Malengo 7 Ya Uhusiano Ya Kufanya Mapenzi Yenu Yawe Bora Zaidi

Malengo 7 Ya Uhusiano Ya Kufanya Mapenzi Yenu Yawe Bora Zaidi

Uhusiano wenu ni muhimu na nyote mnapaswa kuupatia kipau mbele. Ni rahisi kupuuza kazi mnayo hitajika kutia katika uhusiano.

Mapenzi yanapendeza. Tunapo fanya uamuzi wa mtu tunaye tamani kuishi naye maishani mwetu, pia tuna shaka kuhusu njia za kufanya hisia zetu kwa mwenzi wetu zidumu kwa muda mrefu. Kuna malengo ya kukuza uhusiano ili kuyafanya mapenzi yenu yawe bora zaidi na nyote mhisi kutosheleka.

Ni aina gani ya malengo ya kukuza uhusiano  yanaweza kufanya mapenzi yenu yawe bora zaidi?

malengo ya kukuza uhusiano

Unapo tengeneza malengo ya mapenzi ya kufanya umoja wenu uwe bora zaidi, mnapaswa kuweka malengo yanayo timizika. Mwanasaikolojia wa mahusiano, Zoe Coetzee, ana eleza malengo ya uhusiano kama, "somo hasa, ubora ama jambo la kutamani katika uhusiano wenu wa kimapenzi. Badala ya kuwa vigumu kutimiza, linapaswa kuwa hamasisha." Pia, yanawasaidia kujua njia bora zaidi ya kupatiana na kupokea mapenzi katika uhusiano wenu. Hapa kuna baadhi ya malengo ya uhusiano ambao unaweza kufanya mapenzi yenu yawe bora zaidi.

Malengo ya mapenzi ya kufanya uhusiano wenu uwe bora zaidi

wanawake kuanzisha ngono

  • Zungumza kwa uwazi na ufanisi

Ili uhusiano wenu ufuzu, unapaswa kuhakikisha kuwa una zungumza kwa uwazi na mwenzi wako. Na ujumbe wako kufika.

  • Ukweli

Kuwa mkweli kuhusu matarajio na matakwa yako. Ikiwa kuna kitu kisicho kufurahisha, usikipuuze.

  • Amini kwa moyo wote

Kuamini ni pacha la mapenzi. Ni kitu unacho pata kutoka kwa tabia zako kwa mwenzi wako. Ni mchakato unao zidi kuendelea. Wapenzi wanapaswa kuwa na imani kuwa hauta wafeli na unapaswa kuchagua kuwa mwaminifu wakati wote.

  • Kwa mazuri na mabaya

Kuna siku nzuri katika uhusiano na kuna siku zisizo nzuri. Unapo kimbia punde tu unapo ona taabu, huenda ikawa ingekuwa wazo nzuri kuto ingia kwenye uhusiano huo kutoka mwanzoni. Shida zinapo ibuka, tumia ujuzi wako wa mazungumzo kutafuta suluhisho. Pia ikiwezekana, mwone mshauri wa ndoa kama inahitajika.

  • Fahamu mahitaji ya mchumba wako

Hata mapenzi yanapo kuwepo, huenda tuka puuza mahitaji ya wachumba wetu. Wakati wote elewa mahitaji yao. Kufahamu hofu zao tuka kuelekeza jinsi ya kuwapenda kwa lugha yao.

  • Kubishana ipasavyo

Matatizo yanapo ibuka, jadilianeni vyema. Kuwa makini na maneno unayo tumia. Sio wakati wa kumkumbusha vitu asivyo fanya vizuri. Usitumie lugha hasi ama matusi, jadili unacho taka kwa upole hadi mpate suluhu.

  • Upatie uhusiano wenu kipau mbele

Uhusiano wenu ni muhimu na nyote mnapaswa kuupatia kipau mbele. Ni rahisi kupuuza kazi mnayo hitajika kutia katika uhusiano. Ikiwa kwa kweli ungependa uhusiano wenu ukue, unapaswa kuwa akilini zenu wakati wote. Uhusiano mzuri huchukua muda, wakati na kazi nyingi.

Soma PiaMazungumzo 5 Muhimu Sana Katika Uhusiano Yasiyo Paswa Kupuuzwa

Written by

Risper Nyakio