Makubaliano wakati wa kurudi shule kwa kila mwanafunzi nchini Kenya

Makubaliano wakati wa kurudi shule kwa kila mwanafunzi nchini Kenya

Baada ya kila likizo, ni muhimu kwa kila mwanafunzi kuwa na makubaliano yatakayo msaidia anapo anza muhula mpya. Makubaliano haya yanamsaidia kuwa makini kwa masomo yake.

Baada ya kuwa nyumbani kwa muda mrefu wakati wa likizo, hakuna mwanafunzi anaye furahikia kurudi shuleni. Hii ni kwa sababu shuleni kuna ratiba wanao paswa kufuata ilhali nyumbani hakuna. Wanapata wakati wa kutosha wa kulala, wana amka wanavyopenda na pia wana weza kuvitazama vipindi wanavyo taka kwa wakati wowote ule. Hakuna kazi ya ziada. Wana wasaidia wazazi wao kwa muda mchache na kuweza kwenda Kucheza na marafiki zao, kubarizi ama kutembea mahali tofauti. Nyumbani kuna uhuru wa kufanya chochote kile wanacho hisi. Ilhali shuleni hakuna uhuru huu. Wakati mwingi wana paswa kuwa darasani, hata kama kuna wakati wa mapumziko, sio mwingi kama nyumbani. Pia baada ya kuwa na marafiki wako wa nyumbani kwa muda, hakuna anaye furahikia kumuaga mwingine.

Wakati huu wa kurudi shuleni hukuwa wenye hisia nyingi kama vile mawazo mengi, kufurahi kurudi shuleni baada ya muda na pia huzuni ya kuwaacha wazazi na marafiki wa nyumbani. Maneno chanya ya makubaliano na kujipa nguvu ni muhimu kwa wanafunzi wanapo rudi shuleni. Inawasaidia kuwa na mawazo na mtazamo chanya kwa masomo na maisha yao na pia mambo mengine wanayo kumbana nayo wakiwa shuleni. Maneno haya yanawasaidia watoto kuwa na imani, kukumbuka mambo wanayo soma shuleni na pia kuwa na uhusiano mwema na walimu na wanafunzi wenzao shuleni.

Baadhi ni maneno ya makubaliano kwa wanafunzi ya kurudi shuleni

Niko tayari kurudi shuleni

Kuyasema maneno haya kwa mtoto/mwanafunzi kunamsaidia kutoa akili yake nyumbani na mambo aliyo kuwa akiyafanya. Ili yafunguke na akubali kuwa anarudi shuleni na ako tayari kusoma.

Nina ujasiri, mimi ni jasiri na mpenda watu

Maneno haya yana mjaza mtoto na akili za ujasiri anapokuwa shuleni. Haogopi watu ila wana fanya urafiki na wanafunzi wenzake shuleni.

Nina umuhimu na mkarimu

Maneno haya yanamfanya mtoto kujiamini hata anapo feli kwa mtihani, anajipa moyo kuwa ana umuhimu na linamsaidia kutia bidii zaidi katika masomo yake.

Nina uwezo wa kuyakumbuka mambo mapya

Kuongea mambo chanya inamsaidia kuwa na mtizamo mzuri wa mambo anayo yafanya. Anapo kiri kuwa ana uwezo wa kuyakumbuka mambo, atajitahidi kuwa makini wakati wa darasa na kuyakumbuka mambo atakayo funzwa.

Niko tayari kutia bidii masomoni

Kawaida, mambo tunayo yasema na kuya weka akilini ndiyo hufanyika. Mwanafunzi anapo kiri kuwa ako tayari kusoma na kutia bidii, linamsaidia kuwa makini shuleni. Anaachana na mambo yote ya kinyumbani na anatilia mkazo masomo yake.

wanafunzi shuleni

Nawapenda marafiki na walimu wangu

Maneno haya yanamsaidia kuwa na uhusiano mzuri na watu wanao mzingira akiwa shuleni Ikiwemo wanafunzi wenzake na walimu. Inasaidia kuhakikisha hakuna vita vinavyo ibuka na anawapenda wenzake.

Niko tayari kupata marafiki wapya

Makubaliano haya yanamsaidia kuto kaa peke yake akiwa shuleni. Anahusiana na wenzake na pia kuwafanya marafiki wake ili wasaidiane wanapo kuwa shuleni.

Nina weza ibuka mshindi darasani

Ni muhimu kumpa mwanafunzi moyo anapokuwa shuleni. Na kumhakikishia kuwa yeye pia ana uwezo kama wengine wa kupita mtihani na kuibuka nafasi moja. Anapo ona kuwa kuna watu wanao mwamini, anajitahadi ili aibuke nambari moja. Ni rahisi sana kwa mwanafunzi kuishiwa na nguvu na kuto jiamini. Maneno haya ni muhimu sana.

Sina uwoga moyoni na akilini

Makubaliano haya yanamsaidia mwanafunzi kuwa na ujasiri kutoka moyoni. Iwapo alikuwa na uoga wa kurudi shuleni ama aliwaogopa walimu fulani, uoga huo unaisha. Anaweza kuyaweka mawazo yake kwa masomo na wala si kwa uoga kwa mwalimu fulani ama wanafunzi fulani. 

Shule yangu ni ya kupendeza na walimu wangu pia

Kuna uwezekano kuwa kuna wanafunzi wasio penda shule zao na walimu wao. Jambo hili lina fanya alama zao shuleni kudidimia. Mwanafunzi anapo kubali kuwa shule yake ni murua na walimu pia ni wema lina saidia kuwa na mtazamo chanya kuhusu shule yake na masomo.

Nitatimiza ndoto na lengo langu maishani

Mwanafunzi anapo kiri maneno haya, anaweka mchezo kando na kutia bidii kwa masomo ili aweze kutimiza ndoto na lengo lake maishani.

Makubaliano ni muhimu ili wana wanafunzi waweze kupata alama bora shuleni na pia waweze kuwa na muungano mwema na walimu na wanafunzi wengine shuleni.

 

Read Also: The Complete Back To School Shopping List For Mums

Written by

Risper Nyakio