Orodha Muhimu Kwa Mama Anaye Tarajia

Orodha Muhimu Kwa Mama Anaye Tarajia

Ni muhimu kwa mama anaye tarajia kufahamu kuwa mwili wake utabadilika sana baada ya kujifungua lakini akumbuke kuwa ataupenda mwili wake kwa kipimo sawa.

Kuna mengi ya kufikiria kuhusu katika mimba. Hakuna orodha moja inayo weza kutosheleza maswali yote ambayo mama mjamzito huenda akawa nayo katika kipindi hiki. Mama pia anafikiria kuhusu maisha baada ya mtoto kuwasili. Hii ndiyo sababu kuu kwa nini tume orodhesha maswali muhimu kwa mama anaye tarajia kumsaidia kuanzia.

Uhusiano wako

mama anaye tarajia

Ikiwa utangamano wenu kama wanandoa sio mzuri vile, huenda ukashangaa kama kufika kwa mtoto wenu kuta tatiza uhusiano wenu. Karibu 2/3 ya wanandoa hupata kuwa ubora wa uhusiano wao umepungua katika kipindi cha miaka mitatu baada ya kujifungua mtoto na kutosheleka katika uhusiano hudidimia mara mbili ikilinganishwa kwa wanandoa wasio na watoto.

Lakini unapo panga vyema, kuwasiliana na kutia juhudi, mnaweza dumisha furaha na afya baada ya kuwasili kwa mtoto.

Masharti na ratiba

Ngoja kualikwa hospitalini kabla ya kuennda. Usimbusu mtoto. Na kila mtu aliye chumbani sawa na mtoto ana hitaji chanjo dhidi ya kikohozi. Kuna masharti ambayo wazazi wapya walio makini kuwa linda watoto wao wachanga huweka kwa wageni wote wanao watembelea.

Unaweza kosa kuwaambia watu siku unayo tarajia kujifungua, kuwaambia asiye pata chanjo hata ruhusiwa kuona mtoto.

Afya yako ya kiakili

Kulingana na takwimu, idadi kubwa ya wanawake huugua kufilisika kwa mawazo wanapo jifungua. Ni kawaida kuhisi kuwa hauna nishati baada ya kujifungua. Lakini ukizidi kuhisi hivi kwa muda, hakikisha kuwa unawasiliana na mtaalum wa afya umweleze unavyo hisi. Kuwa na utangamano mzuri na mtoto wako hakuta fanyika baada ya siku moja, kutachukua muda. Na wazazi wa kiume pia wana hitaji msaada pia. Mmoja kati ya wanaume 20 hushuhudia kufilisika kimawazo wachumba wao wanapokuwa wajawazito. Na mmoja kati ya 10 hutatizika na mawazo mengi baada ya mtoto kuzaliwa.

Mabadiliko ya mwili baada ya kujifungua

mama anaye tarajia

Ni muhimu kwa mama anaye tarajia kufahamu kuwa mwili wake utabadilika sana baada ya kujifungua. Ila asiwe na shaka kwani ata upenda mwili wake mpya. Na kama utaongeza uzani mwingi, utazidi kukata kilo unapo mnyonyesha mtoto wako.

Chanzo: WebMD

Soma PiaJinsi Ya Kuongeza Nafasi Zako Za Kujifungua Msichana Mrembo

Written by

Risper Nyakio