Majina Ya Watoto Wa Kike Na Wa Kiume Yenye Maana Ya Mwanzo Mpya

Majina Ya Watoto Wa Kike Na Wa Kiume Yenye Maana Ya Mwanzo Mpya

Hapa kuna orodha ya majina yanayo maanisha mwanzo mpya ya kuwapa watoto wako. Kuzaliwa kwa mtoto ni mwanzo mpya na majina haya yatawafaa zaidi!

Mwaka mpya huja na ndoto na fursa mpya. Kwa hivyo pia, kuzaliwa kwa mtoto kuna ashiria mwanzo mpya. Iwapo ungependa mtoto wako awe na jina linalo ashiria nyakati alizo zaliwa, haya ni baadhi ya majina yanayo maanisha mwanzo mpya.

Majina yanayo maanisha mwanzo mpya

Hapa kuna majina ya kuvutia yanayo ashiria mwanzo mpya.

Ya wasichana

girl names for new phases

 1. Amaryllis

Kwa Greek, Amarylis ni jina la warembo wanao hama kutoka mahali pamoja hadi pengine, lina maana ya mpya na freshi.

 1. Anastasia

Anastasia  ni jina lenye mizizi ya Russia, lina maana ya 'kufufuka ama kuzaliwa tena'.

 1. Ausra

Sawa na jina Aurora, Ausra lina maana ya ‘kutwa’, ambayo ni wakati ambapo siku ingali changa na inaanzia tu.

 1. Fatiha

Fatiha ni jina lenya mizizi ya kiarabu, na ni maarufu katika baadhi ya nchi za Mashariki Katikati(Middle East) na nchi za bara la Afrika. Lina maanisha 'chanzo/mwanzo ama kwanza.'

 1. Neoma

Neoma ni jina linalo tokana na Naomi, na hata kama halitumiki sana, hivi majuzi limerudi. Lina maanisha 'mwezi mpya'.

majina yanayo maanisha mwanzo mpya

 1. Renee

Jina Renee ni maarufu kwa sababu ya mwigizaji nyota wa kike kutoka Umarekani anaye julikana kama Renee Zellweger anayekuwa nalo. Renee lina maanisha ‘kuzaliwa tena’.

 1. Roxanna

Jina hili lilitumika kwa mara ya kwanza Europe kabla ya kusambaa kwenye nchi zingine zinazo tumia lugha ya kimombo mwaka wa 1960. Lina maana ya 'kutwa'.

 1. Sahar

Jina hili mara ya kwanza lisikika katika nchi zilizoko Middle East na kisha kusambaa kwenye nchi kama vile US, India, na Pakistan. Lina beba maana ya 'asubuhi, kutwa ama kurauka'.

 1. Zerlinda

Jina hili la kupendeza la ki Hebrew lina tumika sana na watu maarufu. Lina maana ya 'kutwa ya kupendeza'.

Ya vijana

majina yanayo maanisha mwanzo mpya

 1. Asier

Jina hili ni maarufu sana Spain, ambako liko kati ya orodha ya majina 100. Lina maanisha 'mwanzo'.

 1. Arata

Arata lina mizizi ya Japanese na ni maarufu kwa kuwa na kipekee na sio maarufu sana. Lina husishwa na wana Japanese wanao julikana sana. Lina beba maana ya 'mpya ama freshi'.

 1. Fresco

Jina Fresco mara nyingi linatumika kama jina la mwisho. Lakini wakati wa hivi majuzi, watu wameanza kulitumia kama jina la kwanza. Fresco ni jina la Italia lenye maana ya 'freshi'.

 1. Irvin

Jina hili mwanzoni lilitumika kama Irving lakini limepoteza herufi ya 'g', na kulifanya lipendeze hata zaidi. Jina hili la kipekee lina ashiria 'freshi'.

 1. Neo

Neo lili vuma zaidi wakati ambapo mwigizaji Keanu Reeves alilitumia katika “The Matrix.” Jina Neo lina maanisha ‘kipya ama mpya,’ lakini katika Afrika, lina maana ya ‘zawadi.’

 1. Ordell

Iwapo ungependa jina la kale la mtoto wako wa kiume, jina Ordell lina maana ya ‘mwanzo’.

 1. Tan

Wakati huu, jina Tan ni maarufu sana Vietnam kwa kuwa fupi na la kupendeza. Kwa hivyo iwapo unatafuta jina fupi na linalo pendeza, Tan litakufaa zaidi. Maana yake ni ‘mpya’.

Mwanzo mpya una maana ya vitu tofauti na watu tofauti kwani sote tuko katika safari tofauti. Lakini umbali yanayo enda, majina haya ni kuhusu kuanza upya kutoka mahali ama mwanzo wa kitu. Ni tumaini letu kuwa orodha yetu ya majina yanayo maanisha mwanzo mpya itakusaidia kuchagua jina linalo pendeza la mtoto wako.

Soma pia: Majina Bora Zaidi Ya Kuita Mtoto Wa Kike 2020

Name Berry

 

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio