa kiume aliyezaliwa majira ya saa sita za mchana/ alfajiri.
Kipruto
Aliyezaliwa katikati ya safari.
Kipng’etich
Mvulana aliyezaliwa majira ya asubuhi kabla ya kuwapeleka wanyama malishoni.
Kipmaiyo
Lina maana ya aliyezaliwa watu walipokuwa wakiunywa mvinyo.
Kipkemei
Aliyezaliwa wakati wa ukame.
Kiprono
Mtoto aliyezaliwa jioni.
Kiplagat
Aliyezaliwa mapema kabla ya saa sita za usiku.
Kipchirchir
Mtoto aliyezaliwa watu walipokuwa na mbio.
Kimutai
Mvulana aliyezaliwa asubuhi na mapema
Jamii ya wakamba
Mutuku
Mvulana aliyezaliwa usiku
Muuo
Ina maana ya amani
Kyalo
Lina maana ya safari
Mwanza
Maana yake ni wa kwanza
Kalungu
Maana ya jina hili ni sehemu.
Mbandi
Lina maana ya nzige
Makau
Aliyezaliwa wakati wa vita.
Jamii ya wakisii
Metobo
Lina maana ya miiba.
Meroka
Maana yake ni aina ya majani
Makori
Aliyezaliwa kwa njia ndogo.
Nyamari
Mwenye mali nyingi.
Ombiro
Mtu mweusi.
Ongegu
Aliyezaliwa kando ya mto.
Nyang’au
Ina maana ya fisi.
Jamii ya waluo
Otieno
Kijana aliyezaliwa usiku.
Onyango
Aliyezaliwa macheo.
Omondo
Aliyezaliwa kukikucha.
Odiwuor
Kijana aliyezaliwa saa sita za usiku.
Odhiambo
Mtoto wa kijana aliyezaliwa alasiri.
Ochieng
Aliyezaliwa jua lilipokuwa juu.
Okoth
Mvulana aliyezaliwa msimu wa mvua.
Oketch
Kijana aliyezaliwa msimu wa ukame.
Aoro
Aliyezaliwa wakati wa kiangazi.
Odongo/opiyo
Majina yaliyo pewa watoto mapacha.

Jamii ya wakikuyu
Uhuru
Asiye zuiliwa kufanya jambo. Jina hili linatumika na raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Njiraini
Lina maana ya barabara. Mtoto aliyezaliwa mama alipokuwa kwa barabara ama kando ya barabara. Jina lililo nadra sana kupata. Watu maarufu wanao litumia jina hili ni kama vile John Njiraini mkuu wa KRA.
Wachira
Lina maana ya kesi. Huenda mtoto huyu alizaliwa kulipokuwa na kesi katika familia ile.
Kimotho
Maana yake ni kushoto kama vile mkono wa kushoto. Anaye tumia mkono wake wa kushoto kutekeleza majukumu yake ya kila siku.
Muthii
Kijana anayependa kutembea ama kuenda saa zote. Huenda alipewa jina la babu yake aliyekuwa na tabia ya kutembea ama alipenda kuwa safarini wakati wote.
Mwangi
Mtu anayependa kuzurura wakati wote. Mkurugenzi mkuu wa benki ya Equity anajulikana kama James Mwangi.
Macharia
Anayependa kutafuta. Kama vile Samuel Kamau Macharia, maarufu kama S.K. Macharia wa Royal Media Services.
Murimi
Lina maana ya mkulima.
Gitonga.
Mwenye mali na utajiri mwingi. Huenda alizaliwa katika familia yenye mali na iliyo tajirika.
Kageni
Ina maana ya mgeni. Watu maarufu wenye jina hili ni kama vile Maina Kageni.
Jamii ya kimeru
Mwenda
Lina maana ya kijana anayependwa.
Muriithi
Maana yake ni mchungaji. Kwa mara nyingi huwa anayewachunga watu wake ama marafiki zake.
Kirimi
Jina hili lina maana ya mkulima. Huenda alizaliwa katika familia inayo pata riziki kutokana na kulima.
Mugambi
Mtetezi, haswa wa haki za watu. Anapenda kuongea na kutetea watu. Watu wanaopenda kuongea na kupiga kelele hasa wanapo kosewa.
Kimathi
Anayependa kutafuta. Huenda babu yake alipenda kuwatafutia riziki sana.
Koome
Mvulana mwerevu. Watoto wenye jina hili huipuka kuwa werevu zaidi.