Malengo 10 Ya Uhusiano Yatakayo Fanya Mapenzi Yenu Yakue

Malengo 10 Ya Uhusiano Yatakayo Fanya Mapenzi Yenu Yakue

Malengo ya uhusiano ni mwongozo wa jinsi ya kupendana. Malengo haya yatasaidia mapenzi yenu kukua zaidi.

Mapenzi ni kitu cha kupendeza. Tunapo fanya uamuzi wa mtu ambaye tungependa kuishi na yeye milele, tuna hofu kuhusu jinsi utakavyo fanya ili mapenzi yenu yadumu muda mrefu. Kuna malengo ya uhusiano ili kufanya mapenzi yenu yawe na ladha.

Ni aina gani ya malengo ya uhusiano yanayo fanya mapenzi yenu yadumu?

What are the relationship goals that will make your love stronger

Unapo weka malengo ya uhusiano ambayo yanaweza fanya mapenzi yenu yawe na nguvu zaidi, unapaswa kuweka malengo ambayo utaweza kutimiza. Mwana saikolojia wa uhusiano Zoe Coetzee ana fafanua "malengo ya uhusiano kama ushuhuda wa kulenga unapokuwa kwa uhusiano na mchumba wako. Badala ya kuwa kiwango ambacho hakiwezi timizika, yana paswa kuwa hamasisho kwako." Pia alifafanua malengo ya ndoa kama jinsi ya kupatiana na kupokea mapenzi katika uhusiano wako. Kuna baadhi ya malengo ya ndoa ambayo yatafanya mapenzi yenu yawe na nguvu zaidi.

Malengo 10 Ya Uhusiano Yatakayo Fanya Mapenzi Yenu Kukua

malengo ya uhusiano

  • Ongea kwa uwazi na vyema

Ili uhusiano uwe na mafanikio, unapaswa kuzungumza vizuri na kwa njia ya kueleweka na mchumba wako.

 

  • Uaminifu

Kuwa mwaminifu kuhusu matarajio yako na matakwa yako. Ikiwa kuna jambo ambalo halikupendezi, haupaswi kupuuza, hakikisha kuwa unaongelelea jambo hilo.

 

  • Mwamini mchumba wako

Imani ni muhimu sana katika uhusiano. Imani huja na wakati unapokuwa katika uhusiano kulingana na tabia za mchumba wako. Ni utaratibu na jambo linalo kuja baada ya muda. Wachumba wanapaswa kuwa na imani kuwa hauta waumiza.

Build Trust

 

  • Kwa wakati wote, mema na mabaya

Kila uhusiano huwa na nyakati mbaya na zingine nzuri. Hakuna uhusiano ambao hauna matatizo yake. Lakini kama mnapokuwa na tatizo lolote unakimbia, hauko tayari kuwa katika uhusiano na mtu. Ikiwa mna shuhudia matatizo katika uhusiano wenu, mnaweza ongea na mtaalum wa ndoa awashauri.

  • Kufanya mapenzi (jaribu mambo mageni)

Kuna hisia za mapenzi unazo hisi siku za kwanza chache katika uhusiano wenu unapo mtazama mchumba wako. Nafasi nyingi ni kuwa baada ya muda, hisia hizi zita didimia. Ni jambo la busara kwa wachumba kuwekeza katika mambo ambayo yana wafurahisha. Fahamu zawadi ambazo mchumba wako ana pendelea na umnunulie mara kwa mara.

 

  • Jali mahitaji ya mwenzi wako

Hata wakati ambapo mapenzi hayako, huenda tukapuuza ama kukosa kugundua mahitaji ya mwenzi wako. Pia unaweza mwuliza mchumba wako vitu ambavyo angetaka katika uhusiano wenu.

 

  • Kuwa na mjadala wenye afya

Ni vigumu kuepuka matatizo katika uhusiano. Mtakuwa na maoni tofauti kuhusu mambo mbali mbali maishani. Kwa hivyo mnapokuwa na shida hizi, ni vyema kuwa na mjadala wenye afya na kutatiza shida mlizo nazo. Epuka kutumia lugha yenye makali ama matusi mnapo ongea na mchumba wako.

  • Hakikisha unapata wakati wa kujitunza

Wewe ni mtu binafsi. Kuwa wazi na mambo unayo penda kufanya. Uhusiano hufuzu na watu wawili wanao elewa mambo wanayo penda kufanya. Haupaswi kujifunika kwa sababu umepata mchumba. Huu ni wakati wa kuwa na nafasi zinazo kuhimiza kuonyesha talanta yako. Pia ni nzuri kwa afya yako ya kiakili na itakupatia kitu cha kuongea kuhusu.

  • Mkue pamoja

Ni vyema kuelewa kuwa wakati unavyo zidi kupita ndivyo unavyo zidi kuelewa utu wa mchumba wako. Unapo zidi kukua katika uhusiano wenu, mchumba wako huenda akaiga kufanya vitu vinavyo kupendeza. Kwa njia hii mtapata wakati mwingi zaidi wa kuwa pamoja mnapo fanya vitu vinavyo wafurahisha.

  • Patia uhusiano wenu kipau mbele

Hakikisha kuwa una patia uhusiano wenu kipau mbele. Ikiwa mchumba wako ni mtu ambaye sio mgumu, huenda ukapuuza kazi mnayo hitajika kufanya ili uhusiano wenu ufanikiwe. Ikiwa ungependa mapenzi yenu yazidi, mnapaswa kuhakikisha kuwa mnapatia uhusiano wenu kipau mbele. Uhusiano mzuri huchukua muda, kuwekeza kwingi, kujitolea kwa sana.

Tunapo ona wanandoa wakiishi maisha mazuri kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, tuki wapongeza na kutamani mapenzi yetu yangekuwa sawa na yao. Watu wengi hupuuza ukweli kwamba wawili hao walitia juhudi nyingi katika mapenzi yao hadi yalipofika mahali yalipo fika.

 

Soma pia: Jinsi Ya Kuwa Na Urafiki Utakao Badilika Kuwa Uhusiano Wenye Nguvu

Chanzo: HuffPost

Written by

Risper Nyakio