Ndoa huambatana na majukumu mengi ambayo wanandoa wanastahili kusaidiana. Sawa na kuwa na mimba na ulezi wa watoto. Mwanamme ana jukumu la kumsaidia bibi yake anapokuwa na mimba. Tazama baadhi ya majukumu ya mwanamme katika ujauzito. Kufanya hivi kunamsaidia mwanamke kuwa na safari rahisi zaidi ya mimba.
Majukumu ya mwanamme bibi anapokuwa na mimba

- Jielimishe
Wakati wote, kufahamu kitu ambacho mkeo anakipitia na kumsaidia ni muhimu kwake. Mwanamme anaweza kujielimisha kuhusu mambo yanayo fanyika katika ujauzito. Mwanamke mjamzito huwa na mahitaji mengi, kuna mabadiliko mengi yanayofanyika. Mwanamme anapaswa kujielimisha kuhusu vyakula bora katika ujauzito, mavazi ya mama mjamzito na jinsi anavyoweza kufanya kipindi hiki kiwe rahisi kwake.
2. Kumsaidia na ugonjwa wa asubuhi
Hata ingawa sio wanawake wote wanaotatizika na ugonjwa wa asubuhi, ni vyema kwa mwanamme kujielimisha kuhusu ugonjwa wa asubuhi. Iwapo bibi yake ana tatizika na hali hii, anaweza kumletea bidhaa zinazosaidia kuipunguza kama crackers.
3. Mhimize
Mwanamke mjamzito anastahili kuhisi kuwa hayuko peke yake katika safari ya ujauzito. Mbali bwanake ako naye na anamsaidia anapohisi amechoka. Homoni za mwanamke hubadilika sana anapokuwa na mimba. Na kumfanya awe na hisia nyingi, mara kulia bila sababu ama kukasirika. Ni muhimu kwa mwanamme kuelewa haya na kumwegemeza katika kipindi hiki.
4. Msaidie na majukumu ya nyumbani

Mimba inavyozidi kukua, ndivyo itakavyokuwa ngumu kwa mwanamke kufanya majukumu ya nyumbani. Kumsaidia mama kufanya kazi za nyumbani kama vile kusafisha vyombo na kupika kutampa wakati tosha wa kupumzika. Mpikie vyakula anavyotamani zaidi.
5. Tenga muda wa kuwa naye
Mwanamke mjamzito mara nyingi atashauriwa kuchukua muda apumzike. Mama anapokuwa nyumbani mara nyingi peke yake, ni kawaida kuhisi upweke. Mumewe anastahili kutenga wakati wa kuwa naye. Kuchukua muda kutoka kazini na kuwa naye nyumbani ama kumtembeza.
6. Chukua majukumu
Majukumu mengi ya kinyumbani huwa mikononi mwa mwanamke. Ila anapokuwa na mimba, ni vigumu kutekeleza majukumu haya. Majukumu kama vile kuhakikisha kuwa nyumba ina manunuzi ya mwezi ama wiki na chakula tosha cha wiki. Mwanamme anaweza kusaidia kwa kutimiza nyingi kati ya majukumu haya. Kufanya hivi kunamwezezesha mwanamke kuona kuwa anadhaminiwa. Pia unamsaidia kupata wakati tosha wa kupumzika.
7. Msikilize
Ujauzito huwa na panda shuke nyingi ambazo huenda zikamfanya mjamzito ahisi vibaya. Ni vyema kuchukua muda kila usiku na kusikiliza jinsi siku yake ilivyokuwa. Zungumza naye na umweleze kuwa mambo yote yatakuwa sawa.
Mbali na majukumu ya mwanamme katika ujauzito tuliyo angazia, ni muhimu kuandamana naye anapoenda kliniki zake za kila siku.
Chanzo: Healthline
Soma Pia:Ishara Za Mapema Zinazoashiria Mama Ana Mimba