Makosa 5 Ya Kingono Ambayo Wanaume Hufanya!

Makosa 5 Ya Kingono Ambayo Wanaume Hufanya!

Mchakato wote wa ngono unapaswa kuwa jambo nzima na linalo husisha viungo tofauti. Kumbuka kuwa kitu kinacho mpendeza mwanamke mmoja huenda kisi mpendeze mwingine.

Wanaume wengi hujiona kama weledi wa ngono lakini mara nyingi, wanaume kama hao hawawezi watosheleza wake ama wachumba wao kama vile ambavyo wanawake hao wangependa. Kuna makosa mengi ya wanaume katika ngono.

Kwa kweli, kuna haja gani ya tendo hilo ikiwa mchumba wako hahisi kenye unafanya kwa njia nzuri?

Kushindwa kwa waume kutekeleza tendo hili kwa njia inayo faa mara nyingi hufuatia kukosa ujumbe na fikira mbaya kuhusu wanavyo stahili kufanya tendo hili.

Makosa ya wanaume katika ngono

makosa ya wanaume katika ngono

1.Kufikiria kuwa ngono ni mashindano ya nguvu

Wanaume wanapaswa kufikiria kuwa tendo la ngono sio vita ama mashindano ya nguvu. Na kuwa uke wa mwanamke sio kiungo kinacho paswa kupigwa tu. Tendo la ngono lina hitaji ustadi ambao wanaume wengi hukosa.

Sio siri kuwa, kuna baadhi ya wakati ambapo wanawake hutaka ngono kakamavu. Lakini ikiwa wakati wote wewe kama mwanamme hii ndiyo ngono pekee uliyo nayo akilini, unapaswa kujitahini.

2. Kuendelea bila kikomo

Wanaume zaidi wanapaswa kuamini kuwa kumpendeza mwanamke na kumtosheleza kingono sio kufanya mapenzi kwa muda mrefu.

Kuendelea kwa lisaa limoja hakuonyeshi jinsi ulivyo mwanamme kamili, na mapenzi ya muda mrefu huenda yaka chosha.

Mapenzi yana stahili kuwa ya kufurahikia, na wala sio kuonekana kama mashindano ya kuonyeshana jinsi mwanamme alivyo stadi. Kwa hivyo wazo la kuwa unapaswa kufanya mapenzi kwa muda mrefu ili kumtosheleza mwanamke linapaswa kukoma.

3. Kubadili staili nyingi mbio sana

Unapo kaa ukimgeuza mchumba wako kwa pande zote, anakosa hamu ya kuhusika katika kitendo hicho. Kubadili staili katika kitendo cha mapenzi kunapaswa kuchukua muda na nyote mnapaswa kufurahia kipindi hiki.

4. Kumalizia ngono punde tu baada ya kufika kilele

Kufikiria kuwa ngono huisha punde tu unapofika kilele ni makosa kubwa zaidi, kwa sababu huko ni kujipenda.

Kufikiria kuwa kufika kilele ndiyo mwisho wa mchakato wote wa kufanya mapenzi ni kujipenda na kuto fikiria kuhusu mchumba wako. Kwa hivyo hata baada ya kufika kilele, hakikisha kuwa mwanamke pia anafika kilele na ametoshelezwa, na ikiwa bado haja fika, hakikisha unamsaidia kufika kilele chake pia.

5. Kupuuza viungo vingine vya mwili

Wanaume wanapo amua kufanya ngono iwe kuhusu uke tu, hawawezi mtosheleza mwanamke kwa njia zote zinazo faa.

Mchakato wote wa ngono unapaswa kuwa jambo nzima na linalo husisha viungo tofauti. Kumbuka kuwa kitu kinacho mpendeza mwanamke mmoja huenda kisi mpendeze mwingine. Kwa hivyo kuwa makini kufahamu kiungo kinacho msisimua mwanamke wako zaidi.

Soma PiaKinacho Wafanya Wanawake Kuwa Na Wachumba Nje Ya Ndoa

Written by

Risper Nyakio