Ishara Za Mama Mkwe Mwenye Wivu Na Jinsi Ya Kukabiliana Na Tatizo Hili

Ishara Za Mama Mkwe Mwenye Wivu Na Jinsi Ya Kukabiliana Na Tatizo Hili

Ndoa ni safari nzuri ambayo kila mwanamke ama mwanamme anatamani na kila mtu ana sababu kwa nini angependa kuoa ama kuoana. Pia kuna wale ambao wanaogopa kufunga pingu za miasha kwa sababu zao za kibinafsi. Kwa wengi wetu walio kulia kwa familia za kitamaduni ambapo huenda nyanya zetu wali waonea wivu wazazi wetu, huenda wasichana wengi wakaogopa kuolewa kwa sababu hii. Ila makala haya yana nia ya kuangazia mama mkwe mwenye wivu, ishara zake na jinsi ya kukabiliana na tatizo hili ili kuwa na familia yenye furaha.

Ishara Za Mama Mkwe Mwenye Wivu Na Jinsi Ya Kukabiliana Na Tatizo Hili

Ni vigumu kuishi kwa nyumba ambapo hamsikizani na mama mkwe wako kwani huenda kukawa na vurugu, chuki na hisia nyingi fiche kati ya wawili wenu. Kwa sababu hii, ni vyema kwa mke aliye oleka kwa familia fulani kuhakikisha kuwa wana sikizana na mama mkwe wake. Pia ni jukumu la mama mkwe kuhakikisha kuwa bibi ya mvulana wake anahisi anapendwa na kuwa ako nyumbani anapo stahili.

Mama Mkwe Mwenye Wivu Hudhibitisha Ishara Kama Zipi?

mama mkwe mwenye wivu

Utajua kuwa una mama mkwe mwenye wivu iwapo anafanya baadhi ya mambo haya:

  • Kutaka kujua kila kinacho endelea katika maisha yenu ya kibinafsi na kutanga kuingilia uamuzi mnao fanya wa mambo tofauti.
  • Iwapo ana kasirika bwanako anapo kuwa nawe wakati mwingi na mara nyingi kutaka kijana wake ashinde naye.
  • Anajaribu kubadili uamuzi wa bwanako na kumtaka afanye anacho ona kinafaa.
  • Kujaribu kuleta tofauti kati yako na bwanako.
  • Kuona kana kwamba kila kitu ni mashindano kati yako naye.
  • Wakati wote kuongea kukuhusu kwa kijana wake.
  • Hataki uhusishwe katika kufanya maamuzi ya pesa nyumbani mwako.

Jinsi Ya Kuwa Na Utangamano Na Mama Mkwe Mwenye Wivu

mama mkwe mwenye wivu

Kukorofishana na mama mkwe wako kutaleta tofauti zaidi kwenye familia yako. Njia bora zaidi ya kuepuka vita vya kila mara na wivu kati yenu ni kwa kuhakikisha kuwa mna tatua tofauti zenu na kujaribu kutangamana.

Elewa hisia zake

Huenda kuwa mama mkwe wako hafanyi mambo yake jinsi ambavyo umezoea. Ila kumbuka kuwa kila mtu ana njia yake spesheli ya kufanya vitu vyake. Kwa hivyo jaribu kadri kuto kasirika anapo fanya mambo yake kivyake. Pia elewa hisia zake kwani hapo mbeleni hakuwa amezoea kumwona kijana wake akiwa na mtu mwingine kwa muda mrefu. Ila usiwe na shaka kwani atazoea kuwepo kwako.

Msikize anacho kisema

Huenda ikawa kuwa mama mkwe wako ana hisia na fikira nyingi anazo kumbana nazo na anacho hitaji katika wakati huu ni mtu wa kuongea naye tu. Kitu bora zaidi ambacho unaweza fanya ni kumpa wakati wa kuchakata hisia zake. Anapo ongea, zungumza naye kwa upole na utulivu. Huenda kuzungumza huku kuka tatua matatizo mliyo nayo kati yenu.

Mwombe ushauri

Ishara Za Mama Mkwe Mwenye Wivu Na Jinsi Ya Kukabiliana Na Tatizo Hili

Mara kwa mara, mhusishe kwa mambo ya familia yako, sio wakati wote, ila mara moja moja unapo hisi kuwa ungependa kushauriwa kuhusu jambo fulani. Enda kwake umwulize akuongoze jinsi ya kukabiliana na matatizo tofauti.

Sifu utangamano alio nao na kijana wake

Huenda ikawa kuwa hofu yake kuu ni kuwa utafanya kijana wake asiwe na wakati na mamake ama hata kuvurugu uhusiano ulio kati ya wawili hao. Itakuwa bora zaidi kwako kumwonyesha kuwa unaelewa uhusiano alio nao na mvulana wake ana kuwa utadumu milele.

Mnunulie zawadi

Kila mama ana penda zawadi. Na haijalishi muda wako ama watoto ulio nao. Kwani, mama hata akizeeka, mara kwa mara anahitaji kutuzwa na kupelekwa kufanya mambo yanayo mfurahisha.Mnapo kuwa mkifanya shughuli zenu, mtaongea na kuwa na mazungumzo kuhusu mambo tofauti kutawasaidia kutatiza tofauti zenu. Unaweza mwuliza bwanako kuhusu vitu ambavyo mamake anapenda na unaweza enda kumnunulia.

Ishara Za Mama Mkwe Mwenye Wivu Na Jinsi Ya Kukabiliana Na Tatizo Hili

Kumbuka kuzungumza kuhusu kinacho kusumbua

Mazungumzo ya mara kwa mara yata wasaidia kutangamana vyema. Hasa katika kipindi hiki kwani mnaishi karibu. Kwa njia hii huenda mkawa marafiki wakuu!

Epuka vita na vurugu

Ukigundua kuwa na mambo ambayo mama mkwe wako hapendi kufanya, vikifanywa ama hata kuongea kuvihusu, ni vyema kuepuka mijadala hiyo. Fanya kadri uwezavyo ili kuwa na uhusiano mwema na wenye afya na mama ya bwanako.

mama mkwe mwenye wivu

Hakikisha kuwa unaongea na mume wako kuhusu hisia zako na mambo ambayo unahisi kana kwamba yana sababisha tofauti kati yako na mama mkwe wako.

Read Also: “I thought motherhood would be a mix of ice-cream and dodo

Written by

Risper Nyakio