Mambo muhimu ya kuiga kutoka kwa hayati rais mstaafu Daniel Moi

Mambo muhimu ya kuiga kutoka kwa hayati rais mstaafu Daniel Moi

Hayati rais mstaafu Daniel Toroitich Arap Moi alizaliwa mkoa wa Rift Valley na baadaye kujiunga na shule ya Africa Inland Mission kabla ya kujiunga na chuo kikuu kusomea ualimu. Alianza siasa mwaka wa 1995. Baada ya nchi ya Kenya kupata uhuru mwaka wa 1963, alipewa cheo cha kuwa makamu wa rais na aliye mkuu wa nchi, hayati rais Kenyatta. Safari yake ya kuwa rais wa nchi ilianza mwaka wa 1978. Na akaiongoza nchi kwa miaka ishirini na minne (24).

Katika uongozi wake, nchi ilikuwa na chama kimoja cha KANU na watu hawakukubalishwa kuanza wala kujiunga na vyama vingine.

hayati mzee moi

Familia ya hayati rais Moi

Rais Moi alifunga pingu za maisha na Bi. Lena mnamo mwaka wa 1950 hadi walipo achana mwaka wa 1974 kabla ya kuchaguliwa kuwa rais wa Kenya. Baada ya harusi yao walio unganishwa katika kanisa la AIC mission Eldama Ravine, Lena aliitupilia mbali kazi yake ya ualimu na kuwa mama wa kukaa nyumbani ili aikuze familia yake. Hayati mzee Moi alikuwa na watoto wanane, wavulana watano na mabinti watatu. Miongoni mwao wakiwa Gideon Moi, marehemu Jonathan Toroitich, Philip Moi, marehemu William Tuitoek, Jennifer.

Mambo ya kuigwa kutoka kwa maisha yake

Rais Moi anajulikana kwa mambo mengi hasa kwa kuiongoza nchi ya Kenya kwa miongo miwili na miaka mingine mine. Kando na kuwa kiongozi mwema wan chi, kuna mambo mengi ambayo wazazi wa kisasa wanaweza iga kutoka kwa marehemu rais mstaafu rais Moi.

 • Alikuwa mpenda watoto. Kando ya kuwa kiongozi wan chi aliye wapenda watu aliowaongoza alikuwa mpenda watoto sana. Kuna kisa ambacho alikuwa akipita barabarani na kusikia watoto wakishangilia na kumwita jina lake. Aliyasimamisha magari yaliyokuwa yakimsindikiza na kuwapa watoto wale kila mtu vitamu tamu. Kisha kum zawadi mama yao aliyekuwa akilima na kitita cha pesa. Aha! Kweli, rais ya kufurahia huyu alikuwa. Ni muhimu kwa kila mzazi kuwa penda watoto na sio wake tu, ila watoto wote hata wa jirani na kuwahimiza kuishi kwa pamoja kana kwamba watoto wa mama mmoja.
 • Alipenda kuwa zawadi watu. Hayati rais mstaafu Moi, alikuwa yuwapenda kuwa zawadi watu. Watu wanakumbuka kwani kila mara alipo tembelea shule tofauti nchini, baada ya kumburudisha na nyimbo alizo penda, aliwa zawadi kwa kuwanunulia basi la shule. Ni jambo njema kwa wazazi wa kisasa kusoma. Kuwazawadi watoto kwani unawahimiza na kuwapa motisha waendelee kufanya matendo mema.

marehemu rais mstaafu

 • Alikuwa makini wa kusikiza. Hata baada ya serikali yake kujaribu kupinduliwa, hakuifunga milango ya ofisi yake na kusema kuwa hata shughulikia matakwa ya watu. Ila, aliendelea kusikiza watu walio kuja kumtembelea. Alipenda kusikia maoni ya watu mbali mbali na kufanya maamuzi baada ya kuangazia maoni tofauti aliyo pewa. Jambo hili lilimfanya kuteua kiongozi wa wanawake ili kuhakikisha kuwa nchi ya Kenya haikuwa imeachwa nyuma katika kuzingatia haki za wanawake. Naam, ni jambo la kuigwa na kila mzazi. Kuwasikiza watoto wake na kuhakikisha kuwa punde tu wanapo kabiliwa na matatizo yoyote yale, wako huru kuongea na wazazi wao. Kwa kweli, hayati rais ata kumbukwa kwa kuwa mfano wa kuigwa.
 • Muomba msamaha. Rais Moi alipokuwa yuwa staafu na kumwachia rais Kibaki usukani wan chi, alisimama kwenye jukwaa na kuwa bubuwaza wengi alipo omba msamaha kwa yeyote yule aliyekosea. Alisema “ kama iko mtu nimekosea yeye, naomba anisamehe, na kama iko mtu nimekosea, na mimi namsamehe”. Viongozi wangapi wangelifanya hili? Wachache sana iwapo kunao. Aliwaacha watu bila ya kusema baada ya maneno yake haya. Naam, wazazi wa kuigwa wanapaswa kufuata mfano huu wa rais na kuwa waomba msamaha. Hata kwa watoto wao iwapo wamewakosea, wasiwe na aibu kusema na kukubali wanapo kosea. Wana wahimiza watoto wao kufuata nyayo zao na kuwa wanyenyekevu.
 • Kiongozi mwema. Rais Moi aliushikilia usukani wan chi kwa miaka 24. Sio miaka michache na inahitaji juhudi nyingi kuwaongoza watu wa tabaka mbali mbali na kuhakikisha kuwa nchi inakua. Ni jambo ambalo wazazi wanapaswa kufuata na kuushikilia usukani wa nyumba zao. Kuhakikisha kuwa mambo yote yako shwari na hamna yanayo enda mrama.
 • Alikuwa makini. Katika baraza lake la mawaziri, kila waziri alikuwa makini kwa kazi aliyo takikana kufanya. Iwapo waziri wa wizara Fulani alikosa kutimiza wajibu wake, bila shaka angepata amepigwa kalamu bila ya ufahamu wake. Pia wakati wa hayati Moi, ilikuwa ni lazima kwa kila waziri kutazama shajara kila siku. Ili kujua yaliyo kuwa yakitendeka. Ungejua iwapo umepigwa kalamu ama umepewa cheo kikuu kupitia kwa habari za kila siku. Ni muhimu kwa wazazi kuhakikisha kuwa wako makini hasa katika maisha ya watoto wao ili kuwapa ushauri wakiona wanakosea.

Mambo muhimu ya kuiga kutoka kwa hayati rais mstaafu Daniel Moi

Urithi wa marehemu rais mstaafu

Rais Moi atakumbukwa kwa mengi ila kuna mambo na taasisi alizo anza ambazo zitaliendeleza jina na urithi wake. Baadhi ya taasisi kama hizi ni kama vile vyuo na hospitalini kama:

 • Moi Teaching and Referral Hospital
 • University of Moi- Eldoret
 • The Moi International Sports Centre-Kasarani
 • Moi Air Base, Nairobi
 • Moi Stadium Kisumu
 • Nairobi na Mombasa, Moi Avenue

Hayati marehemu rais mstaafu atakumbukwa kwa mengi. Ni vyema wazazi na viongozi wachambue uongozi na maisha yao na vitu muhimu vya kuigwa kutoka kwa kiongozi huyu. Maombi yetu ni kuwa Mola amlaze mahali pema peponi, na aendelee kuifariji familia na nchi kwa kumpoteza kiongozi mkuu.

Read also: Wanaume Hawa Kutoka Kenya Waelezea Ufarisi Wao Na Mipango Ya Kando Na Umuhimu Wake

Written by

Risper Nyakio