Kudumisha ndoa yenye afya na furaha kunahitaji juhudi nyingi. Lazima tufikirie tunavyo husiana na mchumba wetu ili ndoa ifuzu. Hata kama wanaume hufanya mambo haya kwa wake zao, wanawake wana nafasi zaidi za kufanya mambo haya hasi katika ndoa ambayo yanaweza kuathiri uhusiano na ndoa yao.
Mambo Hasi Katika Ndoa

- Kuwa hasi wakati wote
Wanaume wanatengenezwa na kipawa cha kutengeneza mambo, na iwapo yote unayofanya ni kuteta, huenda mchumba wako akahisi kuwa wewe ni mzigo kwake. Sote huwa na siku ambapo hatutaki kufanya chochote. Lakini siku hizi zinapo ongezeka na kuwa muda mrefu, ni muhimu kujaribu kudhibiti hisia zako. Unapohisi kuwa hisia hizi na uchovu na kukasirika zinadumu kwa kipindi kirefu, ni wakati wa kuwasiliana na mtaalum.
2. Kuto mpa mume wako kipau mbele
Wanawake hupenda wanaume wao wanapowapatia kipau mbele. Kwa njia sawa, anafurahia unapompa kipau mbele. Usiingie katika mtego wa kupuuza ndoa yenu na kupatia watoto na kazi kipau mbele. Mpatie mume wako kipau mbele na mengine yote yatafuata.
3. Kumlaumu mambo yanapo enda mrama
Ikiwa ndoa yenu inafuata mtindo wa kitamaduni, mume wako ndiye mtu mwenye mamlaka. Hakuna kitu kibaya na mume wako kuchukua usukani na uongozi wa familia. Lakini unapomlaumu mume wako mambo yanapoenda mrama, huenda ukakwaza uhusiano wenu. Usipokubaliana na maoni yake, ni vyema kukaa chini na kujadili kisha kufanya uamuzi ulio bora kwenu nyote.

4. Kumsumbua mara kwa mara
Kusumbua huja kiasili kwa wengi wetu tunao amini kuwa tusipo sumbua, hatutapata matokeo tunayo yataka. Kufanya hivi kwa muda kunamfanya mchumba wako akasirike na kuto wasiliana nawe kwa njia wazi. Na kuanzisha matatizo mengi katika ndoa yenu.
5. Kuto mwonyesha mapenzi
Kumnyamazia mume wako kwa muda na kutomwonyesha mapenzi sio vyema. Huenda ukadhani kuwa kufanya hivi ni njia ya kumfanya ajue unachohisi, mbali sio vyema. Ukiwa na tatizo na mume wako, ni vyema kuzungumza kwa uwazi.
6. Kuishi maisha ya gharama ya juu kuwaliko
Mume wako huenda akashindwa kukununulia mkoba ambao umekuwa ukitamani kwa muda mrefu. Lakini ikiwa anajizatiti kuwapa mahitaji yenu ya kimsingi na maisha mema, kuwa na shukrani. Jaribu uwezavyo kuishi maisha katika bajeti yenu.
Soma Pia: Kufanya Ndoa Ifuzu: Kuboresha Ndoa Kwa Wanandoa Wanaofanya Kazi